Söngea ulipotokea msiba ina maana hata huyo mchumba wako hakujua kuwa umefiwa awataarifu wazazi wake? Je wewe hukuwa na wazo la kutafuta namba zao kuwataarifu? Na kama kutoa taarifa kwa kutuma mtu ni heshima kwanini hamkumtuma mtu aende kwa ishu hiyo badala yake mkamwagiza mtu tuu ambaye alikuwa na safari zake, nazani ishu hamkuichukulia serious na wala siwalaumu hao wabena, tafuta mwafaka mkaombe msamaha kama ikishindikana basi mke sio liziki yako, uje uoe bombambili kuna watoto wazuri, wapo wengine mjimwema, majengo, lizaboni, mfaranyaki ndio kibao hadi matarawe, karibu uoe nyumbani bro.