Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 5,361
- 11,517
Genta huwa unaandika utoto utoto sana. Yaani hata ukitumia ID nyingine akili inabakini chafu na kisodaYaani inawezekana vipi dakika hizi hizi 20 mnazotupa tukiwa tumesimama Mombo au Msamvu au Singida Sisi Abiria wenu tuweze kuzigawa Kiustadi kwa Kula, Kukojoa na Kunya wakati tukifika tu haya maeneo tunakuwa Abiria wengi na waliotutangulia pia Kihuduma?
Kwani mkisema tu kuwa muda wa Kula na Kujisaidia Huduma zingine Muhimu za Kibinadamu ( kama za Kukojoa na Kunya njiani Safarini ) uwe ni dakika 30 au 45 mtapungukiwa nini?
Matokeo yake kwa hii Roho Mbaya yenu ya kutupa hizi dakika 20 njiani na Kutuwahishia Abiria kurudi katika Mabasi tuendelee na Safari wengine tunajikuta tunakula ndani ya Mabasi kwa Presha huku tunakunya na Kujinyea vile vile ila Siti zenu tu huwa zinatusaidia Kutusitiri mpaka tufikapo mwisho wa Kituo.
Na hakuna Kitendo ambacho KEROZENE nakichukia kama unakuta Abiria umemuomba Kondakta na Dereva unataka Kukojoa halafu unashuka na unaanza Kufungua Zipu ili uuchomoe 'Mkurudungu' wako ukojoe unasikia Dereva anakupigia Honi matokeo yake kwa Kitete ( Presha ) unajikuta unakojoa kidogo tu au unaacha na kujikuta ukianza Kukimbia kuwahi ndani ya Basi huku Ukijamba hovyo Porini hadi unawashtua Vicheche waliojipumzisha, Suruali umeishikilia ikiwa Magotini na kuja Kuvalia vizuri ndani ya Gari mlangoni huku Abiria Wenzako wakikukodolea tu Mubashara.
SUMATRA tafadhalini ongeeni na TABOA kuwa Abiria tunateseka na hizi dakika zao 20 tu wanazotupa tukiwa njiani na sasa tunataka tupewe ama dakika 30 au 45 ili tuweze Kujinafasi vizuri kwa Huduma zote Tatu muhimu za Kula, Kukojoa na Kunya ndipo tuwe tunaendelea na Safari zetu.
Hizi dakika zao 20 Kimahesabu tu hata kama ukiwa ni 'Mathematician' utazigawa vipi kwa Foleni ya Chakula unayoikuta? Kwa Foleni ya Watu Kukojoa katika Vyoo vichache achilia mbali wale ambao unawakuta nao wanataka Kunya ila wamekuta wameshawahiwa na wanaojua Kunya wakiwa Wanaguna tu Vyooni, kutoka haraka hawatoki na hata wakitoka utaambulia Msonyo na Bonge la Kimba linakukaribisha ili Kwanza ulione ndipo 'Uliflashi' likuage ndipo nawe uanze Kushughulikia na lako lililoko Tumboni na linataka kutoka?