Wizara ya Afya, NHIF na siasa kwenye afya

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
221
528
Ukisikia wasomi wa Afrika kushindwa kutumia maarifa kutatua changamoto zinazoikabili jamii, hili la NHIF, wizara ya afya na wamiliki wa vituo binafsi ni mfano tosha wa kufeli kwa wasomi wetu

NHIF iliwahi kulalamikiwa na waziri mwenye dhamana ya afya kwa ubadhilifu wa michango ya wanachama. Kwamba wafanyakazi wa NHIF wanajikopesha sehemu kubwa ya michango bila kufanya marejesho

NHIF waliwahi kulalamika hadharani kuwa vituo vya afya vya binafsi vinazidishi gharama sana zaidi ya gharama halisi alizohudumiwa mgonjwa

Pia NHIF hao hao wakalalamikia wanachama wao kuwa kadi moja inaweza kutumika na zaidi ya mgonjwa mmoja

Hoja ya wafanyakazi wa NHIF kujikopesha kiasi kikubwa cha michango pasipo kufanya marejesho haijawahi kujibiwa wala kuchukuliwa hatua

Hoja ya vituo binafsi kuzidisha gharama zaidi ya ile aliyohudumiwa mgonjwa hili liko wazi kwa baadhi ya vituo. Hatua hazijawahi kuchukuliwa kwa vituo hivyo

Mabishano yanayoendelea kati ya serikali na wamiliki binafsi ni matokeo ya mfuko wa NHIF kuzidiwa nguvu kwa vyote. Hawana mifumo madhubuti ya kudhibiti mapato yao na hawana mifumo madhubuti ya kudhibiti matumizi yao

Kwanini NHIF inakimbilia kupunguza gharama za huduma badala ya kutatu hoja zilizowahi kuibuliwa??

Hoja pekee waliyojaribu kufanyia kazi ni kudhibiti matumizi ya kadi kwa zaidi ya mtu mmoja. Hili limewaongezea gharama za uendeshaji kwasababu wamelazimika kuajiri watu wao watakaofanya kazi hiyo kwenye baadhi ya vituo binafsi hivyo hapa hakuna walichookoa

Vituo binafsi vinapata kiburi cha kuja hadharani na kutishia kuwafukuza wagonjwa wa NHIF waliomahututi baada ya saa48 kwasababu wanajua serikali haina uwezo wa kuhudumia wananchi wake wote vizuri

Kwanini wanapata hiki kiburi? Kauli kama hizi za kuwafukuza wagonjwa wa NHIF unaweza kuitafsiri kama kufanya mauji hadharani huku wakiamini serikali haina cha kuwafanya. Endapo serikali itaruhusu hali hii itokee itakuwa imekiri udhaifu mkubwa sana na huku ni kumchezea simba sharubu

Wanaoifilisi NHIF ni vituo binafsi na wafanyakazi wa NHIF wenyewe halafu vitisho vinakuja kwa wachangiaji.

Je, hii ni kwamba wachangiaji wa NHIF hawana mtetezi? au Mtetezi wa wanachama wa NHIF hana nguvu dhidi ya vituo binafsi vilivyosaini mkataba wa kuhudumia wanachama hawa?

Imefika hatua sasa wananchi tujifunze namna ya kudai haki zetu kwa nguvu.

Hizi sarakasi haziwaumizi vituo binafsi wala NHIF wala serikali, zinawaumiza wanachama wa NHIF. Hivi mchangiaji atakayefariki kwasabau ya sakata hili, NHIF, serikali au hivi vituo binafsi vitaweza kurudisha uhai wake pale watakapokuwa wamemaliza migogoro yao? Watarudisha maisha ya wagonjwa waliowapoteza kwa makusudi? Hivi ndivyo taaluma zao zinavyoeleleza??

Kwa nchi yenye wananchi na serikali inayojitambua, mkurugenzi wa NHIF, mwenyekiti wa Bodi ya wamiliki wa vituo binafsi na waziri wa afya walitakiwa wawe lockup wanatafutia ufumbuzi huko sio kulala usingizi mnono wakati wagonjwa wa NHIF wanasubiri kufukuzwa kutoka vituo binafsi baada ya saa48
 
Ummy Mwalimu hovyo kabisa, ile wizara imemshinda. NHIF ina matatizo makuu mawili,

1. Matumizi mabaya ya fedha za mfuko kwa shughuli za 'utawala'

2. Udanganyifu wa watoa huduma za afya

Jawabu la matatizo yote haya sio kitita kipya. Hilo la kitita ni uhayawani mtupu. Yaani gharama za maisha zipate ila unalazimisha hospitali zishushe bei? Huu si upunguani huu?
 
Mpendwa hiyo ndiyo ilani ya chama chako pendwa CCM inavyotekeleza ilani yake.
 
1709234143885.jpeg
 
tuache ubabe, serikali ikae na washika dau wayajenge...... mchango wa sekta binafs kwenye afya za watz ni kubwa sana, serikali kwenye iwe mlezi na sio mbabe
 
Kuna mambo ukikaa uakatulia ukayafikiria unaweza ukajikuta unacheka mwenyewe halafu watu wakakuona umeanza kuwa chizi au hamnazo kabisa. Kwa taarifa ya CAG ambayo kwa maana nyingine ni ushahidi tosha kuwa wafanyakazi wa bima ya afya wamekopeshana billioni 41 halafu wapo tu matokeo yake mfuko umeyumba mzigo tena anabebeshwa yule aliyechanga bilioni 41 ili apate matibabu.

Ukigeuka huku kiongozi mkubwa tu anatoka Dar/Dodoma na wasaidizi wake mpaka Serengeti kwenda kumkamata mhasibu mbele ya kamera aliyeiba milioni 189 huku alikotoka Dar/Dodoma kaacha wezi wa bilioni 41 (ni wezi hakuna jina jingine la kuwapa hawa) na mpaka sasa hatujawahi kuwajua wala kuwaona mbele ya kamera ni wakina nani hao. Na si ajabu wapo ofisini mpaka leo wanaendelea na kazi huku wameiachia serikali msala inapambana na wachangiaji wa bima ya afya kwa upande mmoja na watoa huduma kwa upande mwingine.

Kwa nini serikali isiwawajibishe hao waliojikopesha hizo bilioni 41 wazirudishe haraka ili ziokoe maisha ya watanzania? Kwa nini inawaogopa halafu yenyewe inapata shida kubadilisha vifurushi ambalo ndilo jambo linaleta mvurugano sasa hivi kati ya serikali na watoa huduma na anayeumia ni mtanzania masikini. Walau basi serikali itutajie hao wadeni waliokopeshwa hizo pesa za bima ya afya tuwajua ni wakina nani na kila mmoja walikopeshwa kiasi gani.
 
Ummy Mwalimu hovyo kabisa, ile wizara imemshinda. NHIF ina matatizo makuu mawili,

1. Matumizi mabaya ya fedha za mfuko kwa shughuli za 'utawala'

2. Udanganyifu wa watoa huduma za afya

Jawabu la matatizo yote haya sio kitita kipya. Hilo la kitita ni uhayawani mtupu. Yaani gharama za maisha zipate ila unalazimisha hospitali zishushe bei? Huu si upunguani huu?
Nasikia Benjamin mkapa hiyo hospital ilijengwa na NHIF lakini mpaka sasa hiyo hela haijawahi kurudishwq
 
Corruption and lack of good governance na kutokuwa na utaratibu wa accountability of sanctions and imprisonment ya wezi ndo hivy ilivyo kwa sasa kwa kila s sector Tanzania
 
Ukisikia wasomi wa Afrika kushindwa kutumia maarifa kutatua changamoto zinazoikabili jamii, hili la NHIF, wizara ya afya na wamiliki wa vituo binafsi ni mfano tosha wa kufeli kwa wasomi wetu

NHIF iliwahi kulalamikiwa na waziri mwenye dhamana ya afya kwa ubadhilifu wa michango ya wanachama. Kwamba wafanyakazi wa NHIF wanajikopesha sehemu kubwa ya michango bila kufanya marejesho

NHIF waliwahi kulalamika hadharani kuwa vituo vya afya vya binafsi vinazidishi gharama sana zaidi ya gharama halisi alizohudumiwa mgonjwa

Pia NHIF hao hao wakalalamikia wanachama wao kuwa kadi moja inaweza kutumika na zaidi ya mgonjwa mmoja

Hoja ya wafanyakazi wa NHIF kujikopesha kiasi kikubwa cha michango pasipo kufanya marejesho haijawahi kujibiwa wala kuchukuliwa hatua

Hoja ya vituo binafsi kuzidisha gharama zaidi ya ile aliyohudumiwa mgonjwa hili liko wazi kwa baadhi ya vituo. Hatua hazijawahi kuchukuliwa kwa vituo hivyo

Mabishano yanayoendelea kati ya serikali na wamiliki binafsi ni matokeo ya mfuko wa NHIF kuzidiwa nguvu kwa vyote. Hawana mifumo madhubuti ya kudhibiti mapato yao na hawana mifumo madhubuti ya kudhibiti matumizi yao

Kwanini NHIF inakimbilia kupunguza gharama za huduma badala ya kutatu hoja zilizowahi kuibuliwa??

Hoja pekee waliyojaribu kufanyia kazi ni kudhibiti matumizi ya kadi kwa zaidi ya mtu mmoja. Hili limewaongezea gharama za uendeshaji kwasababu wamelazimika kuajiri watu wao watakaofanya kazi hiyo kwenye baadhi ya vituo binafsi hivyo hapa hakuna walichookoa

Vituo binafsi vinapata kiburi cha kuja hadharani na kutishia kuwafukuza wagonjwa wa NHIF waliomahututi baada ya saa48 kwasababu wanajua serikali haina uwezo wa kuhudumia wananchi wake wote vizuri

Kwanini wanapata hiki kiburi? Kauli kama hizi za kuwafukuza wagonjwa wa NHIF unaweza kuitafsiri kama kufanya mauji hadharani huku wakiamini serikali haina cha kuwafanya. Endapo serikali itaruhusu hali hii itokee itakuwa imekiri udhaifu mkubwa sana na huku ni kumchezea simba sharubu

Wanaoifilisi NHIF ni vituo binafsi na wafanyakazi wa NHIF wenyewe halafu vitisho vinakuja kwa wachangiaji.

Je, hii ni kwamba wachangiaji wa NHIF hawana mtetezi? au Mtetezi wa wanachama wa NHIF hana nguvu dhidi ya vituo binafsi vilivyosaini mkataba wa kuhudumia wanachama hawa?

Imefika hatua sasa wananchi tujifunze namna ya kudai haki zetu kwa nguvu.

Hizi sarakasi haziwaumizi vituo binafsi wala NHIF wala serikali, zinawaumiza wanachama wa NHIF. Hivi mchangiaji atakayefariki kwasabau ya sakata hili, NHIF, serikali au hivi vituo binafsi vitaweza kurudisha uhai wake pale watakapokuwa wamemaliza migogoro yao? Watarudisha maisha ya wagonjwa waliowapoteza kwa makusudi? Hivi ndivyo taaluma zao zinavyoeleleza??

Kwa nchi yenye wananchi na serikali inayojitambua, mkurugenzi wa NHIF, mwenyekiti wa Bodi ya wamiliki wa vituo binafsi na waziri wa afya walitakiwa wawe lockup wanatafutia ufumbuzi huko sio kulala usingizi mnono wakati wagonjwa wa NHIF wanasubiri kufukuzwa kutoka vituo binafsi baada ya saa48

Wamekopeshana hela nyingi snaa kinyume na Sera za Mikopo. Wamepeana interest ndogo sana

Yule DG Wa NHIF ni wa kwenda GEREZANI
hapaswi kuwepo ofisin
 
Nasikia Benjamin mkapa hiyo hospital ilijengwa na NHIF lakini mpaka sasa hiyo hela haijawahi kurudishwq
Kama ambavyo mifuko ya hifadhi ya jamii ilivyojenga chuo kikuu UDOM ikayumba na sasa wanahangaika na kikokotoo kuwaminya hao waliochangia. Hii serikali hii inatakiwa ipate kizazi jeurui cha kuuliza maswali magumu
 
Back
Top Bottom