tatizo la nchi ni kutokuwa na Social Security ya nchi nzima ambayo kila mtu mwenye kufanya kazi na kulipwa mshahara akatwe kiasi fulani ya mshahara wake ili akistaafu basi apate na yeye anachostahili kipindi cha uzee wake. ule utamaduni wa kuwa na bima kwa kuzaa watoto wengi uliingia shubiri baada ya magonjwa na mfumo wa maisha ya mjini. kwa nini tusiwe na mfuko mmoja wa pensheni wa bima ya afya?
Mzee kama huyu ambaye amefanya kazi miaka hamsini na kama angekuwa amechangia kwa miaka yote hiyo leo kwenye mfuko wa pensheni leo angekuwa anakula pensheni yake vizuri tu. fikiria tu shilingi ya miaka sitini leo ingekuwa na thamani ya kiasi gani.
Tupiganie tuwe na social security ambayo mtu awe house girl ,mlinzi ,mwanamuziki ,mhasibu ,bar maid , changudoa , mhandisi achangie mpaka akifika muda wake wa kustaafu kufanya kazi aweze kujilkimu maisha. Hii itapunguza adha nyingi kwa wazee waliofikia muda wa kustaafu.
unajua unaweza ukawekeza vitega uchumi binafsi vikaja kudondoka au ukaweka fedha benki ikaja dondoka lakini ukiwa na Social Security ambayo na ya nchi nzima ina uwezo mkubwa wa kudiversify risk na ikawa madhubuti.
sijui hata kama kwenye katiba imendikwa ni haki ya kimsingi kwa kila mwenye uwezo wa kufanya kazi kuchangia kwenye social security na kupata mafao yake anapostaafu kazi au anapopata ulemavu wa kutofanya kazi au anapokuwa hana kazi sababu kazi hazipatikani.