Wamekataa mahari ya binti yao, tufanyeje?

Wamekataa mahari ya binti yao, tufanyeje?

Na wewe na mr leo mlikuwa hamuwasiliani progress? Manake nilitegemea ujue all the way kuwa wageni wamekata kona ipi etc

Uzuri wa sisi wote tuko hapa hapa dar na wazazi wote wako hapahapa dar kwahiyo process zote zilikuwa hapa hapa ikawa rahisi
 
Unajiua nashindwa kuelewa hapa hii ni kweli au umetunga?? Dunia hii ya leo ni ya kutoa maagizo kweli mtu akufikishie ujumbe?? Dunia ya mawasiliano hii mlikosa kupiga simu kutoa taarifa wakati ni kitu serious??? Uyo binti alikua hajui hilo tatizo kwamba umefiwa ili naye asaidie kutoa taarifa kwa wazazi wake??? Hii story utakua umetunga bana haiwezi kuwa dunia tunayoishi sasa. Basi kama ni kweli ww utakua mzembe sana

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Umenisemea yangu ya moyoni bi dada...shkamoo kwanza!...Huyu jamaa na familia yake wajishushe kwanza, kisha waache dharau kwenye mambo ambayo morally wana benefit nayo, wakaombe radhi, na kukubali fine, kisha wa apply kwa mara ya pili...
kabisa mkuu mimi ningekuwa huyo binti ningekimbia wala nisingejaribu ingia ndani loh!!
 
Mshenga wenu nae mzembe yeye ndo alipaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha ujumbe unafika kule haraka iwezekanavyo, manake ndo kazi zao hizo
 
Mi naona hapa haribika kitu.....tumia watu wa dini ambao wapo katika maeneo wanaoishi wazee wa mwanamke...Kama ni waislam mtafute Imam wa msikiti wa hapo...Kama ni wakristo tafuta kanisa wanalofanyia ibada.....ukishindwa ni PM nikusaidie nini ufanye...Pole sana Kijana ni hali ngumu sana najua....Ila pia unatakiwa kuelewa kitu kimoja...Kitu chocho ambacho hakina kheri na Wewe Mwenyezi Mungu hukitafutia sababu ya kukuepuka.....kwa hio isipowezekana pia usiforce....Muombe Mwenyezi Mungu akupe mke mwenye kheri na wewe.....
 
Pole kama ulipangiwa kumuowa utaowa ila kuwa makini na mambo ya lazima
 
Mi naona hapa haribika kitu.....tumia watu wa dini ambao wapo katika maeneo wanaoishi wazee wa mwanamke...Kama ni waislam mtafute Imam wa msikiti wa hapo...Kama ni wakristo tafuta kanisa wanalofanyia ibada.....ukishindwa ni PM nikusaidie nini ufanye...Pole sana Kijana ni hali ngumu sana najua....Ila pia unatakiwa kuelewa kitu kimoja...Kitu chocho ambacho hakina kheri na Wewe Mwenyezi Mungu hukitafutia sababu ya kukuepuka.....kwa hio isipowezekana pia usiforce....Muombe Mwenyezi Mungu akupe mke mwenye kheri na wewe.....

asante ndugu
 
Mkuu sometimes things happen for reason.Inawezekana huyo binti sio haki yako,kwani hicho kikwazo kilichotokea ni chakufa mtu ambacho kinaelekea kutengua hilo linalotaka kutokea(ndoa)bora upotezee tu kwani baadaye utakuja juta kama utalazimisha hilo.jambo jema lolote mara nyingi huwa linakuwa smooth
 
Habari wana jf?
Nina mchumba wangu kwa takribani,miezi kumi na tano sasa.

Wote tumeajiriwa katika wizara flani nchini.

Yeye kwao Iringa na mimi kwetu Songea,kipindi chote cha mahusiano yetu hatujawahi kwenda kwa wazazi wa pande zote mbili,isipokuwa taarifa zilipelekwa upande wa mwanamke na waliopeleka taarifa ni wazazi wangu wakitokea songea,taarifa ilipokelewa vizuri na wazazi wa mwanamke.

Mahali ilijadiliwa na kukubaliwa na pande zote mbili na tarehe ya kupeleka mahali ilipangwa na wazazi wa mwanamke na kuafikiwa na wazazi wangu.

Tazizo limekuja baada ya tarehe ya mahali kupangwa ambayo ilikuwa tarehe 13/03/2014.Tarehe hiyo ilikuja na matatizo nyumbani tulifiwa na ndugu wa damu hivyo wakatuma mtu akahairishe ,tatizo mtu aliyetumwa bahati mbaya akafika Iringa na kusahau kupitisha taarifa ukweni ,maana yeye ni mtu wa huko iringa.

Tarehe iliyopendekezwa kupeleka mahari baada ya kuhairishwa ni tarehe 3 April mwaka huu.

Kweli tarehe hiyo ilizingatiwa kwa upande wa wazazi wangu waka fika mpaka Iringa na mshenga akiwa mkuu wa msafara,bahati mbaya ukweni hawa kupata taarifa hivyo wakang'aka kupokea ile mahali ambayo kilikuwa kiasi flani cha pesa wakidai kuwa kimila tumewadharau sana na tumejiamulia tu.

