Wana Mbeya, tumkatae Mwabukusi, anatudharau sana

Kwanini ukereke na nguruwe wanatembea Mbeya? Mbona Mwembechai, Buguruni tunakutana na mbuzi wanatembea?

Chuki yenu dhidi ya Mbeya itwaua
Mji wenu ikifika ussiku saa 2 watu wamelala, waliobakia wote mbeya pazuri kunukishana jasho tu
 
Hali ya hewa inafika mpaka 8°Celsius usiku, unataka watu wa Mbeya tuendele kuzurura mjini ili tupate nini hasa??
 
Stockholm ya Ifakara sawa, ila ya Sweden hujafika bro wacha kufunga watu kamba.

Muda wa kawaida wa kulala kwa wakazi wengi wa Stockholm, Sweden ni kati ya saa 5:00 usiku na saa 6:00 usiku (23:00 - 00:00).
Hata hivyo, ratiba hii hubadilika sana kutokana na majira ya mwaka:

-Wakati wa Kiangazi (Summer): Usiku unakuwa mfupi sana na jua linaweza kuwepo hadi saa 4:00 au saa 5:00 usiku. Hali hii hufanya watu wengi kuchelewa kulala, mara nyingi baada ya saa 6:00 usiku, kwa sababu mwili unahisi bado ni mchana.

-Wakati wa Kipupwe (Winter): Giza huingia mapema sana (hata kabla ya saa 9:00 alasiri). Kutokana na giza hili la muda mrefu, watu wengi huwa na mielekeo ya kwenda kulala mapema zaidi ikilinganishwa na wakati wa kiangazi.
AI sio 💯 perfect kiasi cha kumkosoa mtu mwingine.
 
Kwani sio kijiji kikubwa? Rekebisheni sasa Mwabukusi atakosa cha kusema
 
Rais wa TLs Wakili Boniface Mwabukusi amesema Jiji la Mbeya linaonekana tofauti na majiji mengine nchini kutokana na shughuli nyingi za kijamii na kiuchumi kumalizika mapema usiku, kauli ambayo imezua mjadala miongoni mwa wakazi wa jiji hilo na watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Akizungumza katika mahojiano yaliyorushwa kutoka kupitia Mkataba ya Mawio Online TV, Mwabukusi alisema Mbeya ni miongoni mwa maeneo ambayo shughuli nyingi husitishwa mapema kiasi cha kufanya mitaa kuwa mitulivu mapema usiku.

“Mbeya ndiyo sehemu pekee panaitwa jiji lakini watu wote wanalala saa mbili kamili. Ukimkuta mtu anatembea ujue ni mlevi alipotea njia anajitahidi kurudi nyumbani,” alisema Mwabukusi.
Mie naungana naye, ingawa sio kwa 100%. Mbeya kwenye mipango miji ni 0 kabisa. Mji haujapangwa ukapangika. Mbeya kimiundombinu imefeli sana, kuna barabara moja tu kuu (TANZAM). Ikitokea ina dharura hii barabara, namna ya kufika mjini ni shida, rejea shida ikitokea Mlima Nyoka ama Uyole, raia wanahaha pa kupita.
 
Lakini hoja hapa ni watu wa Mbeya kulala saa 2 na siyo ufinyu wa miundombinu. Je ndugu Idimi unadhani watu wa Mbeya wanalala by saa 2 kwa sababu ya ubovu wa miundombinu au kwa sabau ya hali ya hewa ya Mbeya ? Ambayo kwa kipindi hiki cha mwezi wa 8 inacheza kati ya 8°Celsius na 13°Celsius??
 
Rais wa TLs Wakili Boniface Mwabukusi amesema Jiji la Mbeya linaonekana tofauti na majiji mengine nchini kutokana na shughuli nyingi za kijamii na kiuchumi kumalizika mapema usiku, kauli ambayo imezua mjadala miongoni mwa wakazi wa jiji hilo na watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Akizungumza katika mahojiano yaliyorushwa kutoka kupitia Mkataba ya Mawio Online TV, Mwabukusi alisema Mbeya ni miongoni mwa maeneo ambayo shughuli nyingi husitishwa mapema kiasi cha kufanya mitaa kuwa mitulivu mapema usiku.

“Mbeya ndiyo sehemu pekee panaitwa jiji lakini watu wote wanalala saa mbili kamili. Ukimkuta mtu anatembea ujue ni mlevi alipotea njia anajitahidi kurudi nyumbani,” alisema Mwabukusi.
Mnakua mmeshiba parachichi sana kuvimbiwa mnalala mapema...
 
Lakini hoja hapa ni watu wa Mbeya kulala saa 2 na siyo ufinyu wa miundombinu. Je ndugu Idimi unadhani watu wa Mbeya wanalala by saa 2 kwa sababu ya ubovu wa miundombinu au kwa sabau ya hali ya hewa ya Mbeya ? Ambayo kwa kipindi hiki cha mwezi wa 8 inacheza kati ya 8°Celsius na 13°Celsius??
Kulala mapema ni kwa sababu ya hali ya hewa (baridi kali nyakati za usiku).
 
Back
Top Bottom