SoC03 Wanafunzi wa kike mwaka wa kwanza kwenye mahusiano ya kimapenzi

Stories of Change - 2023 Competition

Tizzo G

Member
Jun 9, 2012
24
14
Kama jamii ya watanzania na Kwa maadili yetu, tunategemea kuona watoto wa kike wakipata malezi Bora na ushauri nasaha kuhusu mahusiano na athari za mahusiano ya kimapenzi hasa Kwa wale wa mwaka wa kwanza katika elimu ya chuo Kwa ngazi ya shahada.

Wanafunzi wengi wa kike hujikuta wakiangukia katika mazingira ya mahusiano ya kimapenzi yasiyo ya afya yanayowapelekea kupata mimba za mapema na kua na zao la watoto wasio na malezi bora kutoka Kwa wazazi wote wawili au mmoja kua masomoni.

Nini Kifanyike?
Kama mdau katika malezi ya wanafunzi wa kike, njia ya kupunguza tatizo la watoto wa kike kuingia katika mahusiano ya kimapenzi wakati wakiwa masomoni linaweza kutatuliwa Kwa kutoa ushauri Kwa watoto wa kike wa mwaka wa kwanza Kwa Kila chuo hapa nchini kama vile inavyotolewa kozi ya kiingereza Kwa Wanafunzi wanaoanza kidato Cha kwanza hapa nchini kama njia ya kumjengea mwanafunzi uelewa katika lugha ya kiingereza ambayo ndio lugha ya mawasiliano katika usomaji, ujifunzaji na ufundishaji Kwa elimu ya sekondari hapa nchini.

Semina hii inaweza kutolewa Kwa Wanafunzi wa kike wa mwaka wa kwanza Kwa Kila chuo Kwa mda wa wiki nne mpaka tano Kwa wale waliohitimu kidato Cha sita na sio wale waliotoka makazini au hata wote ni sawa.
Pili semina hii itapunguza idadi ya watoto wasio na malezi Bora kutoka Kwa mama na baba, ikumbukwe mwanafunzi huyu anaeongelewa ni yule aliehitimu kidato Cha sita na kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza.

Kupunguza idadi ya watoto wasio na malezi Bora kutoka Kwa baba na mama kutalifanya Taifa letu kuwa na misingi Bora ya malezi na kupata watu wenye kulitumikia Taifa Kwa welezi mzuri na kupunguza watoto wa mtaani.

Idadi ya wanafunzi wa kike wanaoingia kwenye mahusiano wakati wakiwa mwaka wa kwanza ni wengi na wengi wao wanaingia bila kujua madhara watakayoyapata kwenye mahusiano hayo Kwa semina ni ya muhimu kwao.

Kumwacha mwanafunzi huyu wa mwaka wa kwanza kuanza masomo ya chuo bila elimu elekezi juu ya madhara ya mahusiano ya kimapenzi akiwa mwaka wa kwanza au akiwa masomoni ni sawa na kumwacha mwanafunzi wa kidato Cha Kwanza bila kupata kozi ya kiingereza ya awali ili kumjengea uwezo wa kuijua lugha ya mawasiliano katika masomo yake.

Njia za kutoa semina hii ni kukutana na wanafunzi Hawa ana Kwa ana katika vyuo husika na pia kuwapa madhara ya watoto waliokosa malezi Bora kutoka Kwa wazazi wao.

Semina hii inaweza kufanyika Kwa kushirikiana na taasisi za kitaaluma za saikolojia na elimu ya uzazi hapa nchini ii kutoa mwelekeo Chanya Kwa wanafunzi wa kike wa mwaka wa kwanza Kwa Kila chuo hapa nchini baada ya kupata kubadili kutoka kwenye wizara husika.

Ni muhimu sana Kwa Wanafunzi wa kike wa mwaka wa kwanza katika ngazi ya shahada, pia hata ikifanyika Kwa Wanafunzi wa mwaka wa kwanza Kwa ngazi ya stashahada na astashada wapate hii semina kwani wote wataweza kupata kujua madhara ya kupita katika mahusiano ya kimapenzi ukiwa masomoni.

Njia nyingine ambayo inaweza kufanyika ili kupunguza athari za mahusiano ya kimapenzi Kwa watoto wa kike wawapo masomoni ni kuishauri taasisi ya elimu ya juu ya vyuo vikuu TCU kuanzisha kozi ya ushauri wa athari za mahusiano ya kimapenzi na elimu ya uzazi juu ya athari za mapenzi katika masomo kama haipo katika mtaala wa elimu ya vyuo vikuu Kwa mwaka wa kwanza na pia madhara ya watoto waliokosa malezi ya wazazi Kwa Taifa na athari katika malengo ya Taifa katika kukuza uchumi na kupigana na maadui watatu yaani umaskini, ujinga na maradhi kama alivyosema Baba wa Taifa Mlw. Julius K. Nyerere.

Pia itamwepusha mwanafunzi wa kike kuingia katika majukumu ya kulea mtoto katika umri mdogo na bila maandalizi ya kua mzazi mda wa masomo.

Kutoa elimu Kwa jamii kuhusu umuhimu wa elimu ya uzazi Kwa watoto wa kike na madhara ya mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo, ikumbukwe majukumu ya malezi ya watoto Kwa mzazi Alie na umri mdogo yaweza kua chanzo Cha msongo wa mawaso Kwa mhusika na pia chanzo Cha kupata wataalamu wasiokua na ujuzi kamili katika fani waliyokua wanasomea wahusika wakati wa masomo Yao chuoni.

Chukulia mfano itokee Kwa mwanafunzi anaesomea udaktari athari zake ni kubwa sana Kwa jamii yetu na Taifa Kwa ujumla.

Mwisho semina hii ikitolewa vizuri itaepusha kupata watoto waliokosa malezi ya mzazi mmoja au wazazi wote, kwani wengi wa wale wanaopata ujauzito wakiwa masomoni mara nyingi wanakuja kuolewa na wanaume tofauti na wale waliozaa nae wakati wakiwa masomoni.
 
Back
Top Bottom