Msimamo wa Wizara ya Afya kuhusu maboresho ya kitita NHIF 2023

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
156
108
MSIMAMO WA WIZARA YA AFYA KUHUSU MABORESHO YA KITITA NHIF 2023.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amevielekeza Vituo Binafsi vilivyoingia mkataba na NHIF Kuzingatia masharti ya Mikataba yao

Waziri ya Wizara ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu amevielekeza vituo vyote vya afya binafsi na vya umma vilivyoingia Mkataba na NHIF kuendelea kutoa huduma kulingana na Mikataba yao waliyoingia, Waziri Ummy ameyasema hayo tatehe 01 Machi, 2024 akiwa Mkoani Lindi.

"Kila mtoa huduma za afya kwa wanachama wa NHIF ameingia mkataba na NHIF, hivyo wazingatie masharti ya mikataba walioingia na NHIF katika kuwahudumia wanachama ".Mhe.Ummy Mwalimu .

1. "Napenda kutoa rai kwa hospitali zote binafsi zilizositisha kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF ziendelee kutoa huduma kwa wanachama wa NHIF"

2. "Kamati ya Kitaalam niliyoiunda iendelee kufanya majadiliano na watoa huduma wakati huduma zikiendelea kutolewa, Nasisitiza majadiliano yataendelea wakati huduma zinaendelea kutolewa" .

3. "Nazielekeza hospitali au vituo vyote binafsi na vya umma kuendelea kuwapokea wagonjwa wa dharura pindi wanapofika katika vituo vyao kwani hili ni takwa la kisheria namba 151 la usajili wa vituo binafsi vya afya na kanuni yake namba 32, kutokuwapokea wagonjwa wa dharura ni kuvunja sheria".

4. "Hatutamvumilia mtoa huduma yeyote ambaye atakiuka sheria ya kutoa huduma hivyo naomba wabadilishe matangazo yao isipokua mgonjwa wa dharura, tujikite kwenye kuwahudumia watanzania fedha Baadae.

5. Nimeona habari au tangazo wakisema watawatoa wagonjwa waliopo wodini ndani ya masaa 48 nataka kusema ni marufuku kuondoa wagonjwa waliopo wodini kwasababu kufanya hivyo ni kuvunja sheria ya madakatari".

"Jambo la Mwisho nazielekeza Hospitali zote za Serikali kujiandaa na kuweka utaratibu mzuri wa kupokea wagonjwa wengi zaidi watakaoshindwa kupata huduma kwenye Vituo binafsi na kuwahudumia hasa kipindi hichi" .

Aidha Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa kusimamia maelekezo ya Serikali.
 
Back
Top Bottom