KERO ZA USAFIRI: Umekumbana na kero gani kwenye harakati za usafiri?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Wakuu,

Usafiri wa umma una vimbwanga yake, unaweza kukutana na jambo mpaka ukatamani ungekuwa na gari lako ili usikutane na masaibu hayo!

Mabasi machafu, wazee wa kubadili ruti na kusema magari hayaendi hasa kukiwa na watu wengi kituoni ni baadhi ya kero nilizokutana nazo kwenye usafiri huu wa jumuiya.

Vipi kwako, ipi/zipi ni kero zako kwenye matumizi ya usafiri wa umma? Wazee wa kupiga mwewe tunasubiri kero zenu pia😃

====

Wewe abiria unajua haki zako? Kwa uelewa zaidi soma hapa;

HAKI ZA ABIRIA NA WAJIBU WA WATOA HUDUMA YA USAFIRI KWA MUJIBU WA KANUNI ZA SUMATRA ZA USAFIRISHAJI ABIRIA ZA MWAKA 2017

Utangulizi

Mwaka 2017 Waziri wa Uchukuzi alifanyia marekebisho kanuni za usafirishaji wa abiria kwa njia usafiri wa mabasi na kanuni hizo kuchapishwa katika gazeti la Serikali nambari 421 la tarehe 06.10.2017. Leo tutaona je kwa mujibu wa kanuni hizo zipi ni haki za abiria na upi ni wajibu wa mtoa huduma. Mtoa huduma ni mtu yeote au taasisi iliyopewa leseni na SUMATRA kutoa huduma ya usafiishaji abiria.

HAKI ZA ABIRIA

Kwa mujibu wa kanuni hizo, abiria ana haki zifuatazo, ambazo kwazo ni wajibu wa mtoa huduma kwa abiria.

1. Haki ya kupanda gari lililo na uzima au kufaa kutembea barabarani. Mtoa huduma anatakiwa kuhakikisha kuwa gari analotumia kusafirishia abiria sio bovu(Kanuni 23(1)(a));

2. Haki ya kuendeshwa na dereva wawili wanaopokezana ikiwa safari hiyo inazidi masaa 8 tangu kuanza kwa safari. Kanuni 23(1)(c).

3. Haki ya kusafiri kwenye gari lililo safi na lenye sehemu za kutupia takataka na mikanda kuwa misafi (Kanuni 23(1)(f)); (Kanuni 25(a)(v));

4. Haki ya kusafiri kwenye gari lisilobeba mizigo ya hatari inayoweza kuhatarisha usalama wa abiria, kama vile gesi, bati, misumari, nk. (Kanuni 23(2)(a));

5. Haki ya kusafiri kwenye gari ambalo limepakia abiria kulingana na idadi iliyopo kwenye leseni ya usafirishaji. Kwa maana ya kwamba gari lisizidishe abiria. (Kanuni 23(2)(b));

6. Haki ya kusafiri katika gari ambalo burudani zinazotolewa wakati wa safari zinaendana na mila na tamaduni za Tanzania na zinatolewa kwa sauti ya chini. (Kanuni 23(2)(c));

7. Haki ya kuendeshwa na dereva anayejali na kuzingatia sheria za usalama barabarani na sheria nyinginezo. (Kanuni 23(2)(d));

8. Haki ya kuhudumiwa na mhudumu ambaye ni msafi na aliyevaa sare nadhifu. (Kanuni 24(1)(b));

9. Haki ya kutobughudhiwa kwenye basi na watu wanaofanya biashara, wanaohubiri injili au kuendesha shughuli au kampeni za kisiasa kwenye basi au kuonesha burudani zilizo kinyume na maadili ya na utamaduni wa mtanzania na kwa sauti ya juu. (Kanuni 24(1)(b)(ii)); (Kanuni 25(b)(iii));

10. Haki ya kupitishwa kwenye ruti ya gari iliyopangiwa na mamlaka na ruti hiyo isikatishwe kabla ya kufika mwisho wa safari. (Kanuni 24(1)(iii)(iv)); 25(b)(viii&ix)); Kanuni 42(1)

11. Haki ya kuuziwa tiketi halali;

12. Haki ya kumfahamu dereva na wahudumu wengine wa basi kupitia vitambulisho vyao. (Kanuni 25(b)(vi));

13. Haki ya basi kusimama kwenye vituo lililopangiwa ambapo kuna choo na huduma nyingine. (Kanuni 25(b)(vii));

14. Haki ya kuelezwa utaratibu wa safari kabla ya gari kuondoka. Kanuni ya 25(b)(x));

15. Haki ya kutozwa na kulipa nauli halali kama ilivyoidhinishwa na SUMATRA kulingana na daraja alilopanda. Kanuni ya 31 na kanuni ya 35;

16. Haki ya kupewa tiketi inayoeleza yafuatayo:

A. Kwa upande wa mabasi ya mikoani nay ale ya nchi nan chi
(i) Jina la abiria na nambari ya siti
(ii) Muda wa kuripoti na muda wa kuondoka
(iii) Kituo cha kuondokea, ruti litakayopita basin a mwisho wa basi
(iv) Nauli
(v) Anwani na namba za simu za msafirishaji
(vi) Namba ya usajili ya gari
(vii) Tarehe ya tiketi kutolewa na tarehe ya safari
(viii) Nambari za dharula za SUMATRA na Polisi
(ix) kodi maalumu ya kuulizia nauli halali ya SUMATRA
(x) Namba za simu za mtoa huduma

B. Kwa upande wa mabasi ya mijini
(i) Namba za usajili wa gari
(ii) Jina la ruti itakayopitwa
(iii) Nauli
(iv) Jina na anwani ya msafirishaji
(v) Tarehe ya kutolewa tiketi
(vi) Namba za simu za msafirishaji

17. Haki ya kurejeshewa nauli yote iwapo ameahirisha safari saa 24 au Zaidi kabla ya siku ya safari. Kanuni 33(5)

18. Haki ya kurejeshewa 25% ya nauli au kubadilisha tarehe ya safari iwapo amefanya maamuzi ya kuahirisha au kubadili tarehe ya safari muza usiopungua masaa 12 kabla ya safari. Kanuni 33(6)

19. Haki ya kupewa usafiri baada ya kukata tiketi. Kanuni 36(1)

20. Haki ya kurejeshewa nauli yote iwapo msafirishaji ameshindwa kuondoa basi ndani ya saa 1 tangu muda wa kuondoka ulioainishwa kwenye tiketi, ispokuwa tu kama abiria kwa hiyari yake ataamua kusubiri apewe usafiri mbadala. Kanuni 36(2)(a)

21. Haki ya kupewa usafiri mbadala au kurejeshewa nauli yote au kupewa chakula na malazi ndani ya masaa 2 iwapo basi limeharibika njiani. Kanuni 36(2)(b)

22. Haki ya kupakia bure bila kulipia mzigo mmoja usiozidi kilo 20 kwa abiria wanaosafiri katika ya mji na mji au nchi nan chi. Mzigo huo usizidi kimo cha sentimita 60, urefu wa sentimita 45 na upana wa sentimita 30. Na kama abiria ni mlemavu basi atakuwa na haki ya kusafirishiwa bure vifaa vyake vinavyomsaidia kwenye ulemavu, kama vile baiskeli ya kutembelea. Kanuni 38(1)(a) na (b)

23. Haki ya kulipia mzigo uliozidi kilo 20 baada ya kupimwa na msafirishaji. Kanuni 38(2)

24. Haki ya kuhifadhiwa mzigo wake vizuri na mahali salama na kupewa mwisho wa safari. Kanuni 40(b)

25. Haki ya kulipwa fidia ya mzigo wake iwapo mzigo umepotea au umeharibiwa kwa uwiano wa thamani ya mzigo ndani ya siku 30 tangu abiria aliporipoti amepotelewa na mzigo au mzigo wake kuharibika safarini na kuwasilisha ushahidi wa kuwa na mzigo huo. Kanuni 40(c)

26. Haki ya abiria mtoto wa chini ya umri wa miaka 3 au chini yake kutolipa nauli kwenye mabasi ya mji kwa mji au nchi nan chi.

Mtoa huduma/msafirishaji yeyote atakayekiuka masharti ya leseni ya usafirishaji, iwe ni yeye mwenyewe au wafanyakazi wake au wakala wake, atakuwa anatenda kosa na atalazimika kulipa faini isiyopungua shilingi laki 2 na isiyozidi shilingi laki 5 au kutumikia kifungo cha kisichopungua mwaka 1 jela na kisichozidi miaka 2 au vyote kwa pamoja.[Kif.43(1)] Bila kujali masharti ya kifungu 43(1), mtoa huduma hataruhusiwa kuajiri mtu yeyote ambaye ametenda makossa ya kukiuka kanuni hizi za usafirishaji zaidi ya mara tatu katika kipindi cha uhai wa leseni yake.

Imetafsiriwa na RSA Tanzania
 
mimi huwa namkakati wangu nikiamua kupanda usafiri wa umma huwa napambana nikae siti ya mbele opposite na driver. Kisha nafungua apps zangu naanza kusoma.
Yanayoendelea huko nyuma sijali.
 
mimi huwa namkakati wangu nikiamua kupanda usafiri wa umma huwa napambana nikae siti ya mbele opposite na driver. Kisha nafungua apps zangu naanza kusoma.
Yanayoendelea huko nyuma sijali.
Umetisha, sasa ikitokea umekaa siti nyingine za kawaida huwa unafanyaje?
 
Wakuu,

Usafiri wa umma una vimbwanga yake, unaweza kukutana na jambo mpaka ukatamani ungekuwa na gari lako ili usikutane na masaibu hayo!

Mabasi machafu, wazee wa kubadili ruti na kusema magari hayaendi hasa kukiwa na watu wengi kituoni ni baadhi ya kero nilizokutana nazo kwenye usafiri huu wa jumuiya.

Vipi kwako, ipi/zipi ni kero zako kwenye matumizi ya usafiri wa umma? Wazee wa kupiga mwewe tunasubiri kero zenu pia😃
Tabia nyingi mbovu huchangiwa na sisi raia (watz) wenyewe. Sisi si raia wenye kuwajibika. Utashangaa coaster imejaa, bado watu wawili au mmoja tu. Mnaweza kuwasubiri hao kwa saa hata mbili. Mmekaa kama mawe ,wala hamfurukuti. Utawaonea huruma wenye watoto wadogo wakianza kulia kwa njaa na adha za garini.

Kwakuwa baadhi ya ruti fupi hazina muda maalumu wa kuondoka na kufika, basi ni busara mgawane huo muda kati ya watoa huduma na abiria. Isiwe kwa upande mmoja tu. Tuwe wakali.
 
Changamoto hii tunaikumba Mara nyingi kwenye vyombo vya usafiri na kutokana na abilia kuwa waoga na kutokuwa na msimamo ndio maana wanaingia kwa magari hayo
 
Wakati mwingine wanaongeza nauli mnapokuwa wengi ama usiku unapoingia. Na sisi abiria huona kawaida sana, unakubali nauli mpya uende nyumbani.
 
Yaan ukija hapa kwa daladala za KIGAMBONI ni kero kubwa sana.. unakuta gari inatakiwa kushusha ipakie kuelekea MKURANGA au VIKINDU... au TUANGOMA.. wanakata route.. wanaishia KIBADA... aafu wanarudi tena Ferry... Kwa ule ukweli wanatutesa sana
 
Ni kweli wanatukera sana sisi abiria, kondakta mwingine unamkuta amevaa headphones hasa hawa wa long safari hana habari na abiria kabsaa akisha kagua ticket.
 
Mm hua nachukia kukaa siti moja na mama juniors. Unakuta nmenunua zangu kiepe na nyama najilia Mara junior ananipokonya nyama na mbaya zaidi mama junior Hana habari na kitendo hiyo. Na akijitahidi sana atasema junior utammalizia anko nyama
 
Back
Top Bottom