Wamekataa mahari ya binti yao, tufanyeje?

Wamekataa mahari ya binti yao, tufanyeje?

aisee!
hujajibu swali. kama ni mtihani umefeli kichwa chini miguu juu😛hoto:
Uzuri wa sisi wote tuko hapa hapa dar na wazazi wote wako hapahapa dar kwahiyo process zote zilikuwa hapa hapa ikawa rahisi
 
Kwa haraka haraka naweza kusema ile hamasa kutoka wa upande wa mume haikuwepo kivile na walichukulia ni jambo la kawaida kutokana na uwepo wa muda mrefu katika mahusiano yenu ya kimapenzi maana miaka kumi na tano sio haba ni kama mke tu.

Kitu cha pili niuzembe, hasara zitokanazo na uzembe ni nyingi kuliko faida nandio matokeo yake yamekuwa haya tunayo yashuhudia hapa.Taarifa ilikuwa muhimu sana kwa hatua iliyokuwepo.

Inamaana ukoo wa huyu binti hauna hata wazee wenye busara ambao wanaweza kulichulia hili swala la msiba kwa uzito kiasi fulani?? Hapa panahitaji busara zitumike zaidi kuliko jaziba.

Chakufanya ni kujadiliana nahuyo mchumba wako lenu liwe moja, kimsingi hata nyie pia mnahaki yenu katika maamuzi juu ya swala hili, kwa wazazi huwa ni kama kufuata baraka, na kuwapelekea shukrani, maana baada ya hapo hakuna kinachoendelea zaidi ya wewe kuchukua mke na kaanzisha familia yako.
 
i buy that! Watu wengine wanaishi na mabinti kama ndugu wa damu..

Wewe hapo mbona naona ndio unazamisha kwenye shimo kabisa...!!

Hao watu inaonekana wako kimila zaidi, tafuta mzee wa kibena mwenye busara zake umweleze hii kadhia iliyokukuta, yeye atakushauri vizuri!!
 
Kwa haraka haraka naweza kusema ile hamasa kutoka wa upande wa mume haikuwepo kivile na walichukulia ni jambo la kawaida kutokana na uwepo wa muda mrefu katika mahusiano yenu ya kimapenzi maana miaka kumi na tano sio haba ni kama mke tu.

Kitu cha pili niuzembe, hasara zitokanazo na uzembe ni nyingi kuliko faida nandio matokeo yake yamekuwa haya tunayo yashuhudia hapa.Taarifa ilikuwa muhimu sana kwa hatua iliyokuwepo.

Inamaana ukoo wa huyu binti hauna hata wazee wenye busara ambao wanaweza kulichulia hili swala la msiba kwa uzito kiasi fulani?? Hapa panahitaji busara zitumike zaidi kuliko jaziba.

Chakufanya ni kujadiliana nahuyo mchumba wako lenu liwe moja, kimsingi hata nyie pia mnahaki yenu katika maamuzi juu ya swala hili, kwa wazazi huwa ni kama kufuata baraka, na kuwapelekea shukrani, maana baada ya hapo hakuna kinachoendelea zaidi ya wewe kuchukua mke na kaanzisha familia yako.

sio miaka kumi na tano ni miezi kumina tano..
Asante kwa ushauri wako.
 
inatia shaka kabisa kwani huyo binti alikuwa wapi wakati wwe masahibu ya msiba yamekukumba na nimeona pale kwenye thread yako unasema uko naye mwanza sasa kwani yeye hakujua kuwa umefiwa au ndo mambo ya mjini nini hayo?

kwanini naye huyo binti hakusema kkwao ili hali mnaishi wote huko mwanza kwanini anyamaze kimya kuhusu hilo je unajua kweli huyo binti ana mapenzi ya dhati kwako au ndo mambo yale?

Cha kufanya ni wewe kuwahimiza nduguzo muende iringa mkaombe msamaha ili mambo makubwa yasiwapate tena
 
Habari wana jf?
Nina mchumba wangu kwa takribani,miezi kumi na tano sasa.

Wote tumeajiriwa katika wizara flani nchini.

Yeye kwao Iringa na mimi kwetu Songea,kipindi chote cha mahusiano yetu hatujawahi kwenda kwa wazazi wa pande zote mbili,isipokuwa taarifa zilipelekwa upande wa mwanamke na waliopeleka taarifa ni wazazi wangu wakitokea songea,taarifa ilipokelewa vizuri na wazazi wa mwanamke.

Mahali ilijadiliwa na kukubaliwa na pande zote mbili na tarehe ya kupeleka mahali ilipangwa na wazazi wa mwanamke na kuafikiwa na wazazi wangu.

Tazizo limekuja baada ya tarehe ya mahali kupangwa ambayo ilikuwa tarehe 13/03/2014.Tarehe hiyo ilikuja na matatizo nyumbani tulifiwa na ndugu wa damu hivyo wakatuma mtu akahairishe ,tatizo mtu aliyetumwa bahati mbaya akafika Iringa na kusahau kupitisha taarifa ukweni ,maana yeye ni mtu wa huko iringa.

