Wana MMU tushirikiane kuboresha Jukwaa letu

Wana MMU tushirikiane kuboresha Jukwaa letu

Status
Not open for further replies.
Na sasa yamekuwa mazoea ya watu humu kuandika risala kama hizi za kutoa wito wa kuacha kubandika mambo ya kipuuzi puuzi lakini wapi.

Kila baada ya wiki chache kunatokea mtu anaandika risala. Anapongezwa, anapewa ma-likes bwerere, halafu hakuna la maana linalotokea.

Watu hao hao waliompa ma-likes ndo unawakuta wanachangia hizo hizo mada zinazodaiwa kuishushia hadhi MMU.

Ubinadamu kazi!!

Miafrika Ndivyo Tulivyo.
 
Nashukuru sana Mr Rocky kwakuliona hili labda ninachokiona ni kuomba moderator wa jukwaa hili kuwa makini na watu wanaotoa post za mzaa kwakuwa unakuta mtu anasema natafuta mwanamke wakunitoa stress unashangaa huyu mtu aliyeandika post kama hii ana maana gani ina maana huku kuna wanawake wako wakisubiri watu kama vile danguro au ni vipi saa umefika wakati wa kuzikataa post kama hizi!!Na kumbuka humu kuna watu wamekutana na wamejenga maisha kutokana na MMU ila sasa hata kama unataka kujenga maisha unatakiwa kukaa mguu pande mstari uwekati!(Mguu ndani mhuu nje)!!kwa lugha nyingine!Sasa wote wenye mizaha mizaha nikumwachia Mods waangaike naye!
KakaKiiza asante sana mkuu na muhimu hapa ni kuwa mwamzo wa mabadiliko na fikra mpya za kuifanya MMU mahali ambapo tunaweza kukutana tukapata mawili matatu ya kusaidia jamii inayotuzunguka
Maana mtaani ni majanga na humu tena kukiwa majanga ni balaa
 
Last edited by a moderator:
Mmh, bora waziondoe tu, maana tutachangia yasiyo na manitki vile vile

Upo sahihi kabisa Mr Rocky kasi ya kumis-use hili jukwaa inaongezeka kwa kasi,utoto,kejeli,kuchambana,matusi vimekuwa kawaida wakati hapo awali havikuwa na nafasi,pamoja na kureport mi naona hamna haja ya kuchangia sredi zisizokuwa na mantiki unapotezeaa tu
 
AshaDii, hicho kipengele cha kwanza ulichokiongelea kimenigusa, na inatokea sana hapa jamvini, kwamba wanafahamia kivyao huko wakija humu wanabakia kutetea maujinga yaliyo wazi kabisa, kuna siku nilisoma mada fulani humu mdada/mmama anatetea upuuzi kwa kuingia ishu ya kijinga kabisa, mtu anamkosoa mtoa mada kwa wema tu, kwamba mada zake zimekaa kama kuhamasisha kuchuna, kuwa na wanaume wenye pesa etc, we unasema ooh umjui fulani, kwenye mazingira halisi hayupo hivyo unavyomfikiria,kwanza umkome kabisa, i was like gosh! nilikuwa namheshimu sana huyo member aliyom attack huyo jamaa alivyo comment yeye anavyoona, nimetokea kumdharau sana, kujuana kwenu kwa namna yoyote ile inamzuia nini member mwingine asikosoe, na nilikuwa nataka kumjibu huyo mdada/mmama alienunua kesi ila nashukuru network siku hiyo ilikuwa kimeo kabisa, mana angenisababishia ban!
naikumbuka vizuri sana hiyo issue.......
ikabidi nipite kando tu maana.....
 
Ndo muanze sasa kujirekebisha.
Ila kwakweli inafikia kipindi unakutana na vijimaada vya kijinga mpaka unaona kuliko kuwepo humu bora ukaapload photo ya mwanao FB ili uwe unafurahia kuiangalia! lol

Zamani kidogo nilikuwa nikipata stress kwenye jukwaa la siasa nilikuwa nakimbilia humu kujiliwaza, baadaye nikajikuta nakimbia tena humu baada ya kuona most of threads wanajadili ndoa in a negative manner, huku mie nikijifikiria jinsi nilivyokaa kwenye ndoa yapata miongo kadhaa, na haijatetereka, nikifikiria maisha yangu kabla ya ndoa na mafanikio yake, nikaona wacha nisijipotezee.

Maadili yanatakiwa kuheshimiwa zaidi.
 
Thanks kwa post hii, hasa hapo bold.

Hapa kuna kila aina ya watu, na ni ngumu kuwachuja.
Na kila mtu katoka alikotoka kwa tabia yake, ni jinsi ya kudeal nao tu ndio inaweza punguza mada za kitoto

Kuna watu wanaangalia mambo objectively. Lakini pia wapo baadhi ambao wanaangalia mambo subjectively. Wanaamni kuwa kila wanachokifanya basi kinafanywa na kila mtu au kinatakiwa kufanywa au kuaminiwa na kila mtu.

Pia wapo baadhi ya watu wengine wana closed minds. Wanaamini wanachokiamini and they are not prepared to even hear the other side of the coin.

At the same time kuna baadhi ya watu ambao they can’t tolerate. They are not prepared to allow the existence, occurrence, or practice of something that one does not necessarily like or agree with without any interference.

Then kuna baadhi ya watu ambao probably ni attention seeker. Hawa watu wana-seek attention kutoka kwa watu wengine as a form of feedback. Hili siyo tatizo lakini linakuwa tatizo kwa both parties kama hii tabia inakuwa too excessive and inappropriate. Wenyewe wanaita “attention seeking disorder”.

Nikiongezea kwa upande wa Wabongo tunapenda sana kujadili mada za kiudaku udaku. We really love this. Tukisikia, kuona au kuambiwa kitu in private, we can't keep our months shut. But wapo wachache ambao they don’t like this.

Kwa hiyo, unapoweka watu hawa wote kwenye kapu moja lazima kutatokota tuu. Hata hivyo, naamini kuwa watu wa aina hii hawapatikani kwenye social media tuu. Wanapatikana pia mitaani. Tunaishi nao kila siku. Wengine ni ndugu zetu, majirani na marafiki zetu. It is just how we handle them.
 
Afadhali yako mkuu Mungi unaweza kudumu kwenye jukwaa la siasa sisi wengine tukiingia mle tunapata mafua na vikohozi visivyoisha maana yale ya mle ni balaa sehemu pekee iliyokuwa ina afadhali ni MMU sasa nako humu ni balaa jingine
Hapo ndipo unapoona kuwa kuna watu wanajaribu sana kuwaaaminisha watu kuwa ndoa ni balaa na wasijiingize humo na maisha mazuri ni ya ubachelor wakati kuna watu wana ndoa zao na zila kila aina ya mazuri yake
 
Last edited by a moderator:
Asha you keep disapointing me! Unazeeka sasa lol! Huwezi amini sijasoma coment yoyote ila zako tu n im disapointed, ila nakufatilia kwa ukaribu still bet my money in u kwenye huu mjadala.

Well na ukongwe wenu sikutegemea haya mapinduz mnategemea mbeleko ya INVISIBLE!!!!!!!! Hahahaaaaaa! Its not funny though! Like seriosly REPORT ABUSE!

Mi nilijua mmejipanga kupambana kifree market, democratically, kibepari kwaku COMPETE NA MADA ZA MAANA kuprove chipukiz
Ni majanga! Mngeleta challange na vita vya MADA! Sadly hapo waanzisha thread ni 3. As long as hamna thread nzuri na mpya kila mara watu watachangia hizo mbaya mpya zilizopo! Tatizo ni upungufu wa GT na thread zilizoenda shule! Kama iko ya maana watu hawawezi kucomment pumba ila kama hamna well watalazimika.

Mi langu jicho lol!

Nyamayo msamehe Kaunga she just has big faith in people. IT WAS MY FFAULT NA SADLY KUCHUNA IS MY PHILOSOPHY! You shouldnt judge her for 1 statement. She is nice you know!
Sithani kama alikuwa Kaunga, naikumbuka hiyo issue na nina uhakika mtu ambaye Nyamayao anamsema siyo Kaunga....I can bet on this.
Ila nakubaliana na mengi ambayo umeshauri, nadhani the best way to revenge this ni kwa kuanzisha mada zenye "changamoto" ili watu wawe busy na hizo. kama hakuwa mada za kujenga basi watu wataishia kuchangia hizo ambazo tunadhani zinabomoa.
Na hii inachangia sana uchakachuaji wa mada. Mimi nataka kuwa MMU na kuongea huku, through mada, kama nikiona mada zote hazinifurahishi basi naishia ku-chat tu na ambaye nimemkuta, mambo yetu ambayo hata hayahusiani na mada. Inasikitisha sana.
Kitu kingine kinachoudhi ni watu kushambulia mtoa mada badala ya mada yenyewe
 
Last edited by a moderator:
Thanks kwa post hii, hasa hapo bold.

