Wanafunzi wa taasisi ya Confucius katika chuo kikuu cha Dar es Salaam Tanzania wajifunza utamaduni wa sikukuu ya Duanwu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
Tarehe 21 Juni, wanafunzi wa shule za upili wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tanzania (UDSM) walitembelea chuo kikuu cha wazi cha Jinhua, mkoani Zhejiang, China, ambapo walijifunza utamaduni wa sikukuu ya jadi ya China –Duanwu.

Sikukuu ya Duanwu ni moja ya sikukuu nne muhimu za jadi za wachina pamoja na sikukuu ya Spring, sikukuu ya Qingming na sikukuu ya mwezi. Mwalimu Songjie wa chuo kikuu cha wazi cha Jinhua alifahamisha historia ya sikukuu ya Duanwu na desturi zake.

1687935988890.png



1687936001531.png



(Mwalimu Song Jie anaelezea desturi za Sikukuu ya Duanwu. Picha: Zhou Yue)


Keki ya maharage ya kijani ni chakula cha jadi cha majira ya joto hapa China. Katika zama za kale, wachina walikunya pombe ya Xionghuang, kula Zongzi, keki ya maharage ya kijani na vyakula vingine ili kuombea afya njema na usalama. Wanafunzi hao waliwafuata wapishi wa keki kutengeneza keki ya maharage ya kijani.

1687936030456.png


1687936040224.png


(wanafunzi wanatengeneza keki ya maharage ya kijani. Picha: Zhou Yue)​

Vilevile, walimu wa sanaa ya kaligrafia wanaandika salamu za sikukuu ya Duanwu kwa kila mwanafunzi. Wanafunzi hao pia wamejaribu kuandika kwa kutumia brashi ya kuandikia ya kichina.

1687936060968.png



1687936070032.png


(Wanafunzi wanajifunza sanaa ya kaligrafia ya kichina. Picha:Zhou Yue)
 
Back
Top Bottom