Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani, kwanini mnatutesa na kutukomoa Abiria wenu katika dakika 20 za huduma mnazotupa mkisimama njiani?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Yaani inawezekana vipi dakika hizi hizi 20 mnazotupa tukiwa tumesimama Mombo au Msamvu au Singida Sisi Abiria wenu tuweze kuzigawa Kiustadi kwa Kula, Kukojoa na Kunya wakati tukifika tu haya maeneo tunakuwa Abiria wengi na waliotutangulia pia Kihuduma?

Kwani mkisema tu kuwa muda wa Kula na Kujisaidia Huduma zingine Muhimu za Kibinadamu (kama za Kukojoa na Kunya njiani Safarini) uwe ni dakika 30 au 45 mtapungukiwa nini?

Matokeo yake kwa hii Roho Mbaya yenu ya kutupa hizi dakika 20 njiani na Kutuwahishia Abiria kurudi katika Mabasi tuendelee na Safari wengine tunajikuta tunakula ndani ya Mabasi kwa Presha huku tunakunya na Kujinyea vile vile ila Siti zenu tu huwa zinatusaidia Kutusitiri mpaka tufikapo mwisho wa Kituo.

Na hakuna Kitendo ambacho KEROZENE nakichukia kama unakuta Abiria umemuomba Kondakta na Dereva unataka Kukojoa halafu unashuka na unaanza Kufungua Zipu ili uuchomoe 'Mkurudungu' wako ukojoe unasikia Dereva anakupigia Honi matokeo yake kwa Kitete ( Presha ) unajikuta unakojoa kidogo tu au unaacha na kujikuta ukianza Kukimbia kuwahi ndani ya Basi huku Ukijamba hovyo Porini hadi unawashtua Vicheche waliojipumzisha. Suruali umeishikilia ikiwa Magotini na kuja kuvalia vizuri ndani ya Gari mlangoni huku Abiria Wenzako wakikukodolea tu Mubashara.

SUMATRA tafadhalini ongeeni na TABOA kuwa Abiria tunateseka na hizi dakika zao 20 tu wanazotupa tukiwa njiani na sasa tunataka tupewe ama dakika 30 au 45 ili tuweze Kujinafasi vizuri kwa Huduma zote Tatu muhimu za Kula, Kukojoa na Kunya ndipo tuwe tunaendelea na Safari zetu.

Hizi dakika zao 20 Kimahesabu tu hata kama ukiwa ni 'Mathematician' utazigawa vipi kwa Foleni ya Chakula unayoikuta? Kwa Foleni ya Watu Kukojoa katika Vyoo vichache achilia mbali wale ambao unawakuta nao wanataka Kunya ila wamekuta wameshawahiwa na wanaojua Kunya wakiwa Wanaguna tu Vyooni, kutoka haraka hawatoki na hata wakitoka utaambulia Msonyo na Bonge la Kimba linakukaribisha ili Kwanza ulione ndipo 'Uliflashi' likuage halafu nawe uanze Kushughulikia na lako lililoko Tumboni na linataka kutoka?
 
Mabasi yapo tofauti kulingana na aina ya abiria. Kuna yale luxury kwaajili ya abiria wasiokua na haraka(mf. kina mama na wazee), haya hukaa hotelini muda usiopungua nusu saa.

Na kuna yale ya kawaida kwaajili ya abiria wanaowahi wanapokwenda (mf. wafanyabiashara na vijana), haya hotelini ni dkk (8-10) tu. Hivyo mtoa mada uchaguzi ni wako upande basi lipi.
 
Juzi kati nilipanda Happy Nation naenda Mwanza, kufika Morogoro pale Kitungwa, asubuhi basi zote za Mwz, Dodoma, Kahama, Bukoba, zimepaki pale, vyoo matundu 30, abiria 2,000..

Kuna mama mahoni yale, kapagawa, kakimbilia basi letu, kapaniki, kasahau hata jina la basi lake, anachokumbuka ni jekundu na alimuacha mwanaye kiti cha nyuma, tukamuacha Msamvu polisi, sijui alimpata mwanaye!

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Kuna moja niliwakomoa natokea Dar es salaam kwenda Dodoma, nimemwambia kondakta asimamishe bus, alivyosimamisha nikashuka, kumbe na abiria wengine walikua hoi ni vile walikuwa hawawezi kusema, watu wote wamemaliza haja zao mimi bado, nakumbuka nilikaa zaidi ya dakika 30 hv, dereva alipiga honi wapi mimi ndiyo kwanza tumbo limeanza , walinisubiri hadi nikamaliza, wakati narudi kwenye bus watu wote wamenikodolea macho, konda analalamika eti nimewachelewesha, nikamuambia wakati mnachukua nauli mbona hamkusema nawachelewesha na rudisheni nauli nusu nipande gari nyingine, kama hamurudishi lazima msikilize shida yangu, tangia hapa maneno yakaisha na safari ikawa murua, abilia kadhaa walinishukuru walikuwa wamezidiwa kwelikweli .

Siku nyingine nasafiri,nilicheka sana, binti alitaka kujikojolea eti anaogopa kumuomba konda asimamishe gari, ikabidi niingilie kati nikamfuata konda na dereva nikawaambia simamisheni gari kuna mtu amebanwa mnataka akojoe humu, wakasimamisha.

Hawa watu wa mabus shida kweli, abilia inakubidi uwe mkali kama una shida ndiyo wanakusikiliza.
 
Mabasi yapo tofauti kulingana na aina ya abiria. Kuna yale luxury kwaajili ya abiria wasiokua na haraka(mf. kina mama na wazee), haya hukaa hotelini muda usiopungua nusu saa. Na kuna yale ya kawaida kwaajili ya abiria wanaowahi wanapokwenda(mf. wafanyabiashara na vijana), haya hotelini ni dkk (8-10) tuu. Hivyo mtoa mada uchaguzi ni wako upande basi lipi.
Bus zote ni hivyo hivyo. Hamna cha luxury wala nini, wote wanajikuta wana haraka wao kuliko abiria.
 
Hapa ndio naona sasa maana ya sisi vijana kupitia mafunzo ya ukakamavu JKT au Mgambo sasa dk 20 kula chakula unalalamika hazitoshi upo serious kabisa
Kuna matatizo mengine ukiwa unasafiri hayana mambo ya jkt, suala la tumbo ukiwa unasafiri halina mambo za jkt, Ile ni involuntarily action omba usikutwe na bwana pepsi hiyo jkt inayeyuka na haitakusaidia.
 
Mabasi yapo tofauti kulingana na aina ya abiria. Kuna yale luxury kwaajili ya abiria wasiokua na haraka(mf. kina mama na wazee), haya hukaa hotelini muda usiopungua nusu saa. Na kuna yale ya kawaida kwaajili ya abiria wanaowahi wanapokwenda(mf. wafanyabiashara na vijana), haya hotelini ni dkk (8-10) tuu. Hivyo mtoa mada uchaguzi ni wako upande basi lipi.
Hayo magari kwaajili ya wazee na wamama wasiokuwa na haraka na ya vijana wenye haraka za kibiashara yameanza kutofautishwa lini?

Mimi sijui tofauti zao na kuwa ni yapi.

Msaada tafadhali.
 
Yaani inawezekana vipi dakika hizi hizi 20 mnazotupa tukiwa tumesimama Mombo au Msamvu au Singida Sisi Abiria wenu tuweze kuzigawa Kiustadi kwa Kula, Kukojoa na Kunya wakati tukifika tu haya maeneo tunakuwa Abiria wengi na waliotutangulia pia Kihuduma?

Kwani mkisema tu kuwa muda wa Kula na Kujisaidia Huduma zingine Muhimu za Kibinadamu ( kama za Kukojoa na Kunya njiani Safarini ) uwe ni dakika 30 au 45 mtapungukiwa nini?

Matokeo yake kwa hii Roho Mbaya yenu ya kutupa hizi dakika 20 njiani na Kutuwahishia Abiria kurudi katika Mabasi tuendelee na Safari wengine tunajikuta tunakula ndani ya Mabasi kwa Presha huku tunakunya na Kujinyea vile vile ila Siti zenu tu huwa zinatusaidia Kutusitiri mpaka tufikapo mwisho wa Kituo.