Hapa kuna kila aina ya watu, na ni ngumu kuwachuja.
Na kila mtu katoka alikotoka kwa tabia yake, ni jinsi ya kudeal nao tu ndio inaweza punguza mada za kitoto

Ni kweli Kongosho na hilo ndio tunalolitafuta hatuwezi kuwaondoa wala huwezi kumzuia mtu kuanzisha kile kwake anachokiona cha maana au kilichoko mawazoni mwake ila muhimu ni namna ya kuhandle issue kama hizo bila kumkwaza mtu au kumuonyesha kuwa amedharaulika
 
Last edited by a moderator:
Zamani kidogo nilikuwa nikipata stress kwenye jukwaa la siasa nilikuwa nakimbilia humu kujiliwaza, baadaye nikajikuta nakimbia tena humu baada ya kuona most of threads wanajadili ndoa in a negative manner, huku mie nikijifikiria jinsi nilivyokaa kwenye ndoa yapata miongo kadhaa, na haijatetereka, nikifikiria maisha yangu kabla ya ndoa na mafanikio yake, nikaona wacha nisijipotezee.

Maadili yanatakiwa kuheshimiwa zaidi.
ha haaaa, tatizo kubwa linakuja unapojaribu kuambia kuwa haya mambo siyo kama wanavyoyafikiria unaishia kujibiwa kuwa wewe wa zamani, siku hizi........ au ushauri wako wa zamani, siku hizi....... sasa unajiuliza si ndo tupo hapa kushauriana? ya zamani tunachanganya na ya sasa then mambo yanasonga mbele.
 
Fixed Point tatizo watu wanataka waishi kama Katarina na daniel kwenye tamthilia za kifilipino sasa ukiwaambia hizo ni tamthilia wanakuona wa zamani na umepitwa na wakati na hauko kwenye ulimwengu wa kidigital ila uko analogy
Na ukiwaambia maisha kama hayo hakuna hawataki kusikia wanakuona wa zamani na hapo ndipo unakuja msamiati wewe ushazeeka tuachie sisi vijana
 
Last edited by a moderator:
We will be ignoring you:glasses-nerdy:

Ujue hapa inabidi tukubaliane kuna kil aina ya watu, tena wenye mitizamo tofauti kabisa ya maisha. Na inawezekana wengine tumeshazeeka kiasi kwamba aina ya maisha ya wengine hatuyawezi au hatuyaelewi.

Pamoja na kuwa ku-report abuse ni mojawapo ya njia za kusuluhisha, je mod atakuwa na vigezo gani vya kuondoa uzi? Maana hata mod wanaongozwa kwa sheria zao. Kuna mambo mengine hayakubaliki katika jamii husika lakini hayakatazwi na sheria za jamii hiyo hiyo.

Hii ni headache kwa kweli, ila tukichuana kwa mada hapo twaweza fika.

Bado natafakari itakuwaje.

If it is abt me on not is not the issue at hand! Mi tatizo naliona ila SULUHISHO LENU LA REPORT ABUSE SIO SULUHISHO!!!!!!"""

I am just challanging you Asha n company mje na SOLUTION APPLICABLE!

Report abuse!!!!!!!!!!! Hahahaaaaaaa!
 
Kuna watu wanaangalia mambo objectively. Lakini pia wapo baadhi ambao wanaangalia mambo subjectively. Wanaamni kuwa kila wanachokifanya basi kinafanywa na kila mtu au kinatakiwa kufanywa au kuaminiwa na kila mtu.

Pia wapo baadhi ya watu wengine wana closed minds. Wanaamini wanachokiamini and they are not prepared to even hear the other side of the coin.

At the same time kuna baadhi ya watu ambao they can’t tolerate. They are not prepared to allow the existence, occurrence, or practice of something that one does not necessarily like or agree with without any interference.

Then kuna baadhi ya watu ambao probably ni attention seeker. Hawa watu wana-seek attention kutoka kwa watu wengine as a form of feedback. Hili siyo tatizo lakini linakuwa tatizo kwa both parties kama hii tabia inakuwa too excessive and inappropriate. Wenyewe wanaita “attention seeking disorder”.

Nikiongezea kwa upande wa Wabongo tunapenda sana kujadili mada za kiudaku udaku. We really love this. Tukisikia, kuona au kuambiwa kitu in private, we can't keep our months shut. But wapo wachache ambao they don’t like this.

Kwa hiyo, unapoweka watu hawa wote kwenye kapu moja lazima kutatokota tuu. Hata hivyo, naamini kuwa watu wa aina hii hawapatikani kwenye social media tuu. Wanapatikana pia mitaani. Tunaishi nao kila siku. Wengine ni ndugu zetu, majirani na marafiki zetu. It is just how we handle them.
Umeongea vizuri sana rafiki.....
niliwahi kusema hapa kuwa siku hizi nimejifunza kuchukulia kama tulivyo, sim-judge mtu. nitatumia fursa niliyokuwa nayo kumsaidia mtu pale ninapoona anapotoka (niseme mimi ninapoona anapotoka) kama atakubali na kurekebika sawa, otherwise inabidi ukubaliane naye anachoamini....
lakini hapa sidhani kama tunazungumzia kuwa na mitazamo tofauti. of course hatuwezi kuwa na mitazamo sawa, lazima tunatofautiana. hata vile ambavyo mimi naamini ni vizuri kuna mtu anaamini sipo sahihi, tuheshimu hilo. lakini hapa nadhani tunazungumzia zaidi utoto ulioingia katika jukwaa. mtu anatoka na mtu (hii haikatazwi), hajaridhika naye, anakuja hapa kutuambia kuwa "wanawake/wanaume siku hizi hivi na hivi", sisi yanatuhusu hayo? kwa nini usimwambie huyo mwanamke/mwanaume wako huko huko mlikokutania badala ya kuja kutujazia mada hapa?
 
Sithani kama alikuwa Kaunga, naikumbuka hiyo issue na nina uhakika mtu ambaye Nyamayao anamsema siyo Kaunga....I can bet on this.
Ila nakubaliana na mengi ambayo umeshauri, nadhani the best way to revenge this ni kwa kuanzisha mada zenye "changamoto" ili watu wawe busy na hizo. kama hakuwa mada za kujenga basi watu wataishia kuchangia hizo ambazo tunadhani zinabomoa.
Na hii inachangia sana uchakachuaji wa mada. Mimi nataka kuwa MMU na kuongea huku, through mada, kama nikiona mada zote hazinifurahishi basi naishia ku-chat tu na ambaye nimemkuta, mambo yetu ambayo hata hayahusiani na mada. Inasikitisha sana.
Kitu kingine kinachoudhi ni watu kushambulia mtoa mada badala ya mada yenyewe

what did l miss here???
 
Fixed Point tatizo watu wanataka waishi kama Katarina na daniel kwenye tamthilia za kifilipino sasa ukiwaambia hizo ni tamthilia wanakuona wa zamani na umepitwa na wakati na hauko kwenye ulimwengu wa kidigital ila uko analogy
Na ukiwaambia maisha kama hayo hakuna hawataki kusikia wanakuona wa zamani na hapo ndipo unakuja msamiati wewe ushazeeka tuachie sisi vijana
nilivyo proud sasa na huo uzee wangu, utanitaka, lol!
cc. Dark City
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu King Kokoo III,aliwahi sema mada za utumbo utumbo zinapata wachangiaji wengi sana,ila kwa kweli hali ni mbaya majukwaa yote,kutukanana imekua jambo la kawaida,tokea nimejiunga JF sijui wai mtusi memba,zaidi kubishana kwa hoja,sijui ni malezi au vp sijui
"Vox popoli vox dei"
 
Adharusi sidhani hata kama ni suala la malezi ni yale mazoea kuwa hata nikitukana what will happen na hakuna wa kunifanya kitu
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom