Wana-jf nimefiwa na mke wangu!!

pole sana mkuu.nakuombea kwa Mola akutie nguvu kipindi hiki cha majonzi na kigumu kwako
 
Pole sana mkuu. ndo nilikuwa najiuliza kulikoni Sajenti haonekani kisana sana jamvini - kumbe ndo hivyo. Mungu akupe nguvu za kuhimili mtikisiko huu na Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya marehemu. Amina
 
May the lord rest her soul in peace Amen. Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu sana kwako, yeye katangulia sisi tutafuata.
 
pole sana kwa msiba mkuu...mungu akupe moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki cha majonzi
 
Innalillah wayna ilayh rajiun. Mbele yake, nyuma yetu. Mungu akupe moyo wa subra.
 
Mkuu pole xana na Mungu akutangulie ktk ths hard tym u r facing.....yeye aliyeziumba mbingu na nchi na akupe ujacri wa kuyashinda majaribu!
 
Pole sana Brother Sajenti kwa Msiba ulio kupata.

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
(إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ)

'Surely we belong to God and to Him shall we return'.
 
Pole sana Mkuu. Mwenyezi akujalie nguvu na ustamilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Sie wote tu wasafiri tujiandae muda wetu ukifika
 
Back
Top Bottom