Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani, kwanini mnatutesa na kutukomoa Abiria wenu katika dakika 20 za huduma mnazotupa mkisimama njiani?

Poleni sana wapanda mabasi tafuteni hela muwe mnakodi hata charter plane nimeumia Sana mnavyoteseka na hawaeawekei magodoro ya kulala na kujinyoosha poleni Sana. I take this personal
 
Watu tunataka kufika mwisho wa safari yetu mapema ww unataka ujinafasi safarini!!, haupo serious ndugu. kwanza shukuru unapata 20minutes, mm tokea nianze kusafiri ni unaambiwa 10dkk kula na kuchimba dawa.
 
Juzi kati nilipanda Happy Nation naenda Mwanza, kufika Morogoro pale Kitungwa, asubuhi basi zote za Mwz, Dodoma, Kahama, Bukoba, zimepaki pale, vyoo matundu 30, abiria 2,000..

Kuna mama mahoni yale, kapagawa, kakimbilia basi letu, kapaniki, kasahau hata jina la basi lake, anachokumbuka ni jekundu na alimuacha mwanaye kiti cha nyuma, tukamuacha Msamvu polisi, sijui alimpata mwanaye!

Everyday is Saturday................................:cool:
hata mm unitokea sana hasa abood za morogolo unaingi KUNYA chalinze
ukitoka unazikuta mbili wkt uliacha 1 aisee uelewi ipi ni ipi sema kwakuwa ni mwanaume na uko shap ukiingia ndani unagundua hii sio faster unakwea nyingine
siku 1 babu mmoja anaenda moro si tunarudi DAR tukambeba tukataka kurudi nae DAR bahati nzuri ile ya mwanzo ilokua haijatoka ila alikuwa kashakaa kabisa kajisahau ni mwenye seat yake ndo kaja kumgutusha wkt huo ndinga ishaingia balabalani inataka kuamsha

yaan safari za abood Dar moro zikikutana gari mbili lazima watu wachanganye tu aisee
 
Hapa ndio naona sasa maana ya sisi vijana kupitia mafunzo ya ukakamavu JKT au Mgambo sasa dk 20 kula chakula unalalamika hazitoshi upo serious kabisa
Hizo tukiwa jkt unalala na kukoroma kabisaa. Maana 20×60sec= 1200 seconds.
Kila tukio gawa suku 60
Kukujoa, kunya, kula na kunawa mikono, unapata karibia 960 kusinzia.
 
Ishirini zote unafanya nini?kapande yale magari ya kawaida yanayofika mwanza sa nane usiku yakitokea dar wakati akina ally's wanafika sa tano kasoro,au yale yanafika arusha sa mbili usiku yakitokea mwanza wakati akina asante rabi wakifika sa 11
kwenye magari hayo utachimba dawa vya kutosha mkuu,
 
Hayo magari kwaajili ya wazee na wamama wasiokuwa na haraka na ya vijana wenye haraka za kibiashara yameanza kutofautishwa lini?

Mimi sijui tofauti zao na kuwa ni yapi.

Msaada tafadhali.
Hata mimi nimesikia leo sijawahi ona luxury wanaoweza kupoteza mda kiasi hicho
 
Hayo magari kwaajili ya wazee na wamama wasiokuwa na haraka na ya vijana wenye haraka za kibiashara yameanza kutofautishwa lini?

Mimi sijui tofauti zao na kuwa ni yapi.

Msaada tafadhali.
Utofauti upo ila sio rasmi wa kutambulika na mamlaka
 
ukitoka nyumbani hakikisha umemaliza kila kitu.
Kama huwezi hakikisha unanunua ndinga yako kukwepa hizo kero.
 
ndio hivyo tu umasikini, ila ilipaswa kama unakwenda Mwanza, unapanda gari mpaka dodoma unapumzika pale kuanzia mchana mpaka kesho yake asubuhi, unakula bata kidogo na kunyoosha mgongo, ukianza safari dodoma unakwenda kulala nzega, na siku tatu unamalizia Mwanza...
Hapa labda uwe mtalii
 
Matokeo ya kuishi in a pithole country,mabasi ya safari ndefu ni lazima yawe na choo ndani kwa ajili ya no 1,na kila baada ya 200km za kusafiri bus linatakiwa kupumzisha abiria kwenye kituo chenye huduma sio porini!vituo vya mafuta vilivyopo kwenye highways ni muhimu viwe na vyoo vya kutosha na huduma zinginezo.

Nilipanda basi moja nikiwa naenda kusini. Safari ya masaa zaidi ya kumi. baada ya masaa manne dereva akasimama porini. Akatangaza Muda wa kuchimba dawa, dakika tano wanawake kulia, wanaume kushoto. Watu wakashuka wa wakatembea kama mita kumi, naona wanawake wanachuchumaa, wanaume wanafungua zipu.

Umbali kati ya wanawake na wanaume ni kama mita tatu. Konda anawahimiza wamalize shughuli chapchap, yuko nervous anasema polisi wanaweza kutokea muda wowote. Dah nilichoka.

Hivi Simba, chui, chatu au mnyama yoyote mfano angetokea, si angeondoka na mtu.
 
Ndio maana bado tuna safari ndefu,tuache siasa uchwara na tufanye maamuzi yanayoshirikisha ubongo,Dar to Mwanza ni kama 1200km huu ni mwendo wa masaa 15 kwa bus,ila kutokana na ubovu wa barabara,huduma za kijamii njiani hamna ni vurugu tupu,ile stendi ya pale Morogoro(nje kidogo ya msamvu)kuna kipindi zinakusanyika bus zaidi ya10 kwa wakati mmoja na kinachotokea pale ni vurugu tupu.
Nilipanda basi moja nikiwa naenda kusini. Safari ya masaa zaidi ya kumi. baada ya masaa manne dereva akasimama porini. Akatangaza Muda wa kuchimba dawa, dakika tano wanawake kulia, wanaume kushoto. Watu wakashuka wa wakatembea kama mita kumi, naona wanawake wanachuchumaa, wanaume wanafungua zipu.

Umbali kati ya wanawake na wanaume ni kama mita tatu. Konda anawahimiza wamalize shughuli chapchap, yuko nervous anasema polisi wanaweza kutokea muda wowote. Dah nilichoka.

Hivi Simba, chui, chatu au mnyama yoyote mfano angetokea, si angeondoka na mtu.
 
Kuna safari moja nilisafiri kutoka dar mpaka mwanza nilikaa seat moja na jimama moja bonge..kila tulipokuwa tukisimama jimama ananunua kitu chochote cha kutia mdomoni....jimama likawa likawa likitaka kujamba linabinua kalio moja...nilipata shida sana wakuu
 
Back
Top Bottom