Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,753
- 5,562
1. Ni kwa mara ya kwanza nafasi ya Katibu mkuu wa chama inapiganiwa (Scramble) na makundi mbalimbali. Hapo kabla utamaduni huu haukuwepo, tulizoea mabadiliko yasiyo ya kimapambano jambo ambalo limeendelea kukipa chama chetu heshima na afya ya muunganiko kwa muda mrefu.
2. Kwa sasa Siri za Chama huenda zinaanza kuvuja. Kabla ya uteuzi wa Makonda kuwa mwenezi taarifa zilivuja siku mbili kabla na jambo hilo likaja kutokea kweli. Kama hili la katibu mkuu nalo litatokea ni dhahiri hatuko salama sana kwenye chama. Nani anavujisha hizi siri na kwa manufaa ya nani? Kesho zitavuja nyingine nzito zaidi na zitathibitika…. Tunakiua chama. Chama kinachounda Serikali lazima taarifa zake ziwe confidential kwa kuwa taarifa zake ni nyeti na ni taarifa ambazo huathiri hadi utendaji wa Serikali.
3. Zamani CCM ilikuwa si rahisi kupasuka kwa kuwa kulikuwa na chombo kilichoitwa baraza la wazee ambao kimsingi walikuwa wanaaminika na wanachama wote kwa kuwa walikuwa watenda haki na wasiokuwa na makundi ndani ya chama. Kwa sasa chombo hiki hakiaminiki tena na hakina kauli mbele ya vijana machachari waliopo ndani ya CCM. Katika mazingira kama haya Chama konakosa kundi muhimu sana la kutuliza mawimbi yayoweza kukipasua chama.
4.Niliwahi kusema kuwa CCM haipo sayari nyingine. Magonjwa yaliyoviuua vyama vingine ambayo vina rika sawa nacho yanaweza kukiua CCM pia, narudia tena kama hakitajikinga na magonjwa hayo nacho kitaathirika na hatimaye kufa. Vyama vingi vilivyoanzishwa katika miaka ya 1950 na 60 vilishatimuliwa madarakani Siku nyingine sana, mfano United National Independence Party (UNIP) cha Kaunda, Malawi Congress Party (MCP) na Kenya African National Union, (KANU). UNIP ya Kenneth Kaunda ilikuwa ya kwanza kuangushwa mwaka 1991 baada ya miaka 27 madarakani, ikafuatiwa na MCP ya Kamuzu Banda mwaka 1994 (miaka 29 madarakani) na kisha mwaka 2002 ikawa zamu ya KANU (miaka 39 madarakani).Baadhi ya vyama vya ukombozi kama Parmehutu cha Rwanda, Mouvement National Congolais (MNC) cha Kongo- Kinshasa vilishafutwa miaka mingi.
Ukichunguza kwa makini kwa nn vyama hivi vilifurushwa madarakani utagundua ni mipasuko ya ndani. Kwa hili linaloendelea CCM tunaelekea kwenye kukipasua chama kwa makundi kinzani.
5.Historia Rasmi ya Rais Samia kuja kuliongoza taifa hili ilianzia mwaka 2015 pale ambapo aliyeteuliwa kugombea Urais Dr. Magufuli alipomchagua kuwa Mgombea Mwenza. Hata yeye binafsi nadhani alikuwa hajui kama muda mfupi ujao atakuwa Rais watanzania wote pia hawakujua kwamba ipo Siku ndani ya Muda Mfupi ujao Taifa hili litaongozwa na Mwanamke. Katika hili ni Mungu pekee aliyekuwa anajua nini kitatokea toka alipoteuliwa kuwa Mgombea mwenza na huo tunasema ulikuwa mpango wa Mungu ulikuwa wala sio Mpango wa CCM. Hata Rais Magufuli alikuwa ameshaanza kusema hadharani kuwa mgombea atakayekuja atakuwa kijana na mdogo kwake ki Umri na kulikuwa na watu walikuwa wameshaanza kutajwa huku nje ila hakuna aliyemfikiria Rais Samia kuwa ndiye ajaye.
