Tundu Lissu: Hakuna Rais kwenye nchi hii amewahi kutufanyia kitu mbaya kama Rais Samia

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Wakuu, tupo live leo kutokea Viwanja vya Uhuru, Bukoba kwenye uzinduzi wa Operation 255 Katiba Mpya okoa Bandari Zetu ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiongozana na Tundu Lissu na John Mnyika pamoja na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho watakuwa wanazungumza.

===

Chopa iliyombeba Freeman Mbowe, Tundu Lissu na John Mnyika ikiwasili uwanjani

John Heche
Dola ya Marekani imefika 2550, maana yake maisha yanazidi kupanda. 90% ya ngano tunaagiza nje. Hii inamaanisha maisha yatakuwa magumu.

Wameuza madini yote, dhahabu, tanzanite, nickel n.k. Wamefikia sehemu wameamua kuuza bandari, sote katika nchi yetu bandari ni uchumi, usalama wa nchi, uhuru wetu. Bila aibu wanazunguka nchi nzima kutetea kuuza bandari zetu.

Lazima tujuandae kuchukua hatua kali dhidi ya Serikali hii.

Ezekiel Wenje
CHADEMA tunaamini katika sera ya majimbo, ni aibu bei ya kahawa Uganda ipo juu Uganda kuliko hapa. Nani ana mashaka kati yenu kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi hii?

Matatizo ya nchi hii hayahitaji maombi, yanahitaji akili. CCM wameishiwa, tukiwagusa tu kidogo wanakimbilia kwenye maombi. Nchi inabadilika kwa fikra, sio kwa maombi.

CCM na serikali wamekiri hawana uwezo wa kuongoza mashirika yetu, leo wamekiri hawana uwezo wa kuongoza bandari. Kama wameshindwa hivyo vichache, watawezaje kusimamia nchi nzima?

Tujipange kwa uchaguzi, tuje tuwashughulikie.

Salum Mwalimu
Tunawaomba ndugu zetu watanganyika tusikanyagane. Tunatambua hasira yenu ya kuitaka Tanganyika yenu na sisi tunawaunga mkono.

Siku nyingi wazanzibari tumewambia (wantanganyika) mmelala, mmezubaa, nmapumbazwa, hamsikii. Leo tunashukuru mmefinywa na nyie mmeamka.

Wazanzibari tulikataa kuua zanzibar yetu, ukienda zanzibar leo kuna serikali yake, kuna Rais wake, kuna mawaziri wake, bunge, spika n.k… vya Tanganyika viko wapi?

Tudai katiba mpya, tuwe na serikali 3. Ndio falsafa na sera ya CHADEMA. Sipo tayari muungano uvinjike, lakini nitakuwa wa kwanza kupiga kura ya kuufanyia mabadiliko, kila mmoja abaki na mamlaka yake na heshima yake.

John Mnyika
Kwa yaliyotokea 2019 na 2020, na kwa uongozi mbovu uliopo sasa unaouza bandari na rasilimali zetu tiba ni kuiondoa madarakani serikali iliyopo sasa.

Lakini tuna kikwazo cha sheria na katiba mbovu zinazofanya uchaguzi usiwe huru na haki, ombi langu kwenu tusiache kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Tundu Lissu
Kuna mambo ya ajabu sana yanafanywa nchi hii na watu ambao tulidhani wana akili.

Ni lini katika nchi hii mliona CCM inatembea nchi nzima kuunga mkono mkataba wa kugawa nchi yetu kwa nchi nyingine? Chama kizima? Wote

Wosia wa Mkapa kabla hajaaga dunia alituambia aliiba. Haya kaandika mwenyewe kwenye kitabu chake.

Bandazi zote sio zetu tena, kila kinachoitwa bandari katika nchi hii amekabidhiwa Dubai kwa kipindi kisicho julikana.

CCM kwa kuwa Rais Samia ni mwenyekiti wao lazima wafe naye, ndio maana wanaranda nchi nzima. Hii ya Rais Samia ni kubwa, ni mbaya kuliko mikataba mingine yote. Tusimlaumu Magufuli kwenye hili, hayupo. Nilitaka nisiende, lakini sasa nitaenda Chato kumwamsha Magufuli aje aone ya Samia, ya CCM yake, nitaenda waweke askari Barabarani tu.

Mkataba huu mwanzo hadi mwisho hauonesho faida, sisi tutapata nini na wao watapata nini. Ni mkataba wa milele hadi shughuli za ziwa/bahari zitakapoisha. Mnafikiri huyu Rais aliyesaini Mkataba huu amepewa nini mpaka atuuze nini hii?

Hakuna Rais wa Tanzania ambaye katufanyia kitu mbaya kama huyu (Rais Salia, siyo Magufuli pia na unyama wake wote. Hakuna Rais ametapanya mali zetu namna hii.

Tuchukue hatua ya kuhakikisha havuki 2025 akijiita Rais, tusipofanya hivyo bandari hazitarudi. Pia, Katiba yetu imeyengeneza mungu wa nchi, jukumu la pili ni kutengeneza Katiba ambayo itazuia watu wa aina hii.

Nilimsema Mkapa akanishtaki, alikuwa mkatoliki kama mimi. Akaja Kikwete na mambo yake na wizi wake, alikuwa mwislam, tulimwita mwizi akatushtaki. Akaja Magufuli, mkatoliki na yeye, nilisema pia. Rais Samia amegawa pia bandari zetu kwa waarabu sio kwa kuwa ki mwislam, bali kwa kuwa ni mwizi.

Freeman Mbowe
Sera za CHADEMA zimeundwa kwa maneno 4 ambayo ni Haki, Uhuru, Demokrasia na Maendeleo ya watu wetu.

Wanataka kutugawa sababu ya dini, kwenye Mkataba wa Bandari hakuna udini. Kwenye kusimama kwenye haki hatutarudi nyuma, naomba imani zote zisimame kwenye kweli na haki.

Pia soma: Tundu Lissu: Nitakwenda Chato, nitamwambia Magufuli amka uone Rais Samia anavyofanya
 
Wako vizuri Bukoba

1690549942518.png
 
Wapumbavu wanakinasibisha na udini chama chenye watu wenye akili kubwa!

Na hata hivyo, ukombozi wowote huwa hauji kwa walioshiba na wenye kila kitu, bali huja kwa walio na njaa, walioonewa na kukandamizwa na watawala

Yeyote anayeishi kwenye nchi hii ambaye anahisi kukandamizwa na kuonewa na watu wachache waliohodhi utajiri wa nchi yetu, huku wakitumia turufu ya udini ili waendelee kutunyonya watanzania

Bila kujali dini yako na kabila na hata chama chako,  AMKENI, acha ujinga wa dini, dini ni kushika maagizo ya Mungu, ukweli mwingine ni huu, dini haileti chakula mezani, haijengi barabara, haishushi bei ya chakula, dini inakupa nafasi ya kutenda wema kwa watu na kisha kwenda kwa mwenyezi Mungu pekee,

Adamu alikabidhiwa kazi ya kuitunza aridhi, inapotokea mtu anachezea huu urithi aliotupa Mola wetu, kama wanavyofanya sisiem, tunawaambia hapana,

TANZANIA AMKENI
 
28 Julai 2023
Bukoba, Tanzania

MEYA wa zamani Manispaa ya Bukoba, Chief Kalumuna atikisa CCM

Meya wa zamani Chief Kalumuna leo ametoa ripoti ya hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ilivyo Halmashauri ya mji wa Bukoba.

Kuwa ripoti inaonesha mambo ya maendeleo yamesimama tangu CCM wapore uchaguzi 2020.

