Wanasheria tusaidieni kufungua kesi mahakamani ili mikataba yote ya rasilimali zetu ambayo Rais Samia kasaini na wageni ipelekwe bungeni

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,504
51,099
Wanasheria wetu wanaonisoma, naombembeni mlisaidie Taifa kufungua kesi mahakamani ili mikataba yote inayohusu rasilimali zetu ambazo utawala wa Rais Samia umesaini ipelekwe bungeni.

Tunajua kuwa ipo sheria inayohusu rasilimali na Soveregnty ya nchi, inayotaka mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi yetu ipitishwe bungeni.

Sasa tunasikia rais kasaini mkataba wa Ushirikiano na waarabu wa UAE kuhusu misitu yetu. Mkataba haujapitishwa bungeni na sisi wananchi hatujui humo ndani kuna nini!.

Ipo haja mahakama iiagize serikali itii sheria.

Pengine ndiyo maana Samia badala ya kupeleka mikataba hiyo bungeni yeye anakimbilia kubadili sheria ili kuhalalisha uvunjaji wake wa sheria.

Hii maana yake ni kwamba anajua fika wakati anasaini mikataba hiyo, alikuwa anavunja sheria lakini akaamua tu kusaini kwa kuwa anajua atazibsdili sheria zinazombana kumfavor yeye.

Na si mkataba wa misitu tu, tunasilia kuwa kasaini mikataba mingine 37 ambayo hatujui ndani kuna nini.

Ipo haja mahakama imlazimishe mikataba inayopaswa kufikishwa bungeni ifike bungeni!.
 
Our President:

1) Represents the best interests of all of the people.

2) Represents our nation in talking with foreign nations for the best of our beloved Tanzania.

#Miluzi Mingi Humpoteza Mchungaji

#SiempreJMT

#Mama Anaupiga Mwingi
 
Ikienda bungeni inatoa fursa kwa wenye rasilimali zao kujua nini kinaendelea kuhusu rasilimali zao, pamoja na kwamba bunge lenyewe halijitambui
Na kesi zikifunguliwa mahakamani, hiyo pia ni fursa ya wananchi kujua kilichomo kwenye hiyo mikataba, hata kama Bunge na Mahakama hazitazuia hiyo mikataba.

Ni fursa kwa Mahakama ya wananchi kupima na kutoa hukumu isiyozuiwa na Bunge wala Mahakama za maghumashi.
 
Tunajua kuwa ipo sheria inayohusu rasilimali na Soveregnty ya nchi, inayotaka mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi yetu ipitishwe bungeni.
Sheria haijasema mikataba yote inayohusu rasilimali za taifa lazima ipitishwe Bungeni, sheria imetoa option kwa kusema neno "may", kumaanisha inaweza kupitishwa Bungeni au kutopitishwa!, sio lazima!
Kasome ibara ya 12 ya The natural wealth and resources act". attached
Sasa tunasikia rais kasaini mkataba wa Ushirikiano na waarabu wa UAE kuhusu misitu yetu. Mkataba haujapitishwa bungeni na sisi wananchi hatujui humo ndani kuna nini!.
Kwanza rais hasaini mikataba, kile kinachofanyika rais akiwa ziara mbalimbali ni kwa rais kushuhudia mikataba ya ushirikiano ikisainiwa na sio rais anasaini!.

Hiyo inayoitwa mikataba ya ushirikiano sio mikataba kwa maana halisi ya mikataba yaani contracts, hizo ni MoU, kwa kizungu ni memorandum of understanding, ni makubaliano tuu yaani agreements na sio contracts, hata ile IGA ni makubaliano tuu na sio mkataba, mkataba ni HGA.

MoU sio lazima zipelekwe Bungeni!

Kasome pia
P
 
Attachments

  • tan185073.pdf
    182.4 KB · Views: 3
Sheria haijasema mikataba yote inayohusu rasilimali za taifa lazima ipitishwe Bungeni, sheria imetoa option kwa kusema neno "may", kumaanisha inaweza kupitushwa Bungeni au kutopitishwa!, sio lazima!