Tarehe iliyopendekezwa kupeleka mahari baada ya kuhairishwa ni tarehe 3 April mwaka huu.

Kweli tarehe hiyo ilizingatiwa kwa upande wa wazazi wangu waka fika mpaka Iringa na mshenga akiwa mkuu wa msafara,bahati mbaya ukweni hawa kupata taarifa hivyo wakang'aka kupokea ile mahali ambayo kilikuwa kiasi flani cha pesa wakidai kuwa kimila tumewadharau sana na tumejiamulia tu.

Wakaitana wanaukoo na kushauriana wasiipokee licha ya kuwaomba msamaha na kuwaeleza yaliyotusibu wamekataa katakata wanadai KAMA KUOLEWA BINTI YAO ATAOLEWA TUU.

Yaani wamekataa katakata na hawataki kuona nyayo zetu pale.

Juzi mchumba wangu akanishauri tuchukue likizo ya dharura twende kwao.Tukafanya hivyo baada ya kwenda wanaukoo waliitana na kututamkia kuwa kuanzia siku hiyo hatuna mamlaka ya kuishi pamoja na kunambia hivi

Nanukuu, "wewe kijana hauna nafasi ya kuishi na binti yetu tena ,ukoo wenu mmejaa dharau na kiburi,binti yetu ataolewa tu sehemu stahiki".

Kiukweli baada ya kutamkiwa hivyo niliwaeleza wazazi wangu wakaniambia kama ipo ipo tu.
Niliaga nikaondoka lakini walimzuia binti yao kuondoka siku hiyo,yeye aliondoka siku iliyofuata,alipowasili hapa Mwanza alinieleza kuwa wazazi wake wanamsihi aachane na mimi endapo atataka kuendelea kuwa miongoni mwa wanafamilia yao.

Nikamuuliza aumuzi wake kaniambia,hayupo tayari kuwakosea wazazi wake hivyo tufanye kila tuliwezalo kupatanisha ama sivyo itifaki itazingatiwa.

NAOMBENI WASAA WENU JAMANI NIFANYEJE HAPO?

Kuna jamaa mmoja alinambia hapo wanataka fidia nusu mahari kulingana na mila zao Wabena na sie hali ngumu.

Au wana mpango wa kuninyima mke?

Ni habari ya ukweli kabisa.

Suluhisho ulishapewa utoe fine ya nisu mahali mliyokuwa mmekubaliana,badala ya kutekeleza hilo unakuja huku,unataka jf wakuchangie hiyo fine ya nusu mahali?

Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
kwa means zote za mawasiliano zilizopo duniani umeshindwa fikisha ujumbe hapana sikubali kabisa na hoja ya jamaa something not okey. tell me the alll relative walikuwa wanajua kuwa wanaenda kutoa mahari do u think walikuwa wote wamezimia kwa ajili ya kilio wakasahau hilo hapana that family is careless... mbona walikumbuka kuomba ruhusa kazini na kuja kwenye msiba? mbona walikumbuka kuombea ruhusa wanafunzi kwa ajili ya msiba ?... mbona walikumbuka kutoa taarfa za msiba kwa ndugu na marafiki? kwa nini wasahau familia ambayo their about to be a family? think twice...ni kweli wanadharau anataka kutuambia huo msiba ulikuwa amuhsu binti no nono

Point zimesheheni vilivyo!
 
Ni kweli tatuzi lipo hapo, lakini si kiasi cha jukataa mahari. Kwa wazazi ambao hawapendi binti yao awaaibishe hilo ni tatizo linaliongeleka. Nashauri tafuteni wazee kama wawili wa huko Iringa na wawili wa Songea wakaonbe msamaha kama mnapendana kwa dhati na mnayo kweli nia ya kuoana. Zaidi sana muombe Mungu ili upate muongozo wake kama ni mkeo utaoa tu hiyo ni mikwala ya kawaida tu. Kuoa kuna gharama. Usikate tamaa, mkilimaliza hilo ipo siku mtakumbushana na kucheeeka sana na kufurahi
 
Suluhisho ulishapewa utoe fine ya nisu mahali mliyokuwa mmekubaliana,badala ya kutekeleza hilo unakuja huku,unataka jf wakuchangie hiyo fine ya nusu mahali?

Sent from my iPhone using JamiiForums app

wewe bado si muelewa..nimekuambia hiyo faini ya nusu mahali nilitamkiwa na mpangwa mmoja wahuko iringa ,nilimuomba ushauri akaniambia may be wanataka faini ya nusu mahali..wenyewe hawaja tamka..zaidi ya kutaka kuvunja mahusiano ya binti yao.
 
Sasa umejaribu ushauri huo ikashindikana?

Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Sasa umejaribu ushauri huo ikashindikana?

Sent from my iPhone using JamiiForums app

ndomaana nikaja hapa niwa sikie na wenzangu...nashukuru kwa mawazo na ushauri wenu ..nahaidi kuufanyi kazi ..na nitakuja tena katika jukwa hili kuwa juza hatima yake ..lakini kwa sasa lina endeshwa kwan za mikononi mwa wazazi wangu..mie nilisha timuliwa ukweni.
 
Back
Top Bottom