Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,153
Hizi heka heka za mivutano baina ya serikali kupitia NHIF na watoa huduma za afya wa vituo binafsi sio jambo lenye kheri, mwisho wake utakuwa mbaya sana.
Haijarishi nani ataibuka mshindi lakini mwisho wa siku afya za watanzania zinakwenda kupuputika vibaya.
Ni kweli NHIF inazilipa fedha nyingi taasisi binafsi za afya (hivyo huendeshaji wa hizo taasisi kwa zaidi ya 50% huenda unategemea pesa kutoka NHIF) lakini ukitazama malipo ya kitita kipya cha mafao cha NHIF umejaa kasoro kubwa zenye kuzinyonya kiasi cha kuelekea kuziua kabisa taasisi binafsi. Haijarishi taasisi binafsi zitaamua kuchukua mkondo gani (kugoma au kuendelea kutoa huduma), mwelekeo wa kufa utabakia pale pale. Na ili ziendelee kuwepo na huku zikiendelea kutoa huduma, ni lazima zijipange kutoa huduma duni sana kwa wagonjwa, na huo ndio msiba wa watanzania wengi ulipo.
Hekima ilikuwa ni kukaa mezani ili kufikia muafaka.