Kwanza rais hasaini mikataba, kile kinachofanyika rais akiwa ziara mbalimbali ni kwa rais kushuhudia mikataba ya ushirikiano ikisainiwa na sio rais anasaini!.

Hiyo inayoitwa mikataba ya ushirikiano sio mikataba kwa maana halisi ya mikataba yaani contracts, hizo ni MoU, kwa kizungu ni memorandum of understanding, ni makubaliano tuu yaani agreements na sio contracts, hata ile IGA ni makubaliano tuu na sio mkataba, mkataba ni HGA.

MoU sio lazima zipelekwe Bungeni!

Kasome pia
P
Tukisema "rais kasaini" ni figurative language kuwa "serikali yake imesaini", si lazima awe kasaini yeye kwa mkono wake. Ni sawa na tunavyosema kuwa "Nyerere kampiga Amini", haimaanishi alibeba bunduki na kwenda msitari wa mbele, bali alikuwa amiri jeshi mkuu ambaye chini ya uongozi wake utawala wa Amin uliangushwa.

Tukisema Samia kaongeza ajira hatumaanishi ni yeye anayeajiri kila mtu nchini.

Tuelewe lugha yetu ya kiswahili vizuri, tashbiha zake n.k
 
Asante, nimeelewa figurative of speech
Thanks
P
 
Wanasheria wetu wanaonisoma, naombembeni mlisaidie Taifa kufungua kesi mahakamani ili mikataba yote inayohusu rasilimali zetu ambazo utawala wa Rais Samia umesaini ipelekwe bungeni.

Tunajua kuwa ipo sheria inayohusu rasilimali na Soveregnty ya nchi, inayotaka mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi yetu ipitishwe bungeni.

Sasa tunasikia rais kasaini mkataba wa Ushirikiano na waarabu wa UAE kuhusu misitu yetu. Mkataba haujapitishwa bungeni na sisi wananchi hatujui humo ndani kuna nini!.

Ipo haja mahakama iiagize serikali itii sheria.

Pengine ndiyo maana Samia badala ya kupeleka mikataba hiyo bungeni yeye anakimbilia kubadili sheria ili kuhalalisha uvunjaji wake wa sheria.

Hii maana yake ni kwamba anajua fika wakati anasaini mikataba hiyo, alikuwa anavunja sheria lakini akaamua tu kusaini kwa kuwa anajua atazibsdili sheria zinazombana kumfavor yeye.

Na si mkataba wa misitu tu, tunasilia kuwa kasaini mikataba mingine 37 ambayo hatujui ndani kuna nini.

Ipo haja mahakama imlazimishe mikataba inayopaswa kufikishwa bungeni ifike bungeni!.
Wabunge wa kupelekewa hiyo mikataba ndo akina Ndiyoooooo? Kifupi hakuna hoja itapita ndani ya bunge iliyoasisiwa na ccm isiungwe mkono. Wataunga mkono hoja.

Wale wanawaza hela tu
 
Hatari sana. Baada ya huyu Mama Abdul kuondoka madarakani nchi itakua utumwani completely, kuna haja ya kuanza kuifuatilia kwa ukaribu mikataba yote ambayo ameisainia huko MAFICHONI
 
Our President:

1)Represents the best interests of all of the people ,

2)Represents our nation in talking with foreign nations.....for the best of our beloved Tanzania....

#Miluzi Mingi Humpoteza Mchungaji

#SiempreJMT

#Mama Anaupiga Mwingi
Mchungaji bubu ndie anayewapoteza kondoo wake, na wala mchungaji bubu hajaweka mbele maslahi ya watanganyika, usiandike uongo hapa, huyo ana represent interest za waarabu, hao ndio anaowasikiliza na kutenda vile wanavyotaka, huu ndio ukweli.
 
Wanasheria wetu wanaonisoma, naombembeni mlisaidie Taifa kufungua kesi mahakamani ili mikataba yote inayohusu rasilimali zetu ambazo utawala wa Rais Samia umesaini ipelekwe bungeni.

