Wana-jf nimefiwa na mke wangu!!

Wana-jf nimefiwa na mke wangu!!

Pole sana mkuu. Kumbuka kuwa sisi ni wa Mwenyezi mungu,na kwake ndio marejeo.
 
INNA LILLAH WAINNA ILAIHI RAAJIUU'N... KWAKE MWENYE EZ MUNGU NA KWAKE TU NDIO MAREJEO YETU ! Mola Mlezi akujaalie Subra na akupe nguvu ya kuweza kuhumili muswiba huu mkubwa ! na pia akuwezesha na kukufanyia wepesi wa kuweza kuwalea watoto alokuachia (LULU) ili uwalee katika MAADILI mema na ucha Mungu wa hali ya Juu... Mola awaongoze watoto katika Njia stahiki ... Amin

Pole sana!
 
Inna lilahi wa Inna illahi Rajjun!
Pole sana mkuu. Mungu akupe moyo wa subra na akuwezeshe kushinda uchungu wa kipindi hiki.
Ailaze roho ya marhem mahala pema.

Sisi sote njia ni moja yeye ametangulia sisi tujiandaee.

[/QUOTE]
 
Pole sana Mkuu kwa kuondokewa na kipenzi chako. Mungu akupe faraja kipindi hiki cha majonzi Sajenti
 
Pole sana kamanda. Tunamuomba mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu peponi na wewe na watoto wenu awapatie nguvu yakuweza kukivuka kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana! Mwenyezi Mungu akupe nguvu ya uvumilivu na faraja! Pia,aipumzishe roho ya Marehemu pahala pema!
 
pole mkuu! mungu ampumzishe mahala pema shemeji, wakristo huwa tunaamini mungu atamfufua siku ya mwisho!
kwake tumetoka, na kwake tunarejea..jina la bwana lihimidiwe!
 
Alale pema peponi na we mjilie bwana akupe nguvu katika kipindi hiki cha majonzi
 
polesana mkuu
natumaini biblia inasema mjane mpaka afikishe 60 yrs na weweujafika MUNGU AKUPE UVUMILIVU UPATE WA KUANZIA KABLA YA PASAKA MKUU NAJUA INACHUKUA MUDA KUSAHAU
 
Nasikitika kuwafahamisha kuwa nimepata msiba leo alfajiri mke wangu kipenzi amenitoka. Kimsingi mazishi yamefanyika leo saa 10 kwenye makaburi ya changanyikeni...wife ameniachia watoto wawili wa kike 11 & 8.

Pole sana mkuu na Muumba akutangulie katika kipindi hiki kigumu cha majonzi
 
Pole sana Mkuu,Mungu akupe moyo wa ustahimilivu akupitishe kwenye kipindi hiki kwa amani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom