Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

Bila uchochezi now watakuja 'kumbeba huyo baadae'
sasa ndo wasimuonee haya..
haya yanatokea kwa mtu ambayo yupo very close na mimi.....
babake alikuwa anajulikana mji mzima kwa hela, watoto wake walikuwa wanatembea kwenye magari tu, enzi hizo ambazo umiliki wa baiskeli ulikuwa shida. alibahatika kuwa na mtoto mmoja (nje ya ndoa), ambaye kwa sababu alikataliwa na baba na mama wa kambo basi alijisomesha ili angalau aweze kujikwamua kimaisha.
wale watoto wa ndani walikuwa na starehe tu kiasi kwamba hakuna aliyekumbuka shule.
huwezi amini kwa sasa huyo mtoto aliyekataliwa ndo anahudumia ukoo mzima, kuanzia baba/mama aliyemkataa, watoto wa watoto wao ambao walikataa kwenda shule, na watoto wa mzee ambao bado wanaenda shule......
na sasa mzee sababu anaona mwanaye alishasamehe na kuamua kuhudumia "familia" yake basi ameanza kudai haki yake kama mzazi, anatamka kabisa kuwa nahitaji kiasi hiki kwa mwezi..... bila aibu
 
Mkuu ujamaa uliisha mwishoni mwa miaka ya 1980, na scrappers za kutoka Japan zikaanza kumwagika....Na pia wapo watu kibao ambao waliishi kipindi hicho lakini walijitutumua kiasi kwamba huwezi kuwasikia wakilia lia ....

Nadhani uchambuzi wa kina unatakiwa ili kuwatendea haki wote ... And this is what we are trying to reflect on!!

Babu DC!!

sawa kabisa je maumivu yaliyo baki nyuma..??sinahakika kama ujamaa ulikoma 1980 au baada ya hapo, maana 1980 ndo kipindi cha machungu ya vita ya Kagera,kingine hata kwa wakati wao muziki haikuwa ajira rasmi na wezakusema na ilitumika kama kiburudisho tuu katika sherehe za chama na kitaifa pia na kuwaliwaza wananchi baada ya kazi.Hawa wazee waliishia kupata sifa tu nadhani kama unakumbukumbu hapo kabla wakati bongo fleva inaanza mfumo kama huo ulikuepo,unakuta mtu jina kubwa hana kitu zaidi ya sifa za kupewa bia za bure,kuitwaitwa mitaani na kupewa madem wakali mtaani
 
Enzi za Nyerere mashamba ni unaomba tu unakatiwa lako
watu wengi walinunua mashamba ambayo now ni viwanja
kama mtu kama Gurumo alipewa 'elfu ishirini' asingeulizwa kununua nyumba moja au mbili
Mbona Filbert Bayi na Bakhresa walianza enzi hizo hizo?

Mi viwanja ambavyo mshua kaniachia (yeye aliviwahi enzi hizo za 47) leo nikiamua kuviuza tu tayari bilionea :smiling:.

Sasa mzee Gurumo yeye alikuwa wapi aka hizo asiwahi hivyo viwanja? Manake kuanzia Sinza huku hadi huko Mikocheni enzi hizo yalikuwa mapori mapori tu na Dar ilikuwa ni kama tupu tu.

Watu tulikuwaga tunaenda Mikocheni kuchuma mabungo na kuwinda ndege. Lakini vipori vyote vya enzi hizo (na hapa nazungumzia miaka ya 80 tu) havipo tena.
 
Jamani mnapoyasema yeye msimsahau na Mungu wote tungekuwa kama daimond nan angekuwa ngurumo?kumbukeni kwamba jitihada zako pekee hazishindi kudra za MUNGU.simtetei ngurumo wala simlaumu kila kitu kinasababu yake............

Hoja yako ingekuwa na uzito mkubwa sana kama yeye mwenyewe asingetoka hadharani kulalamika na kulaumu serikali kwa hali aliyonayo sasa.

Ina maana yeye hana mchango kwa kile kinachompata sasa??

Babu DC!!
 
Hebu piga picha halafu umwone mheshimiwa anafuta machozi eti serikali imeshindwa kukulinda ukaibiwa na wajanja wa JF....

Haki ya nani Maxi lazima atiwe misuko suko...lol!!

Babu DC!1
umeona eeehhhh!
yaani mtu anashindwa kutimiza wajibu wake halafu anasingizia serikali.... tuwe serious jamani.....
sasa mzee sijui atapeleka mashtaka yepi? maana naibiwa jf, fb,tweeter, yahoo, hotmail........ si serikali itapata kichaa?
 
Mi viwanja ambavyo mshua kaniachia (yeye aliviwahi enzi hizo za 47) leo nikiamua kuviuza tu tayari bilionea :smiling:.

Sasa mzee Gurumo yeye alikuwa wapi aka hizo asiwahi hivyo viwanja? Manake kuanzia Sinza huku hadi huko Mikocheni enzi hizo yalikuwa mapori mapori tu na Dar ilikuwa ni kama tupu tu.

Watu tulikuwaga tunaenda Mikocheni kuchuma mabungo na kuwinda ndege. Lakini vipori vyote vye enzi hizo (na hapa nazungumzia miaka ya 80 tu) havipo tena.

watu hupenda tu kusingizia serikali kwa uzembe wao
 
sawa kabisa je maumivu yaliyo baki nyuma..??sinahakika kama ujamaa ulikoma 1980 au baada ya hapo, maana 1980 ndo kipindi cha machungu ya vita ya Kagera,kingine hata kwa wakati wao muziki haikuwa ajira rasmi na wezakusema na ilitumika kama kiburudisho tuu katika sherehe za chama na kitaifa pia na kuwaliwaza wananchi baada ya kazi.Hawa wazee waliishia kupata sifa tu nadhani kama unakumbukumbu hapo kabla wakati bongo fleva inaanza mfumo kama huo ulikuepo,unakuta mtu jina kubwa hana kitu zaidi ya sifa za kupewa bia za bure,kuitwaitwa mitaani na kupewa madem wakali mtaani

Mkuu, sijasema kuwa ujamaa uliisha mwaka 1980 bali nimesema kuwa ilikuwa mwishoni mwa miaka ya 1980!

Nadhani hapo mwisho umeeza tu kuwa wengine vipau mbele vyao vilikuwa hapo...!!

Babu DC!!
 
haya yanatokea kwa mtu ambayo yupo very close na mimi.....
babake alikuwa anajulikana mji mzima kwa hela, watoto wake walikuwa wanatembea kwenye magari tu, enzi hizo ambazo umiliki wa baiskeli ulikuwa shida. alibahatika kuwa na mtoto mmoja (nje ya ndoa), ambaye kwa sababu alikataliwa na baba na mama wa kambo basi alijisomesha ili angalau aweze kujikwamua kimaisha.
wale watoto wa ndani walikuwa na starehe tu kiasi kwamba hakuna aliyekumbuka shule.
huwezi amini kwa sasa huyo mtoto aliyekataliwa ndo anahudumia ukoo mzima, kuanzia baba/mama aliyemkataa, watoto wa watoto wao ambao walikataa kwenda shule, na watoto wa mzee ambao bado wanaenda shule......
na sasa mzee sababu anaona mwanaye alishasamehe na kuamua kuhudumia "familia" yake basi ameanza kudai haki yake kama mzazi, anatamka kabisa kuwa nahitaji kiasi hiki kwa mwezi..... bila aibu

Umeona sasa
mtu ananunua magari wakati mashamba yanauzwa angenunua hata eka 1000
leo angekuwa mbaali
kabaki kulaumu watu tu
 
The Boss, unaongelea topic ambayo naiogopa kuliko zote. Najiuliza kila siku, when is it the right time kufanya hizo investments basi? Manake kila hela ninayopata inapata matumizi yasiyo ya msingi. Kuna kujispoil (wants and not needs, lara 1 keshatuzodoa), holidays na michango ya harusi, ndugu wasiotaka kuwajibika na uwiii!
Hayo majumba najenga lini? Hizi hela nilizonazo ndo ntakuja kuzijutia wakati saa hizi hazinitoshi?
Mbu njoo rafiki
ni swala la kujua tu malengo yako. pamoja na kila kitu unachotaka kujifanyia/kufanyia watu, unatakiwa kujua mwisho wa siku wewe unataka nini.
huwa nawatimuaga ndugu zangu ambao wao na mimi wote wafanyakazi, wao inapofika muda wa kulipa ada ya shule ya mwanaye anakuja kwako kukuambia anaomba msaada hana hela ya ada, hali kadhalika inapofika kulipa kodi ya nyumba.
Huwa najiuliza hiki kitu hakijatokea ghafla, mtu unajua kabisa mwezi fulani nalipa ada/kodi kiasi fulani. Mshahara wako kwa miezi 2 hautoshi kulipa (usiniambie ulikuwa unategemea dili). kwa nini usianze ku-accumulate kidogo kidogo mpaka itakapokamilika? hilo deal likitokea utafanyia kitu kingine.....
 
Hapa ndipo utakapowajua wachumi wa darasani na wale wa kuzaliwa...

Halafu mtu kama huyo anakunywa bia kama vile ana complementary coupons za TBL..lol!!

Babu DC!!
 
usitake kulinganisha mindset ya tabaka la wafanyakazi la kipindi hicho na watu wachache nasema wachache mno ambao siku zote kwenye matabaka yote na kwenye mataifa yote lazima waibuke pamoja na kubana kwa mazingira yote. hawa hata kama mpo darasani mtalalamika mwalimu haji darasani kufundisha lakini wao utakuta wamescore maksi za ajabu tofauti na majority.

hebu fikiria kipindi hicho mtu akiambiwa nenda kigamboni ukanunue shamba wangapi wangekucheka na kukuona zuzu siyo tu kigamboni sehemu tu za pembezoni mwa mji kimara tegeta miaka hiyo nani angeweza kuona kuwa ardhi ingepanda thamani kama ilivyo leo.

mindset ya wafanyakazi wa kijamaa ilikuwa ngumu mno kutengeneza mindset ya maentrepreneurs wawekazaji wenye kuangalia mambo miaka ishirini au kumi na tano inayokuja.

maisha yalikuwa ya mla mla leo mshahara unatosha matumizi na vijisavings vya kupelekea watu vijijini. tusiwalaumu sana. ila walifanya kazi ya kulijenga taifa kwa nyimbo zao. walihamasisha elimu dhidi ya magonjwa kilimo ufugaji uzalendo kupigana vita ya kutetea hadhi ya nchi. mbaya zaidi hawakuwa na pension scheme au life insurance scheme wanazojivunia vijana wa leo waliopo tanzania na nje ya nchi.
 
Hapa ndipo utakapowajua wachumi wa darasani na wale wa kuzaliwa...

Halafu mtu kama huyo anakunywa bia kama vile ana complementary coupons za TBL..lol!!

Babu DC!!

Mkuu mimi nina Babu yangu mmoja
watoto wa nyumba ndogo na wa ndugu wa mbali aliwasomesha hadivyuo na kuwatafutia na kazi
watoto wake wote darasa la saba
yeye alikuwa manispaa ana cheo
kauza viwanja vya manispaa yeye akajenga nyumba yake moja tu
kafa lofa na hakuna watoto wa kumsaidia...
 
well said. tujifunze kuwekeza ktk maisha y baadae tho ha2jui cku ye2 ya kufa
 
Mara zote maendeleo ya mtu mmoja na namna awazavyo ndivyo unavyoweza kupata taswira ya maendeleo ya Taifa fulani.
Tukionacho kwa Mzee Gurumo sasa hivi si jambo geni sana maana ni wazee wengi tu wa zamani ambao nao wapo dhoofu ili hali pamoja na kwamba walikuwa na fursa za kutosha.
Sababu ya kufikia hapo walipo ni kwamba fursa walizozipata hawakuzitumia kwa manufaa ya kiuchumi(fikra dumavu)....hawakubadili ulimwengu wa umaarufu kuwa ndio mpenyo wao kiuchumi
 
Kinacho shangaza ni kuwa bado hawaoni walipokosea
wao still 'hawakukosea'
ni kurusha tu lawama
 
Umenikumbusha!

Leo tulikuwa na mjadala hapa maeneo ya kazi

Kuna jamaa walikuwa wanadai kuna watu "wamepangiwa" kukosa na wengine kupata,nikawauliza kuhusu walipotoa huo mtazamo wao hawakuwa na majibu ya kuridhisha kabisa wakabaki wananiambia tu eti Mungu ndie anaepanga nani apate nini na kwa kiasi gani

Nilichowaambia mimi ni kuwa watu kama hawa ndio wanafanya watu waendelee kuwa maskini hasa watoto wao wanaowalea,wanawafanya wabweteke bila kujibidiisha kikazi na kifikra

Pia wanataka kumfanya Mungu aonekane ni mwenye upendeleo wa kuwapa wengine nyingi na wengine kidogo jambo ambalo sio kweli

Nijuavyo mimi Mungu hapangi nani apate na nani asipate ila ameweka kanuni ambazo kila atakaezifuata na kuzitii na pia kufanya kazi kwa bidii kwa uangalifu na kutumia akili kwa kiwango chake atapata kwa kiwango hicho,haya mambo ya kukaa na kudanganyana eti Mungu hajanipangia kuwa tajiri ni maneno ya kivivu na ni maneno ya kukemewa kwa nguvu zote

Wazee kama hao uliosema hapo wamevuna kwa kiwango chao kama walichezea watakula kuchezea hoko,Mungu sio boi wako wa kufix mistake zako tena nyingi za kijinga unazozifanya kila uchao

Ukiwa mhongaji utavuna uhongaji!!!!!!!
 
Back
Top Bottom