Madai ya UDOM kuchelewesha vitambulisho vya Wanafunzi, chuo chasema chanzo ni uzembe wa Wanafunzi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Chuo cha UDOM kina utaratibu mbovu (1).jpg
Siku chache baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kulalamika kuwa kuna hali ya sintofahamu kubwa kwa Wanafunzi wa Chuuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) akidai kuna ucheleweshwaji wa vitambulisho na hivyo wanashindwa kufanya mitihani, uongozi wa chuo umetoa ufafanuzi.

Awali, memba huyo alidai Sheria ya Chuo inazuia kufanya mtihani bila kuwa na kitambulisho ‘active’, matokeo yake wapo waliolazimika kusogeza mbele mitihani yao ili wafanye Mitihani Maalum Septemba 2024 kwa madai hawajafanikiwa kupata Vitambulisho Vipya licha ya kukamilisha mchakato wa kujisajili mapema.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Rose Joseph anaelezea upande wa pili kilichotokea na kinachoendelea, anasema:

“Tangu chuo kilipofunguliwa katika mhula huu mnamo Oktoba 28, 2023, kwa mujibu wa Kanuni na Taratibu za Usajili wa Wanafunzi ni kuwa pindi wanapoingia chuo (Mwanafunzi) wanatakiwa kukamilisha mchakato wa usajili kisha ndio wanapata namba na kitambulisho.

“Tangu wakati huo hadi sasa (jana Februari 23, 2024) tumesajili Wanafunzi 33,127, hao wapo vizuri wamefuata taratibu inavyotakiwa.

“Tunatambua kuwa kuna Wanafunzi wanachangamoto ya ada, mfano wapo wanaotegemea wafadhili na wengine wanajilipia wenyewe, hivyo huwa inatokea kunakuwa na uchelewaji wa hapa na pale.

“Hali hiyo imekuwa ikisababisha tuongeze muda wa usajili na kuwakumbusha kuwa wajisajili kwa kuwa hawataweza kuingia kwenye chumba cha mitihani bila kuwa na kitambulisho.

“Hivyo, baada ya kufika muda wa mitihani ndio watu wanakurupuka kufanya usajili, matokeo yake hatuwezo kuwahudumia wote kwa mara moja, wao wanataka kulipa na wapate vitambulisho hapohapo, kuna uzembe ambao wanaufanya lakini wanalaumu chuo wakati ni uzembe wao wenyewe.

“Inapofiki hatua hiyo system inazidiwa nguvu kwa kuwa kila Mwanafunzi anaingia kusajili dakika za mwisho, kisha wanaanza kutoa lawawa.

“Tumekuwa tukitoa matangazo mara nyingi kuwakumbusha wajisajili, tumetumia hadi Serikali ya Wanafunzi lakini wapo ambao hawakutimiza hilo kwa kuwa tunajua lawama zitafuata mwishoni.”


Kuhusu hoja ya Mdau, soma hapa - Chuo cha UDOM kuna utaratibu mbovu wa kutoa vitambulisho, wanatuumiza Wanafunzi
 
Hawa UDOM si ndio wanakamata watu wakikosoa mifumo yao??

Anyway mimi niligraduate hapo miaka 7 wayback kipind hiko usajili ilikuwa unapanga foleni, kusema kweli chuo kilikuwa na mifumo ya hovyo sana, hususani kipindi cha usajili pia mfumo ulikuwa hovyo katika ufungukaji wa UDOM SR. na mengineyo...

Kingine kulikuwa na malecture wenye sifa japo ni baadhi ya depertment hawaoni shida kusapisha darasa zima, kulikuwa hamna dawati la malalamiko kwa wanafunzi,

Mazingira ya maji yalikuwa shida mara 100,

Wizi ulikuwa changamoto kwa wanafunzi ulinzi ukikuwa hauko imara ulikuwa unaruhusu Intruder kuingia hadi mabwenini na kisha kusababisha wizi,

Vitambulisho kupata ilikuwa changamoto nyingine, na hapa nimeshangaa kuliona hapa leo nimestuka kuona bado hawajabadilika, pia nina waswasi pengine hata haya mengine bado hayajabadilika.


By the way mungu awatangulie Vijana mpambane,
Kusoma Vyuo vyetu vya serikali ni kuwindana, mwanafunzi anataka apate GPA nzuri itakayoendana na soko huku Wakuu wa Chuo wamepanga kuwapunguza.


NB. Hii Coment yangu ni ya miaka 7 wayback sihitaji kelele na nyie Wazee wa UDOM sitaki ushahidi,
 
UDOM ni chuo cha kipumbavu kwenye mifumo yao ya TEHAMA. Cha ajabu eti ndio chuo chenye miundombinu mizuri ya kuifundisha. Yaani chuo hakiwezi kutumia resources zake vizuri ila eti kinaweza toa graduates wazuri wa miundombinu hiyo na kinawafundisha chenyewe.
 
“Hivyo, baada ya kufika muda wa mitihani ndio watu wanakurupuka kufanya usajili, matokeo yake hatuwezo kuwahudumia wote kwa mara moja, wao wanataka kulipa na wapate vitambulisho hapohapo, kuna uzembe ambao wanaufanya lakini wanalaumu chuo wakati ni uzembe wao wenyewe.
Chuo chenye wataalamu wa IT lukuki kimeshindwa kuunda mfumo unaotengeza ID kutoka kwenye malipo?
 
Facebook, TikTok, X zinatumika dunia nzima kwa wakati mmoja na hizizidiwi. Shida ni nini kwa mifumo yetu. Hata ya kiserikali utakuta inazidiwa, inazidiwaje?
 
Back
Top Bottom