Wana Mbeya, tumkatae Mwabukusi, anatudharau sana

Wana Mbeya, tumkatae Mwabukusi, anatudharau sana

Wapuuzi wakubwa nyie mbeya pamekaa kishamba sana na hata nature ya watu wa mbeya ni ushamba na ujuaji useless kabida, mji hauna plan kabisa ule
Na wewe kwenu ni wapi? Isije ukaponda Mbeya kumbe kwenu mnaishi kwenye mashimo
 
Ukweli mchungu

Hakuna ukweli wowote kwa maneno ya Mwabukusi. Kabwe, Mwambene, Soweto, Mbeya Pazuri n.k.? Maeneo hayo saa 6:00 usiku huwa bado yapo wazi. Kabwe, kwa mfano, watu hufika saa 1:00 au saa 2:00 ndipo panapokuwa na shughuli nyingi. Sasa Mwabukusi kusema Mbeya saa 2:00 watu wamelala si kweli. Labda kama hajapita maeneo hayo au hajui hali halisi; afanye utafiti kwanza
 
Mh. Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi, unashangaa watu wa Mbeya kulala saa mbili usiku? Kwanza, jiji lile lina ubaridi mkali wa hadi nyuzijoto 8°C au 10°C nyakati za usiku, siyo joto la huko unakozurura. Pili, usiku ni wakati wa kupumzika baada ya kazi ngumu ya uzalishaji, na siyo muda wa kuzurura barabarani bila mpango.
Zamani, wakati wa sakata la DP World, tulikuona una akili na unaongea pointi za maana sana. Kumbe ulikua unatafuta kiki tu! Siku hizi umepoteza mwelekeo kabisa na umekuwa mropokaji asiye na sifa, unayeongea maneno yasiyo na tija kama Mwijaku tu. Mbeya inazalisha kwa akili, haishindi kijiweni!
Punguzeni kupigana miti mapema.
 
Huyo ni mpinga maendeleo wa Jiji letu, Mbeya magorofa tunajenga kila kukicha. Mwabukusi hata kibanda cha saloon hajawai fungua hapa Mbeya. Halafu yasemekana huyu ni mzaliwa wa Arusha. Basi rudi nyumbani kwenu Arusha Tanzania ni kubwa hujalazimishwa kuishi Mbeya. Hana hoja za kuishauri serikali ili iboreshe jiji letu na magorofa tutazidi kuyajenga fala tu huyo
Uko mbeya si ndo mliwekewa lifti kwenye jengo la ghorofa kwa mara ya kwanza 2014 mkashangilia mji mzima?

Mji mpaka downtown kuna nyumba za udongo kibao.

Bado sana huo mji mnaukuza tu.
 
“Mbeya ndiyo sehemu pekee panaitwa jiji lakini watu wote wanalala saa mbili kamili. Ukimkuta mtu anatembea ujue ni mlevi alipotea njia anajitahidi kurudi nyumbani,” alisema Mwabukusi.​
Na wewe toka lini umekuwa Mnyakyusa wa Mbeya? Mie nakujua wewe kuwa mtu wa Zanzibar. Au umehamia Mbeya siku hizi?
 
Hiyo sio sababu stockholm hapa , na miji yenye baridi mpaka barafu hawalali mapema kiasi hiko

Hiyo sio excuse
Stockholm ya Ifakara sawa, ila ya Sweden hujafika bro wacha kufunga watu kamba.

Muda wa kawaida wa kulala kwa wakazi wengi wa Stockholm, Sweden ni kati ya saa 5:00 usiku na saa 6:00 usiku (23:00 - 00:00).
Hata hivyo, ratiba hii hubadilika sana kutokana na majira ya mwaka:

-Wakati wa Kiangazi (Summer): Usiku unakuwa mfupi sana na jua linaweza kuwepo hadi saa 4:00 au saa 5:00 usiku. Hali hii hufanya watu wengi kuchelewa kulala, mara nyingi baada ya saa 6:00 usiku, kwa sababu mwili unahisi bado ni mchana.

-Wakati wa Kipupwe (Winter): Giza huingia mapema sana (hata kabla ya saa 9:00 alasiri). Kutokana na giza hili la muda mrefu, watu wengi huwa na mielekeo ya kwenda kulala mapema zaidi ikilinganishwa na wakati wa kiangazi.
 
Itumieni hiyo baridi kama fursa
Muda wa kawaida wa watu kulala mkoani Mbeya, Tanzania ni kati ya saa 3:30 usiku na saa 4:30 usiku (21:30 - 22:30).
Tofauti na Stockholm, muda wa kulala Mbeya haubadiliki kulingana na majira ya mwaka kwa sababu nyakati za kuchomoza na kuzama kwa jua ziko vilevile mwaka mzima. Hata hivyo, ratiba hii inaathiriwa na mambo yafuatayo:

Hali ya Hewa ya Baridi: Mbeya inajulikana kwa kuwa na baridi, hasa nyakati za usiku. Hali hii hufanya watu wengi kuwahi kuingia ndani na kulala mapema ili kujikinga na baridi.

-Shughuli za Kiuchumi: Jamii kubwa ya Mbeya inajihusisha na kilimo, biashara, na ujasiriamali. Watu wengi huwahi kulala ili waweze kuamka mapema sana alfajiri kuanza kazi zao.