Na hakuna Kitendo ambacho KEROZENE nakichukia kama unakuta Abiria umemuomba Kondakta na Dereva unataka Kukojoa halafu unashuka na unaanza Kufungua Zipu ili uuchomoe 'Mkurudungu' wako ukojoe unasikia Dereva anakupigia Honi matokeo yake kwa Kitete ( Presha ) unajikuta unakojoa kidogo tu au unaacha na kujikuta ukianza Kukimbia kuwahi ndani ya Basi huku Ukijamba hovyo Porini hadi unawashtua Vicheche waliojipumzisha, Suruali umeishikilia ikiwa Magotini na kuja Kuvalia vizuri ndani ya Gari mlangoni huku Abiria Wenzako wakikukodolea tu Mubashara.

SUMATRA tafadhalini ongeeni na TABOA kuwa Abiria tunateseka na hizi dakika zao 20 tu wanazotupa tukiwa njiani na sasa tunataka tupewe ama dakika 30 au 45 ili tuweze Kujinafasi vizuri kwa Huduma zote Tatu muhimu za Kula, Kukojoa na Kunya ndipo tuwe tunaendelea na Safari zetu.

Hizi dakika zao 20 Kimahesabu tu hata kama ukiwa ni 'Mathematician' utazigawa vipi kwa Foleni ya Chakula unayoikuta? Kwa Foleni ya Watu Kukojoa katika Vyoo vichache achilia mbali wale ambao unawakuta nao wanataka Kunya ila wamekuta wameshawahiwa na wanaojua Kunya wakiwa Wanaguna tu Vyooni, kutoka haraka hawatoki na hata wakitoka utaambulia Msonyo na Bonge la Kimba linakukaribisha ili Kwanza ulione ndipo 'Uliflashi' likuage ndipo nawe uanze Kushughulikia na lako lililoko Tumboni na linataka kutoka?
Unajiendekeza! Ukipewa dk 45 utataka dk 90.
Safarini mnataka mmpewe muda wa kula hadi kande!
 
Kuna moja niliwakomoa natokea Dar es salaam kwenda Dodoma, nimemwambia kondakta asimamishe bus, alivyosimamisha nikashuka, kumbe na abiria wengine walikua hoi ni vile walikuwa hawawezi kusema, watu wote wamemaliza haja zao mimi bado, nakumbuka nilikaa zaidi ya dakika 30 hv, dereva alipiga honi wapi mimi ndiyo kwanza tumbo limeanza , walinisubiri hadi nikamaliza, wakati narudi kwenye bus watu wote wamenikodolea macho, konda analalamika eti nimewachelewesha , nikamuambia wakati mnachukua nauli mbona hamkusema nawachelewesha na rudisheni nauli nusu nipande gari nyingine, kama hamurudishi lazima msikilize shida yangu, tangia hapa maneno yakaisha na safari ikawa murua, abilia kadhaa walinishukuru walikuwa wamezidiwa kwelikweli .

Siku nyingine nasafiri,nilicheka sana, binti alitaka kujikojolea eti anaogopa kumuomba konda asimamishe gari, ikabidi niingilie kati nikamfuata konda na dereva nikawaambia simamisheni gari kuna mtu amebanwa mnataka akojoe humu, wakasimamisha.

Hawa watu wa mabus shida kweli, abilia inakubidi uwe mkali kama una shida ndiyo wanakusikiliza.
Dk 30 unazijua kweli!
 
ndio hivyo tu umasikini, ila ilipaswa kama unakwenda Mwanza, unapanda gari mpaka dodoma unapumzika pale kuanzia mchana mpaka kesho yake asubuhi, unakula bata kidogo na kunyoosha mgongo, ukianza safari dodoma unakwenda kulala nzega, na siku tatu unamalizia Mwanza...
 
Kuwe na mabasi ya Luxury yenye vyoo ndani kwenye ruti ndefu zote mfano Dar Mwanz, Dar Kahama, Dar Mbeya nk. Abiria achague mwenyewe apande Luxury au Semi Luxury
 
Back
Top Bottom