Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,610
Wanabodi
Nipashe la leo,
Screen Shot 2023-06-25 at 6.00.46 AM.png
Screen Shot 2023-06-25 at 6.01.11 AM.png

Kama kawaida yangu kila Jumapili, huwaletea makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, kuzungumzia jambo lolote la kisiasa, kiuchumi na kijamii lenye maslahi kwa taifa. Mada hizi huwa zina, swali , na hoja, kisha jibu, utalitoa wewe msomaji mwenywe. Swali la leo ni kutuhusu sisi Watanzania "Watanzania ni Watu wa Ajabu?, Wanapigiaje Kelele Jambo Dogo la Mkataba wa Bandari, wakati Mambo Makubwa Muhimu na ya Msingi sana kama Katiba yao imenajisiwa, na Uhuru Wao wa kuchagua na kuchaguliwa umeporwa lakini Wako Kimya?!.

Leo naendelea na mada ya wiki iliyopita kuhusu makubaliano ya kiserikali, IGA ambapo Bunge letu limeridhia Serikali yetu kuingia mkataba wa HGA na kampuni ya DPW ya Dubai, kutuendeshea Bandari yet ya Dar es Salaam ombalo ni jambo zuri na jambo jema kwa maslahi ya taifa, lakini bado kuna kelele nyingi huku na kule, kupinga jambo hii. Baadhi ya hoja za kupinga ni hoja za msingi na zina mashiko, ambazo inabidi serikali yetu sikivu izizingatie, lakini hoja nyingine ni kelele za kijinga tuu kwa watu wajinga kwa kutokujua.