-Maisha ya Mijini vs Vijijini: Katika maeneo ya mijini kama Mbeya Mjini (Soweto, Mwanjelwa), baadhi ya watu huchelewa kulala hadi saa 5:00 au saa 6:00 usiku kutokana na biashara na burudani. Maeneo ya vijijini watu huwahi zaidi, mara nyingi kabla ya saa 3:30 usiku.
 
Sasa unapaniki nini mkuu😀😀umeona hata kwenye huu Uzi wako Kuna mtu kakusapoti huu udaga wako?
Kwani misingi ya mjadala ni ipi? Au uhuru wa mawazo una maana gani? Unapimaje ubora wa mada? Ubora wa mada unapimwa kwa number of engagements na siyo kwa namna watu walivyoniunga mkono!!

Sijui ndugu ulisoma shule gani, kadai karo zako wakurudishie
 
Uko mbeya si ndo mliwekewa lifti kwenye jengo la ghorofa kwa mara ya kwanza 2014 mkashangilia mji mzima?

Mji mpaka downtown kuna nyumba za udongo kibao.

Bado sana huo mji mnaukuza tu.
Bado huijui Mbeya. Hata Dar es Salaam kuliko jengeka kupo kama Masaki, Oysterbay na Mbezi au Mikocheni.

Lakini pia kuna swekeni ambako nyumba zimejengwa utafikiri mabanda ya kutunzia mkaa kama Kigogo, Kinondoni shamba, Buguruni Kisiwani, Vingunguti etc

Next time ukienda Mbeya waambie wajomba zako wakupeleke maeneo kama Block Q, VETA, isyesye, Uzunguni, Uhindini, New Forest etc
 
Mimi kwetu jombe , na mbeya ni historia tu
Nyie watu wa Njombe mabingwa wa kuweka wazazi wenu misukule ili mpate utajiri, na hata utajiri wenu hauwasaidii lolote maana mnaishi kufala tu
 
Na wewe toka lini umekuwa Mnyakyusa wa Mbeya? Mie nakujua wewe kuwa mtu wa Zanzibar. Au umehamia Mbeya siku hizi?
Mimi siyo Mnyakyusa bali Msafwa kamili toka Mbeya, Wanyakyusa kawatafute Rungwe na Kyela
 
Aliyoongea ni kweli mbeya hamna kitu, airport inauzwa vibama na mahindi, munalala saa 2 usiku, hamna sehemu za bata ikifika usiku nyote munajazana mbeya pazuri, vumbi limejaa kila kona, Mashamba hadi kati kat ya mji, hakuna mipango miji, mzunguko wa pesa ni mdogo mno bora hata Mtwara,nyumba za udongo zimejaa mjini, routes za Daladala ni 3 sijui 2 tu, Bajaji zimejaa kila kona hawana Ustaarabu na ndio usafiri wenu.

Muache ubishi kubalini, mbeya ni kijiji Kilichoumuka. Chenye vurugu
 
Aliyoongea ni kweli mbeya hamna kitu, airport inauzwa vibama na mahindi, munalala saa 2 usiku, hamna sehemu za bata ikifika usiku nyote munajazana mbeya pazuri, vumbi limejaa kila kona, Mashamba hadi kati kat ya mji, hakuna mipango miji, mzunguko wa pesa ni mdogo mno bora hata Mtwara,nyumba za udongo zimejaa mjini, routes za Daladala ni 3 sijui 2 tu, Bajaji zimejaa kila kona hawana Ustaarabu na ndio usafiri wenu.

Muache ubishi kubalini, mbeya ni kijiji Kilichoumuka. Chenye vurugu
Mbeya Jiji ina rank namba 5 katika GDP (sijui kama unajuwa maana ya GDP) kwa mujibu wa takwimu za TAMISEMI, utasemaje mzunguko wa fedha ni mdogo??
 
Mwabukusi yuko sawa. Mbeya ni kijiji kikubwa
Hata Dar es Salaam ina maeneo yenye maisha duni kama ilivyo Mbeya. Siyo kwamba Dar nzima iko kama Masaki na Oysterbay au Upanga.

Kuna maeneo ni ushenzini sana kama Kinondoni shamba, Mwanyamala Kisiwani, Kigogo, Mburahati, Buguruni Kwamnyamani, Vingunguti, Kowalano Kaliagogo etc
 
Sema mwabukusi naye kaanza kukosa vya kuongelea unawezaje kuuponda namna hiyo mkoa wako hata kama una mapungufu. Mimi nafikiri wenye kuichangamsha Mbeya ni wazawe wenyewe na wengi wao wamemeishia kuishi Dar na mmojawapo ni yeye Mwabukusi. Sasa kama yeye mwenyewe anaishi dar tena kwa kujenga na sio kupanga unataka nani sasa akaichangamshe Mbeya au unataka nani atembee huo usiku wakati watembeaji wenyewe ndo nyinyi na wote mumeishia dar!?
Kasema kweli. Mbeya watu wanawahi sana kufunga biashara na kwenda kulala. Binafsi naona baridi inachangia pia.

Kuhusu miundombinu, ni kweli barabara zinawatia aibu.
 
Back
Top Bottom