Wanasiasa wengi hawajawekeza kwenye sekta ya Afya ndo maana wanaruhusu huu uhuni wa NHIF!

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,892
3,196
Asalaam Aleykum.

Ama baada ya salamu hizo, niangukie kwenye mada moja kwa moja.

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na taharuki kwa wanufaika wa mfuko wa NHIF mara baada ya watoa huduma za Afya upande wa hospitali binafsi na zile zinazomilikiwa na Taasisi za dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kutishia kusitisha huduma kutokana na kulalamikia kitita kipya cha NHIF kitakachoanza kutumika mnamo mwezi wa kwanza 2024. Kitita hiki kimepunguza gharama za kupata matibabu (pamoja na mambo mengine), gharama za kuwaona Madaktari toka 35,000/= hadi 25,000/=, toka 20,000/= hadi 15,000/=, toka 7,000/= hadi 5,000/= n.k.

Hii kwa kweli binafsi naichukulia kama dharau ya Serikali kwa wamiliki na watoa huduma za Afya kwa sababu ya hali ya mfumko wa bei, kushuka kwa thamani ya sarafu yetu dhidi ya dola na kupanda kwa gharama za maisha kwa ujumla. Haiwezekani na haingii akilini kabisa kwamba gharama za maisha zimepanda kwa kila kitu, halafu upande wa Afya ndo gharama zishuke!

Kwa haraka haraka nafikiri hii hali imekuwa hivyo kwa sababu wanasiasa wengi wamewekeza kwenye mambo ya mafuta na usafirishaji na ndio maana huko gharama zinapanda kila uchao. Gharama za mafuta zimekuwa zinapanda kwa karibu kila mwezi, huku gharama ya nauli kwa mwaka huu unaoenda kuisha pekee zikiwa zimepanda mara 2!

Hebu wanasiasa msituharibie maana sisi tulio wengi tunategemea zaidi huduma za Afya toka hospitali binafsi kutokana na kutokutosheleza na urasimu mwingi uliopo katika hospitali za Umma (za serikali).
Nimalizie tu kwa kuweka bayana kwamba mimi si mmiliki na wala sina ubiya wowote na watoa huduma za Afya, ila nimeguswa tu na huu unyanyasaji wanaofanyiwa ilhali wana mchango mkubwa sana katika kuboresha huduma zetu wananchi ili tuwe na Afya njema, tuendeleze Ujenzi wa Taifa letu.
Naomba kuwasilisha.
 
Hiyo inaitwa mtajijua wenyewe..
Wao wanatibiwa bure, hawapati hasara kwenye biashara zao.
Haiwahusu, pambaneni na hali zenu.

Mwaka wa kuujua usanii wa wanasiasa wa bongo na tukafanya maamuzi yakinifu, ndio tutakapotupa shida chini na kubanjuka tu
 
Siyo wanatibiwa tu bure Mkuu, wakiugua kidogo tu, breki ya kwanza ni India, kama siyo Marekani kwa gharama za kodi zetu!
That is not fair.
 
Asalaam Aleykum.

Ama baada ya salamu hizo, niangukie kwenye mada moja kwa moja.

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na taharuki kwa wanufaika wa mfuko wa NHIF mara baada ya watoa huduma za Afya upande wa hospitali binafsi na zile zinazomilikiwa na Taasisi za dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kutishia kusitisha huduma kutokana na kulalamikia kitita kipya cha NHIF kitakachoanza kutumika mnamo mwezi wa kwanza 2024. Kitita hiki kimepunguza gharama za kupata matibabu (pamoja na mambo mengine), gharama za kuwaona Madaktari toka 35,000/= hadi 25,000/=, toka 20,000/= hadi 15,000/=, toka 7,000/= hadi 5,000/= n.k.

Hii kwa kweli binafsi naichukulia kama dharau ya Serikali kwa wamiliki na watoa huduma za Afya kwa sababu ya hali ya mfumko wa bei, kushuka kwa thamani ya sarafu yetu dhidi ya dola na kupanda kwa gharama za maisha kwa ujumla. Haiwezekani na haingii akilini kabisa kwamba gharama za maisha zimepanda kwa kila kitu, halafu upande wa Afya ndo gharama zishuke!

Kwa haraka nafikiri hii hali imekuwa hivyo kwa sababu wanasiasa wengi wamewekeza kwenye mambo ya mafuta na usafirishaji na ndio maana huko gharama zinapanda kila uchao. Gharama za mafuta zimekuwa zinapanda kwa karibu kila mwezi, huku gharama ya nauli kwa mwaka huu unaoenda kuisha pekee zikiwa zimepanda mara 2!

Hebu wanasiasa msituharibie maana sisi tulio wengi tunategemea zaidi huduma za Afya toka hospitali binafsi kutokana na kutokutosheleza na urasimu mwingi uliopo katika hospitali za Umma (za serikali).
Nimalizie tu kwa kuweka bayana kwamba mimi si mmiliki na wala sina ubiya wowote na watoa huduma za Afya, ila nimeguswa tu na huu unyanyasaji wanaofanyiwa ilhali wana mchango mkubwa sana katika kuboresha huduma zetu wananchi ili tuwe na Afya njema, tuendeleze Ujenzi wa Taifa letu.
Naomba kuwasilisha.
Niseme tu viongozi wetu ni wagumu mno kusikiliza. Huwezi kuweka bima ya afya wakati hujawaandaa watu Kwa cash economy, hili tumelizungumza mpaka wengine sauti zimekauka. Kwakweli governance ya nchi hii ni mtihani mzito
 
Sijui tutafanyaje Mkuu,
Maana walioshikilia mpini ni kama wendawazimu! Hawataki kuambiwa ukweli.
Anyway, tutazidi kuwaambia, wakijisikia kutukata, watukate.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom