Wanafunzi wa Chuo cha Ushirka Moshi (MoCU) level ya Diploma kushindwa kufanya udahili kutokana na kucheleweshwa kwa matokeo ya supplementary

MTOTO MWEMA

New Member
Oct 17, 2023
1
1
Uongozi wa Chuo kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) umechelewesha kutoa matokea ya supplementary kwa wanafunzi wa level ya Diploma na pia kutuma matokeo hayo NACTE kwa ajili ya utambuzi, Hivyo kusababisha zaidi ya wanafunzi 200 kushindwa kufanya maombi ya elimu (Degree) kwa mwaka wa masomo 2023.

Pamoja na juhudi kubwa za Serikali kupitia taasisi zake za kudahili wanafunzi ambazo ni TCU na NACTE kuongeza muda wa kutuma maombi kwa kufungua dirisha la 4 ili wanafunzi waliokosa nafasi awali waweze kutuma maombi yao. Ila imekuwa vigumu kwa wanafunzi waliomaliza Chuo cha Ushirika Moshi kutokana na kukosa matokeo yao kwa wakati.

Hali hii inafifisha juhudi za Serikali katika kuhakikisha vijana wa kitanzania wanapata elimu. Wanafunzi wa Chuo cha Ushirika Moshi tunaomba Waziri mwenye dhamana pamoja na taasisi zake husika kuingilia suala hili na kuweza kulitatua na kutoa angalizo kwa Uongozi wa chuo hiko kushughuliia masuala yote ya muhimu kwa wakati.
 
Back
Top Bottom