  1. Tatizo kubwa la Watanzania ni ujinga, ukosefu wa elimu!. Kwenye hili la bandari, Watanzania wanahitaji kuelimishwa tuu.Juzi kati, nimetembelea Idara ya Habari Maelezo, nimekutana na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe, kwanza nikampongeza kwa uteuzi, na kumshushia yeye zigo lote la lawama kwa hizi sintofahamu zote, zinazoendelea kuhusu hili la bandari, kwa kumweleza, limefikia hapa kwa kukosekana uwazi na elimu kwa umma kuhusu jambo hili. Nikampongeza kwa open up hadi Club House, lakini hizo Club House ziwe za proactive na sio kusubiri kelele ndipo wanakuwa reactive!. Tangu kelele za mkataba kuanza, kwanini mpaka sasa hakuna kipindi chochote cha elimu kwa umma kuhusu hili?. Msigwa alimalizia kwa taarifa ya kutia moyo sana, Maelezo inakwenda ku open up hadi kuwa na studio yake.
  2. Watanzania ni watu wa ajabu sana!, Wanapigiaje kelele kamkataba kamoja tuu kadogo kwa rasilimali bandari, lakini kuna mambo makubwa muhimu sana ya msingi kama ubatili wa katiba, na kuporwa kwa uhuru wao, ambayo ni mambo muhimu sana!. Kwanini Watanzania wako kimya kwenye mambo makubwa ya msingi ya katiba yao kunajisiwa na uhuru wao kuporwa, halafu wanapigia kelele suala la rasilimali bandari?. Hii tasfsiri yangu, Watanzania ni watu wa kelele kwenye petty issues, lakini very serious issues, wako kimya!.
  3. Ili nisionekane na mimi ni mpinzani, namshauri Rais Samia, usiwasikilize kabisa wanaopinga ukodishwaji wa bandari kwa kampuni ya DPW ya Dubai, kwa hoja muflis, wapuuzwe!, ila wanaopinga kwa hoja za msingi, zenye masikio, wasikilizwe ili kazi nzuri ya Rais Samia iendelee!, ili HGA iwe safi na imenyooka!,
  4. Kati ya Katiba, Uhuru na Rasilimali, kipi ni muhimu zaidi?. Kitu muhimu cha kwanza kwenye nchi yoyote ni watu, uhuru wao, na katiba yao, mengine yote ikiwemo rasilimali yanafuata.
  5. Tuna katiba mbovu yenye ubatili, katiba mbovu hiyo, imeruhusu Bunge letu kutunga sheria batili na sheria mbovu, zinazoruhusu mikataba mibovu ya rasilimali zetu, huo mkataba mbovu wa IGA ni matokeo, tuu, badala ya kudeal na chanzo, mnahangaika na matokeo!.
  6. Watanzania nimewaelezea kuwa ni watu wa ajabu sana kwasababu katiba yao imenajisiwa kwa kutiwa ubatili!, huku Watanzania wamenyamaza kimya!. Kwa nini haki zao mbili kuu za msingi za kuchagua na kuchaguliwa, zimeporwa na kufinyangwa finyangwa huku Watanzania wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  7. Serikali yao imetunga sheria batili kinyume cha katiba, ikazipeleka Bungeni kutungwa kuwa sheria!, Bunge, lililoshehenezwa wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, baada ya kupokea mswada huo, Bunge letu tukufu, likazipitisha sheria hizo batili kwa kuzitunga kuwa sheria!, huku Watanzania wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  8. Rais wa JMT hajawahi kuwa mwanasheria, anawategemea wasaidizi wake wabobezi na wabobevu wa sheria, kama wamezipitisha, sheria hizo batili, rais akazisaini kuwa sheria kamili licha ya ubatili wake!, huku Watanzania wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  9. Mchungaji Mtikila (RIP), akafungua shauri Mahakama Kuu kupinga sheria batili hiyo, bila support ya Watanzania wowote huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, Mahakama Kuu, ikatamka sheria hizo ni batili zifutwe toka vitabu vya sheria!. Serikali yetu ikakata rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, ikashindwa!.
  10. Baada ya Serikali kushindwa, ikapeleka Bungeni mabadiliko haramu ya katiba ya JMT kwa kuvichomekea vipengele hivyo batili, Bunge letu Tukufu, livichomekee kiubatili ndani ya katiba yetu!. Bunge letu Tukufu likafanya mabadiliko batili ya katiba yetu ya JMT na kuuchomekea ubatili huo ndani ya katiba yetu!, huku Watanzania wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  11. Mchungaji Mtikila hakukubali katiba yetu inajisiwe, kwa kuchomekewa ubatili!, hivyo akafungua shauri jingine kupinga mabadiliko hayo ya katiba kuingiza ubatili ndani ya katiba yetu!, huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  12. Mahakama Kuu, ikampa ushindi Mchungaji Mtikila, ikatamka mabadiliko hayo ya katiba ni batili, na yamechomekewa ndani ya katiba yetu kiubatili!, huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  13. Serikali yetu makini yenye wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, ikakata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu iliyotimiza wajibu wake kikamilifu kupinga katiba yetu kunajisiwa kwa kuchomekewa batili kiubatili!, huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  14. Mahakama ya Rufani, ikatoa uamuzi wa ajabu kabisa kwa kusema "The Court is not the custodians of the will of the people", na kulitaka Bunge lile lile lililochomekea batili ndani ya katiba yetu kiubatili ndilo liondoe batili hiyo!, huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  15. Mpaka leo ninapoandika hapa, batili hiyo iliyochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu bado ipo!. Ina maana tuna katiba yenye ubatili ndani yake!, huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia?!, hawa sio watu wa ajabu?!
  16. Mpaka leo ninapoandika hapa, bado tuna sheria batili ndani ya sheria zetu, zinazopora uhuru wa Watanzania kuchagua na kuchaguliwa, huku Watanzania wengine wote wamenyamaza kimya tuu, wanaangalia!, hawa sio watu wa ajabu?!Iweje leo, Bunge hili hili lililopitisha ubatili ule wa ajabu kabisa, kwanza kwa kutunga sheria batili, na hata baada ya mahahama kutamka vipengele hivyo ni batili, bado Bunge lilivichomekea kiubatili, vipengele hivyo batili ndani ya katiba yetu likanyamaziwa!, lakini lilipopitisha kijimkataba kidogo tuu cha rasilimali Bandari kwa kampuni ya DPW ya Dubai, watu wanapiga kelele mpaka karibu zifike mbinguni?, hawa Watanzania wanaopigia kelele, haka kamkataba, hawa sio watu wa ajabu?!

Hitimisho
Unanyamaziaje katiba yako inanajisiwa, uhuru wako unaporwa, halafu unapigia kelele jambo la kheri kama uendeshaji wa Bandari?!, huu sio uthibitisho kuwa sisi Watanzani ni watu wa ajabu sana?, kwanini wanashadadia sana kulipinga jambo la kheri, kusaidiwa kuendesha bandari yetu kwa ufanisi baada ya sisi kushindwa, halafu jambo kubwa na la msingi sana kama katiba yako imenajisiwa, uhuru wako muhimu kabisa wa kuchagua na kuchaguliwwa umeporwa!, kwanini tunanyamaza?!, sisi sio watu wa ajabu sana?

