Wamekataa mahari ya binti yao, tufanyeje?

Wamekataa mahari ya binti yao, tufanyeje?

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
917
Reaction score
597
Habari wana jf?
Nina mchumba wangu kwa takribani,miezi kumi na tano sasa.

Wote tumeajiriwa katika wizara flani nchini.

Yeye kwao Iringa na mimi kwetu Songea,kipindi chote cha mahusiano yetu hatujawahi kwenda kwa wazazi wa pande zote mbili,isipokuwa taarifa zilipelekwa upande wa mwanamke na waliopeleka taarifa ni wazazi wangu wakitokea songea,taarifa ilipokelewa vizuri na wazazi wa mwanamke.

Mahali ilijadiliwa na kukubaliwa na pande zote mbili na tarehe ya kupeleka mahali ilipangwa na wazazi wa mwanamke na kuafikiwa na wazazi wangu.

Tazizo limekuja baada ya tarehe ya mahali kupangwa ambayo ilikuwa tarehe 13/03/2014.Tarehe hiyo ilikuja na matatizo nyumbani tulifiwa na ndugu wa damu hivyo wakatuma mtu akahairishe ,tatizo mtu aliyetumwa bahati mbaya akafika Iringa na kusahau kupitisha taarifa ukweni ,maana yeye ni mtu wa huko iringa.

Tarehe iliyopendekezwa kupeleka mahari baada ya kuhairishwa ni tarehe 3 April mwaka huu.

Kweli tarehe hiyo ilizingatiwa kwa upande wa wazazi wangu waka fika mpaka Iringa na mshenga akiwa mkuu wa msafara,bahati mbaya ukweni hawa kupata taarifa hivyo wakang'aka kupokea ile mahali ambayo kilikuwa kiasi flani cha pesa wakidai kuwa kimila tumewadharau sana na tumejiamulia tu.

Wakaitana wanaukoo na kushauriana wasiipokee licha ya kuwaomba msamaha na kuwaeleza yaliyotusibu wamekataa katakata wanadai KAMA KUOLEWA BINTI YAO ATAOLEWA TUU.

Yaani wamekataa katakata na hawataki kuona nyayo zetu pale.

Juzi mchumba wangu akanishauri tuchukue likizo ya dharura twende kwao.Tukafanya hivyo baada ya kwenda wanaukoo waliitana na kututamkia kuwa kuanzia siku hiyo hatuna mamlaka ya kuishi pamoja na kunambia hivi

Nanukuu, "wewe kijana hauna nafasi ya kuishi na binti yetu tena ,ukoo wenu mmejaa dharau na kiburi,binti yetu ataolewa tu sehemu stahiki".

Kiukweli baada ya kutamkiwa hivyo niliwaeleza wazazi wangu wakaniambia kama ipo ipo tu.
Niliaga nikaondoka lakini walimzuia binti yao kuondoka siku hiyo,yeye aliondoka siku iliyofuata,alipowasili hapa Mwanza alinieleza kuwa wazazi wake wanamsihi aachane na mimi endapo atataka kuendelea kuwa miongoni mwa wanafamilia yao.

Nikamuuliza aumuzi wake kaniambia,hayupo tayari kuwakosea wazazi wake hivyo tufanye kila tuliwezalo kupatanisha ama sivyo itifaki itazingatiwa.

NAOMBENI WASAA WENU JAMANI NIFANYEJE HAPO?

Kuna jamaa mmoja alinambia hapo wanataka fidia nusu mahari kulingana na mila zao Wabena na sie hali ngumu.

Au wana mpango wa kuninyima mke?

Ni habari ya ukweli kabisa.
 
Hivi huko Songea hakuna simu?
Ilitakiwa mpige simu mapema sana ukweni kwako Iringa, mara baada ya ninyi kufiwa na ndugu yenu wa karibu. Biashara ya kutuma mtu Iringa ndio hio inakukosesha mke.
 
Hivi huko Songea hakuna simu?
Ilitakiwa mpige simu mapema sana ukweni kwako Iringa, mara baada ya ninyi kufiwa na ndugu yenu wa karibu. Biashara ya kutuma mtu Iringa ndio hio inakukosesha mke.

kutuma mtu ni heshima flani...
Cm iringa mtandao ni shiida siwajua mamba ya voda.
 
Hapo binti ndiye ana nafasi ya kwanza kuwasihi wazazi wake lakini pia nanyi sasa mtume ujumbe wa kuomba radhi kwa yaliyotokea as long as mambo ya kuoana si kuleta uadui bali udugu!!

Bado suluhu ipo unless huyo binti hana mpango na wewe so atakubali kuondoka kwako bila kujitahidi kutaka suluhu.
 
Hapo binti ndiye ana nafasi ya kwanza kuwasihi wazazi wake lakini pia nanyi sasa mtume ujumbe wa kuomba radhi kwa yaliyotokea as long as mambo ya kuoana si kuleta uadui bali udugu!!

Bado suluhu ipo unless huyo binti hana mpango na wewe so atakubali kuondoka kwako bila kujitahidi kutaka suluhu.

okeeee
 
kutuma mtu ni heshima flani...
Cm iringa mtandao ni shiida siwajua mamba ya voda.

Pole sana.
Kikubwa, mtafute watu wa kule kule Iringa wajaribu kuwaelewesha wakwe kwa mara ya mwisho, ikishindikana basi uachane na binti yao, kwa sababu zilizo wazi kabisa.
 
Uandishi huu unatudhalilisha sisi wangoni Mkuu.....ha ha ha ha ha natania. Jaribuni tena kufuata taratibu husika ili muone kama mlikosea mahali.Yawezekana kuna mambo yalikiukwa au kuachwa kufanywa kimila.Mila za wa-Iringa ni tofauti na wa-Songea
 
Pole sana.
Kikubwa, mtafute watu wa kule kule Iringa wajaribu kuwaelewesha wakwe kwa mara ya mwisho, ikishindikana basi uachane na binti yao, kwa sababu zilizo wazi kabisa.

asante kwa ushauri wako.
 
unaupungufu wa mawasiliano mkuu... mkuu kuna mambo najiuliza uhusiano wako na binti ukoje kiasi kwamba ashindwe kujua kuwa umefiwa? je ulikuwa huna namba hata ya mama mkwe mtarajiwa na kutoa taarifa mapema kuwa umefiwa na si kumtuma mtu manual? kilichokufanya wewe ushindwe kutoa taarifa ni nini?
hata mimi nina wasi wasi ya kuwa wewe na familia yako mnadharau sana tena s kidogo.... kumbuka siku ya mahari yawezekana walijiandaaa hata kwa chakula kidogo na kuita wanaukoo na marafiki huku wakiwasubiria na ninyi amkufika imagine hali waliyokuwa nao .... mkuu jiongeze katika maisha kitu TAARIFA ni muhimu sana ,... jiongeze unasimu jua namna ya kuitumia mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom