Baraza la Madiwani ladai Kifo cha Hayati Magufuli kimekwamisha ujenzi wa Chuo Kikuu Chato

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
Screenshot_2024-03-20-21-18-42-354_com.brave.browser-edit.jpg

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita, limembebesha mzigo mzito Mkuu mpya wa Wilaya hiyo wakimtaka kufuatilia sababu za kukwama kwa ujenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Chato, tangu kutokea kifo cha Hayati Rais Dk. John Magufuli.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Christian Manunga, wakati akifungua kikao cha baraza hilo, huku mkuu mpya wa wilaya hiyo, Said Nkumba, akiwa amealikwa kuhudhuria kikao hicho ikiwa ni pamoja na kujitambulisha kwa madiwani wa halmashauri hiyo.

"Wilaya yetu inayo miradi mingi ya maendeleo ambayo inapaswa kusimamiwa ili ikamilike kwa ubora, pamoja na miradi hiyo tunatambua wewe ni mfuatiliaji mzuri wa maendeleo sasa tunakuomba pia ufuatilie sababu za kukwama kwa ujenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Dar es salaam tawi la Chato kwa maana tayari msingi ulichimbwa na baadhi ya shughuli kuanza, lakini sasa vifaa vingi vinazidi kuharibika pasipo kujua hatma ya hili" amesema Manunga.
 
Hili si suala la mkuu wa wilaya kufuatilia.

Sababu za ujenzi kukwama zipo wazi na zinajulikana.

Miradi mingi ya chato ilijengwa kwa matakwa ya Magu na sio vinginevyo.

Aliyetaka ameshakufa na miradi ambayo ilikuwa haijaanza na ile ambayo ilikuwa kwenye hatua za awali yote chali.
 
Back
Top Bottom