Wasalaam

Pasikali
Rejea za mwandishi kuhusu sakata la Bandari
  1. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
  2. Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!
  3. Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
  4. Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?
  5. Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?
  6. DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?
  7. Je, ni Kweli Bunge letu ni Dhaifu na Kibogoyo?
Mabandiko ya Mwandishi Kupigia Kelele Mambo Makubwa Muhimu ya Msingi, ya Uhuru, Katiba, Sheria na Haki
  1. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
  2. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  3. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
  4. Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
  5. Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?
  6. Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?
 
Mkataba ungekuwa unasema hivyo kama anavyosema waziri mkuu Kassim Majaliwa tusingelalamika.

Sasa hivi ufafanuzi unatolewa mwingine na mkataba unasema mengine, sisi watanzania hatutasikiliza chochote ambacho hakipo kwenye mkataba ,yatakuwa ni matumizi mabaya ya masikio yetu.
Hata chifu Mangungo wa Msovera alipewa maelezo mazuri sana

Kuna gunduzi nyingi sasa hivi kama magari ya kutumia umeme, gesi na mwarabu anategemea mafuta kwa hiyo walishaona mbali sana ndiyo maana ya mikataba ya milele.

Next generation biashara ya mafuta inaweza kuja kuwa ya kawaida sana lzm waandae pa kukimbilia
 
Baadhi ya Watanzania ni kuangalia Mita 10 tu mbele hawana habari kuangalia mita 1000
sababu bandari ni sehem ya mapato halali na haram wapenda haramu au Dili huona mwisho mita 10, bado tunasafari ndefu hii nchi kufikia hayo ya Muda mrefu
 
Mimi Sijasoma andiko, mmeishia kwenye Kichwa Cha Habari.


Itoshe tu kusema , Mh Pascal , Kwa Sasa wee ni Pro Chawa unayetumia Kalamu yako kuwatia watanzania kwenye Reli .


Bandari ni suala Dogo?. Suala Dogo ambalo ndio Linaloilisha Bajeti ya Nchi.

Hapana, hata Kama Mama amekurejeshea kile ulichokipoteza Kwa miaka Ile ya Hayati, uchawa umezidi, sio Bora ukae kimya?.



Ati unagusia Uhuru wa watu, Kwa sababumliwaaminisha watanzania kua JPM anabana uhuru wa watu ,Sasa Mama kaurejesha uhuru wa watu??? Kwamba watu wako huru kuongea ? ... WATANZANIA SIO WAJINGA, UHURU ULIKUWEPO.


Kuhusu Katiba Mpya, hili la Bandari pia Wataalam wa sheria , waweka wazi kua Lina chembechembe za Katiba, kwakua tumelipazia sauti , tutaendelea kulipazia sauti .



WATANZANIA TUENDELEE KUPAZA SAUTI ,TAASISI MBALIMBALI, VIONGOZI W DINI, ENDELEENI KUPAZA SAUTI, BANDARI IMEUZWA, TANZANIA IMEUZWA !!.
 
Mimi Sijasoma andiko, mmeishia kwenye Kichwa Cha Habari.


Itoshe tu kusema , Mh Pascal , Kwa Sasa wee ni Pro Chawa unayetumia Kalamu yako kuwatia watanzania kwenye Reli .


Bandari ni suala Dogo?. Suala Dogo ambalo ndio Linaloilisha Bajeti ya Nchi.

Hapana, hata Kama Mama amekurejeshea kile ulichokipoteza Kwa miaka Ile ya Hayati, uchawa umezidi, sio Bora ukae kimya?.



Ati unagusia Uhuru wa watu, Kwa sababumliwaaminisha watanzania kua JPM anabana uhuru wa watu ,Sasa Mama kaurejesha uhuru wa watu??? Kwamba watu wako huru kuongea ? ... WATANZANIA SIO WAJINGA, UHURU ULIKUWEPO.


Kuhusu Katiba Mpya, hili la Bandari pia Wataalam wa sheria , waweka wazi kua Lina chembechembe za Katiba, kwakua tumelipazia sauti , tutaendelea kulipazia sauti .



WATANZANIA TUENDELEE KUPAZA SAUTI ,TAASISI MBALIMBALI, VIONGOZI W DINI, ENDELEENI KUPAZA SAUTI, BANDARI IMEUZWA, TANZANIA IMEUZWA !!.
 
Kibaya zaidi ni uongo...
Mtu msomi anansema mkataba hauna kikomo..

Wakati kuna "termination clause"inasema kabisa uhai wa IGA utategemea na uhai wa HGA......
Iwapo mkataba wa HGA itakuwa miaka 25 basi IGA ni miaka 25...
Kipengele kipo wazi kabisa
 
Back
Top Bottom