A
Anonymous
Guest
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Kwenda kwa:
Makamu Mkuu wa Chuo
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
YAH: MALALAMIKO YETU WANAFUNZI KUHUSU MATOKEO
Husika na kichwa cha habari
Sisi ni Wanafunzi wa Department of Mathematics, Information and Communication Technology kwa ngazi mbalimbali Certificate, Diploma na Degree tunaleta tena malalamiko kwako kuhusiana na uongozi wa hii idara ni mwendelezo wa malalamiko ya mwaka jana tarehe 22-09-2022 ambapo tulilalamika ukamtuma Prof. Matobola Joel Mihale kutusikiliza na kweli tulifanya zoom meeting tarehe 7-10-2022.
Akasikia malalamiko yetu na matokeo yake Head of ICT, Dr Rojas aliondolewa na kupewa Dr Juliana lakini mambo hayajabadilika ni yaleyale, Walimu wapo mbali na Wanafunzi (wapo busy na mambo yao binafsi) yaani hawajali hata kidogo utadhani kuna uadui kati ya wanafunzi wa Walimu (vita kati ya walimu na wanafunzi) simu hawapokei wala ujumbe huwa hawajibu kabisa.
Mwaka jana 07-10- 2022 tulipofanya kikao na Pro Mihale aliahidi kurudisha mrejesho lakini mpaka leo hajaonekana tena, inatupa mashaka sana kama Wanafunzi kuwa hiki chuo hakijali Wanafunzi hata kidogo wala Dr Juliana tukimwambia hashughuliki na chochote sana sana ni Mr Ombeni pekee ndiyo anajali wanafunzi.
Watu wanalalamika kuhusu matokeo yao, mtu anaweza kufanya somo moja zaidi hata ya mara 3 bila kuwekewa matokeo, mbona wenzetu wa faculty zingine hawalalamiki na matokeo yao wanawekewa kwa wakati?
Sisi wa ICT ndiyo ilitakiwa tuwe mfano bora wa matumizi ya TEHAMA lakini ndiyo mfano mbovu kabisa. Je, hao Walimu kazi yao nini sasa na wanalipwa mishahara kwa kazi gani?
Tuonamba TCU na wewe muitishe kikao na Wanafunzi kupitia zoom meeting msikie kero za Wanafunzi sababu hii inaleta taswira mbaya sana kwa chuo, Mwanafunzi akilalamika matokeo yake anaambiwa aende Head Quarter, hivi kweli ndiyo utaratibu?
Yaani Mwanafunzi atoke Musoma/Kigoma au Kagera akafuatilie matokeo ya somo moja na ada amelipa? Regional Centre nazo huwa hazina msaada wowote zaidi ya kutoa control number za malipo ya mitihani hata tukipeleka malalamiko yetu hakuna kinachobadilika na huwezi kuona hata faida ya hizi Regional Centre.
Tunaomba wizara ya Elimu na TCU waingilie kati tunaona wewe kama Makamu Mkuu wa chuo labda unawaonewa haya hawa Walimu lakini wanaharibu sana ‘image’ ya chuo ukimtoa Mr Ombeni wengine wote hawana sifa za kuwa Walimu wa Chuo Kikuu kama hiki tena department of ICT ambako ndiyo Dunia ilipo kwenye TEHEMA.
Ushauri wetu ni kama wa mwaka jana (2022) Walimu wote wahamishwe isipokuwa Mr Ombeni akichelewa hata kuweka matokeo lazima awe na sababu za msingi hawa wengine hata kupokea simu wanaona kero na wakipokea kauli ni mbaya (poor customer care) na wakiahidi ahadi zao ni uongo, huwa tunajiuliza kazi zao ni zipi sasa? Mbona Mr Ombeni anafanya kwa wakati?
Tunaomba msaada wa mamlaka husika zitusaidie tumechoshwa na urasimu wa hawa walimu wetu.
Tunaomba kuwasilisha
Nakala
Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Waziri wa Elimu
TCU- Tanzania
TAKUKURU Makao makuu
Abdul Nondo
Jamii Forums - Tanzania