Wakaitana wanaukoo na kushauriana wasiipokee licha ya kuwaomba msamaha na kuwaeleza yaliyotusibu wamekataa katakata wanadai KAMA KUOLEWA BINTI YAO ATAOLEWA TUU.

Yaani wamekataa katakata na hawataki kuona nyayo zetu pale.

Juzi mchumba wangu akanishauri tuchukue likizo ya dharura twende kwao.Tukafanya hivyo baada ya kwenda wanaukoo waliitana na kututamkia kuwa kuanzia siku hiyo hatuna mamlaka ya kuishi pamoja na kunambia hivi

Nanukuu, "wewe kijana hauna nafasi ya kuishi na binti yetu tena ,ukoo wenu mmejaa dharau na kiburi,binti yetu ataolewa tu sehemu stahiki".

Kiukweli baada ya kutamkiwa hivyo niliwaeleza wazazi wangu wakaniambia kama ipo ipo tu.
Niliaga nikaondoka lakini walimzuia binti yao kuondoka siku hiyo,yeye aliondoka siku iliyofuata,alipowasili hapa Mwanza alinieleza kuwa wazazi wake wanamsihi aachane na mimi endapo atataka kuendelea kuwa miongoni mwa wanafamilia yao.

Nikamuuliza aumuzi wake kaniambia,hayupo tayari kuwakosea wazazi wake hivyo tufanye kila tuliwezalo kupatanisha ama sivyo itifaki itazingatiwa.

NAOMBENI WASAA WENU JAMANI NIFANYEJE HAPO?

Kuna jamaa mmoja alinambia hapo wanataka fidia nusu mahari kulingana na mila zao Wabena na sie hali ngumu.

Au wana mpango wa kuninyima mke?

Ni habari ya ukweli kabisa.

Kama mliyemtuma kutoa taarifa ya kufikwa na msiba ni mwanaume basi ujue nae alimmezea mate huyo mchumba wako ndio maana akavuruga
 
Unajiua nashindwa kuelewa hapa hii ni kweli au umetunga?? Dunia hii ya leo ni ya kutoa maagizo kweli mtu akufikishie ujumbe?? Dunia ya mawasiliano hii mlikosa kupiga simu kutoa taarifa wakati ni kitu serious??? Uyo binti alikua hajui hilo tatizo kwamba umefiwa ili naye asaidie kutoa taarifa kwa wazazi wake??? Hii story utakua umetunga bana haiwezi kuwa dunia tunayoishi sasa. Basi kama ni kweli ww utakua mzembe sana

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

yaani huwezi tofautisha kitu chakubumba na halisia...?
Au hauja ielewa vizuri post?
Nimekuambia binti pamoja na mimi tupo mwanza kikazi suala la mahalili likuwa mikononi mwa wazazi wangu..nao baadaya ya kuona mawasiliano ni tatizo akatumwa mtu ambaye waliamini kabisa taarifa zime fika ukweni ..mbona unakichwa kigumu wakati kichwa chako mkuu ni chepesi?
 
Pia ukizingatia kwa kina....family ya huyu mwanamke ni watu wenye misimamo mikali...kitu ambacho si kizuri katika kuunganisha udugu(family) ....Jaaliza kumetokozea kutokufahamia tayari mkiwa ndani ya ndoa halafu wanakua na misimamo kama hii...unafikiri mnaweza kufikia sulhu kaka? Binadamu lazima tuwe na tabia ya kusameheana na kuchukuliana...tukikizingatia mnataka kufanya jambo la furaha na la kukuza kizazi....be positive kaka!..."unaweza ukalipenda jambo likawa ni shari kwako na unaweza ukalichukia jambo na likawa ni kheri kwako"
 
all ni all huyu mwanaume anamakosa. taarifa haikufika. ni bora hata huyu kijana angeieleka. hata kama mimi nikija kupata binti yangu uniambiae unaleta mahari tarehe 4 niite wazee niite ndugu usitokee bila taarifa alafu uje tarehe 30 na vipesa vyako laki 2. sichukui maana mahali ni suala la heshima sio malipo.

hapa kijasho kina nitoka
 
kutuma mtu ni heshima flani...
Cm iringa mtandao ni shiida siwajua mamba ya voda.

Mlifanya mambo ya kiswahili mlitakiwa mtume ujumbe mzito ukiongozwa na mshenga kwa shughuli ya kutoa taarifa pekee; hiyo faini ya nusu mahari kama huitaki acha binti wa watu vinginevyo amani ndani ya nyumba haitakuwepo. Tekeleza masharti chukua chombo ukitumia mabavu itakula kwako
 
umejidanganya.....angalia usije ukapatwa na matatizo makali ...MUNGU HAPANGIWI BWANA WE FANYA MISIFA TUU.
NYAMAFU WEWE.
misifa ya niini? nyamafu mwenyewe..... tena ndo upewe mwenye matusi kama wewe..... unataka kuonewa huruma kubali umekosa fanya maamuzi na si kuleta ubabe na mfume dume hapa.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom