Idadi ya Wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2024 yaongezeka kwa 1.57% ikilinganishwa na Mwaka 2023

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Baraza la Mitihani la Tanzania zimekamilisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2024.

Uchaguzi ulihusisha wanafunzi 1,092,984 wakiwemo Wasichana 507,933 na Wavulana 585, 051 ambao walifaulu Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2023.

Idadi ya Wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2024 imeongezeka kwa Wanafunzi 16,947 sawa na ongezeko la asilimia 1.57 ikilinganishwa na Wanafunzi 1,076,037 waliopata alama za kuwawezesha kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka, 2023.

Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali itahakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za Serikali hakuna atakayekosa nafasi kwani Serikali imetenga shilingi bilioni 140.5 kwaajili ya ujenzi wa madarasa mapya sambamba na ukarabati wa madarasa yaliyopo kuelekea muhula mpya wa masomo utakaoanza Januari 08, 2024.

Kupata uchaguzi kidato cha kwanza 2024, fungua Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2024
 
Back
Top Bottom