Tunajua kuwa ipo sheria inayohusu rasilimali na Soveregnty ya nchi, inayotaka mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi yetu ipitishwe bungeni.

Sasa tunasikia rais kasaini mkataba wa Ushirikiano na waarabu wa UAE kuhusu misitu yetu. Mkataba haujapitishwa bungeni na sisi wananchi hatujui humo ndani kuna nini!.

Ipo haja mahakama iiagize serikali itii sheria.

Pengine ndiyo maana Samia badala ya kupeleka mikataba hiyo bungeni yeye anakimbilia kubadili sheria ili kuhalalisha uvunjaji wake wa sheria.

Hii maana yake ni kwamba anajua fika wakati anasaini mikataba hiyo, alikuwa anavunja sheria lakini akaamua tu kusaini kwa kuwa anajua atazibsdili sheria zinazombana kumfavor yeye.

Na si mkataba wa misitu tu, tunasilia kuwa kasaini mikataba mingine 37 ambayo hatujui ndani kuna nini.

Ipo haja mahakama imlazimishe mikataba inayopaswa kufikishwa bungeni ifike bungeni!.
Bahati mbaya hatuna bunge bali kikundi cha wahuni ambao sio wawakilishi wa wananchi bali machawa wa Samia
 
Wanasheria wetu wanaonisoma, naombembeni mlisaidie Taifa kufungua kesi mahakamani ili mikataba yote inayohusu rasilimali zetu ambazo utawala wa Rais Samia umesaini ipelekwe bungeni.

Tunajua kuwa ipo sheria inayohusu rasilimali na Soveregnty ya nchi, inayotaka mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi yetu ipitishwe bungeni.

Sasa tunasikia rais kasaini mkataba wa Ushirikiano na waarabu wa UAE kuhusu misitu yetu. Mkataba haujapitishwa bungeni na sisi wananchi hatujui humo ndani kuna nini!.

Ipo haja mahakama iiagize serikali itii sheria.

Pengine ndiyo maana Samia badala ya kupeleka mikataba hiyo bungeni yeye anakimbilia kubadili sheria ili kuhalalisha uvunjaji wake wa sheria.

Hii maana yake ni kwamba anajua fika wakati anasaini mikataba hiyo, alikuwa anavunja sheria lakini akaamua tu kusaini kwa kuwa anajua atazibsdili sheria zinazombana kumfavor yeye.

Na si mkataba wa misitu tu, tunasilia kuwa kasaini mikataba mingine 37 ambayo hatujui ndani kuna nini.

Ipo haja mahakama imlazimishe mikataba inayopaswa kufikishwa bungeni ifike bungeni!.
Hawawezi kufungua kesi mpaka waione mikataba husika ilo kuweza ku establish kesi yenye mantiki
 
Kila mtu analinda kitumbua chake hapa Tanzania kuanzia kahaba,rais,makamu,waziri mbunge matajiri wafanya biashara diwani hadi barozi wa nyumba kumi.
Ukiwa na wadhifa kitu chakwanza ni namna ya kuendelea nao huo wadhifa wako.
Serikali ikitaka jambo lake hakuna wa kupinga. Hzo taka taka sijui bunge au mahakama haziwezi kuzisimamia serikali bali serikali husimamia kila kitu kuanzia bunge,mahakama na hilo baraza kwa maslahi mapema ya walio juu.
Kazi ya bunge ni kusikiliza,kutii,kuipamba na kupitisha matakwa yote ya serikali. Angalia spika anapatkanaje. Mfano shuleni mkuu wa shule amchague HP alafu wanafunzi wapige kura ya ndio au hapana. Hapo huyo HP atakuwa amechaguliwa au ameteuliwa? Kwa nini mchako wa spika usifanyike kwa wazi ndani ya bunge alafu serikali itaarifiwe tu?
Spika amepelekwa bungeni na serikali na ndie kiranja wa bunge. Wabunge bhana eti mkono kuubwabwa(wananchi) macho kumchuzi(serikali). Hakuna mbunge asiyependa nyama hasa hawa wa ccm C&D ili warudi tena buchani.
 