Rais Samia anatakiwa afahamu kuwa anaoketi nao mezani na kushauriana nao ni Moja ya Makada 38 waliotangaza nia 2015 kutaka kuliongoza taifa hili. Rais Samia asifikiri ndoto hizi zao za kuwa kuwa Rais zimekufa, ni dhahiri zipo na huenda kila tukio linalotokea kwenye Siasa na Uchumi lipo calculated kwenye kutaka madaraka ya juu sana ya Nchi hii. Hizi ni hesabu za watu sio rahisi kuziona na hata ukiziona sio rahisi kuzitambua hivyo kila hatua inayopigwa na Rais inatakiwa iwe imehakikiwa vizuri asije kukanyaga Shimo akatumbukia.
Waingereza huwa wana Msemo unaosema “give someone enough rope and he/She will hang himself/herself” kwa tafsiri isiyo Rasmi ni kwamba unapomuona mtu anafanya makosa mpe nafasi ya kutosha kuyafanya ili makosa yake yamwadhibu mwenyewe. Hizi vita zinazopiganwa nje na ndani ya Chama ni scramble ya madaraka ya juu pia ya nchi. Kuna watu wanaona wanachelewa na umri unakimbia hivyo hata mabadiliko yatakayofanywa kwenye chama siku za karibuni yanatakiwa hesabu kali zaidi kuliko huko nyuma. Mwenyekiti na Rais wetu anatakiwa azungukwe na watu ambao ni very loyal na wenye nia ya dhati ya kumsaidia kushinda urais 2025 na si vinginevyo.
6. Duniani kuna majasiri, majasiri hawajawahi kuisha Duniani. Pamoja na ukali wa Magufuli kuna majasiri waliwahi kumuita Mshamba kwenye Simu na akawadukua akawasikia, pamoja na Magufuli kuwa Mkali na utamaduni wa Chama kumtaka yeye mwenyewe achukue fomu ya kugombea urais mwenyewe ndani ya CCM kuna majasiri kama kina Membe walimwambia haiwezekani nao walitaka kuchukua form. Ikabidi afukuzwe uanachama na Form ikachapwa moja na ikatolewa kwa kificho kwa JPM. Tusifikiri majasiri wameisha au hawapo tena Duniani wanaweza kuwashangaza umma muda wowote hivyo maamuzi yoyote ndani ya Chama na mabadiliko yoyote ndani ya Chama yanapaswa kuangalia pia aina ya watu ili majasiri wasipate nafasi za kutoa maamuzi.
7. JPM alifanikiwa sana kutawala na kuongoza kwa pamoja chama na Serikali kwa sababu moja kubwa alikataa kurithi watoto wa awamu ya nne waliokuwa kwenye nafasi za juu serikalini na kwenye chama. Kwenye chama alileta watu wake kina Bashiru na Polepole huku Serikalini akiingiza kina Dr. Mpango, Prof Kabudi, Kina Makonda, Kina mnyeti, Sabaya na wengineo. Watu hawa sio kwamba walimheshimu tu bali walifikia kiwango cha kuanza kuabudu watu wa aina hii ni ngumu kukugeuka au kusaliti.
8. Unazaliwa utamaduni mpya ndani ya Chama kuwa mtu akitaka cheo fulan ndani ya Chama basi watamchafua aliyepo kwenye nafasi hiyo. Kwa utamaduni huu chama hakitakaa kitulie daima. Hili ni la Kuzuia lisitokee kabisa.
9. Kama Mwenyekiti ataridhia kujiuzulu kwa SG Chongolo basi kundi lililohusika kumwondoa madarakani lisitoe mrithi wake. Mrithi wa SG anatakiwa mtu anayetokea nje ya makundi ya Urais, mtu mwaminifu na
10. Kujiuzulu ni ukomavu, kama kweli SG kajiuzulu ni kwa mara ya kwanza kwa nafasi hiyo SG kuondoka kwa kujiuzulu.