Wanasheria wetu wanaonisoma, naombembeni mlisaidie Taifa kufungua kesi mahakamani ili mikataba yote inayohusu rasilimali zetu ambazo utawala wa Rais Samia umesaini ipelekwe bungeni.

Tunajua kuwa ipo sheria inayohusu rasilimali na Soveregnty ya nchi, inayotaka mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi yetu ipitishwe bungeni.

Sasa tunasikia rais kasaini mkataba wa Ushirikiano na waarabu wa UAE kuhusu misitu yetu. Mkataba haujapitishwa bungeni na sisi wananchi hatujui humo ndani kuna nini!.

Ipo haja mahakama iiagize serikali itii sheria.

Pengine ndiyo maana Samia badala ya kupeleka mikataba hiyo bungeni yeye anakimbilia kubadili sheria ili kuhalalisha uvunjaji wake wa sheria.

Hii maana yake ni kwamba anajua fika wakati anasaini mikataba hiyo, alikuwa anavunja sheria lakini akaamua tu kusaini kwa kuwa anajua atazibsdili sheria zinazombana kumfavor yeye.

Na si mkataba wa misitu tu, tunasilia kuwa kasaini mikataba mingine 37 ambayo hatujui ndani kuna nini.

Ipo haja mahakama imlazimishe mikataba inayopaswa kufikishwa bungeni ifike bungeni!.
Bunge lipi?
 
Sheria haijasema mikataba yote inayohusu rasilimali za taifa lazima ipitishwe Bungeni, sheria imetoa option kwa kusema neno "may", kumaanisha inaweza kupitishwa Bungeni au kutopitishwa!, sio lazima!
Kasome ibara ya 12 ya The natural wealth and resources act". attached

Kwanza rais hasaini mikataba, kile kinachofanyika rais akiwa ziara mbalimbali ni kwa rais kushuhudia mikataba ya ushirikiano ikisainiwa na sio rais anasaini!.

Hiyo inayoitwa mikataba ya ushirikiano sio mikataba kwa maana halisi ya mikataba yaani contracts, hizo ni MoU, kwa kizungu ni memorandum of understanding, ni makubaliano tuu yaani agreements na sio contracts, hata ile IGA ni makubaliano tuu na sio mkataba, mkataba ni HGA.

MoU sio lazima zipelekwe Bungeni!

Kasome pia
P
Vipi umeamka vibaya nini? Unasema MoU hazipelekwe Bungeni kwa sababu ni makubaliano na siyo mikataba. Unasema kuwa IGA siyo mkataba ni makubaliano. Kwa hiyo IGA ilipelekwaji Bungeni wakati ni makubaliano, na makubaliano huwa hayapelekwi bungeni?

Kuulinda uwongo ni kazi ngumu sana, ndiyo maana Serikali imeshindwa, na wewe pia umeshindwa kabisa.

Wote tunaoipenda nchi yetu TUSEME NO KWA MKATABA WA KISHENZI WA DP NA VIONGOZI DHULUMATI WANAOUZA RASILIMALI ZA NCHI YETU KWA MANUFAA YAO BINAFSI.
 
Mchungaji bubu ndie anayewapoteza kondoo wake, na wala mchungaji bubu hajaweka mbele maslahi ya watanganyika, usiandike uongo hapa, huyo ana represent interest za waarabu, hao ndio anaowasikiliza na kutenda vile wanavyotaka, huu ndio ukweli.
Fikiria mtu anapewa Urais, kituo chake cha kwanza anaenda kwa mjomba wake aliyepo Oman, mjombake anampeleka kwa kiongozi wa Oman. Ni sawa na mtu anayeebda kusema kuwa, mjomba, wamenipa nchi kule, naye mjomba anamwambia kuwa twende tukamjulishe kiongozi wetu.

Kitafsiri na kimantiki, Oman, wanaona wamepewa koloni kupitia uongozi wa mtoto wao.
 
Back
Top Bottom