Chief Kalumuna anakumbushia mambo makubwa waliyofanya CHADEMA ilipoongoza halmashauri na kuufahamisha msafara wa viongozi kuwa mojawapo ya maendeleo ni taa za kumulika mitaa ya Bukoba ni mazao ya uongozi wa CHADEMA waliposhika hatamu ya kuongoza halmashauri.
 
Wakuu, tupo live leo kutokea Viwanja vya Uhuru, Bukoba kwenye uzinduzi wa Operation 255 Katiba Mpya okoa Bandari Zetu ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiongozana na Tundu Lissu na John Mnyika pamoja na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho watakuwa wanazungumza.

===

View attachment 2701418
Chopa iliyombeba Freeman Mbowe, Tundu Lissu na John Mnyika ikiwasili uwanjani

John Heche
Dola ya Marekani imefika 2550, maana yake maisha yanazidi kupanda. 90% ya ngano tunaagiza nje. Hii inamaanisha maisha yatakuwa magumu.

Wameuza madini yote, dhahabu, tanzanite, nickel n.k. Wamefikia sehemu wameamua kuuza bandari, sote katika nchi yetu bandari ni uchumi, usalama wa nchi, uhuru wetu. Bila aibu wanazunguka nchi nzima kutetea kuuza bandari zetu.

Lazima tujuandae kuchukua hatua kali dhidi ya Serikali hii.

Ezekiel Wenje
CHADEMA tunaamini katika sera ya majimbo, ni aibu bei ya kahawa Uganda ipo juu Uganda kuliko hapa. Nani ana mashaka kati yenu kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi hii?

Matatizo ya nchi hii hayahitaji maombi, yanahitaji akili. CCM wameishiwa, tukiwagusa tu kidogo wanakimbilia kwenye maombi. Nchi inabadilika kwa fikra, sio kwa maombi.

CCM na serikali wamekiri hawana uwezo wa kuongoza mashirika yetu, leo wamekiri hawana uwezo wa kuongoza bandari. Kama wameshindwa hivyo vichache, watawezaje kusimamia nchi nzima?

Tujipange kwa uchaguzi, tuje tuwashughulikie.

Kwa sasa kununua kitu nje ni 25850=$1
 
Hawana jipya.. Kila wakati serikali inasema leteni vifungu vyenye changamoto waangalie namna gani wanaweza kuviboresha kwa pamoja, wao wanakimbia huku na huku.. Wasitumie bandari kama sehemu ya kujibosti kisiasa... Watafute hoja zao za kutoka nazo ila si bandari
Ardhi itawatokea tumboni RUDISHENI
 
Kama tulivyoahidi hapo awali kwamba , tutawaletea kila kinachotendeka kwenye Mkutano huo Mkubwa wa Uzinduzi wa Oparesheni 255, Okoa bandari zetu inayoongozwa na Chadema, tumekuja tena kutimiza Ahadi hiyo.

Huu ni msafara wa Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu ukiingia Viwanja vya Mashujaa.

Screenshot_2023-07-28-17-06-05-1.jpg
Screenshot_2023-07-28-17-06-15-1.jpg
Screenshot_2023-07-28-17-05-57-1.jpg

Awali Wananchi walipanga foleni kwa ajili ya kujisajili kidigitali (CHADEMA DIGITAL)

Screenshot_2023-07-28-16-22-52-1.jpg

Usiondoke JF
 
Wapumbavu wanakinasibisha na udini chama chenye watu wenye akili kubwa!

Na hata hivyo, ukombozi wowote huwa hauji kwa walioshiba na wenye kila kitu, bali huja kwa walio na njaa, walioonewa na kukandamizwa na watawala

Yeyote anayeishi kwenye nchi hii ambaye anahisi kukandamizwa na kuonewa na watu wachache waliohodhi utajiri wa nchi yetu, huku wakitumia turufu ya udini ili waendelee kutunyonya watanzania

Bila kujali dini yako na kabila na hata chama chako,  AMKENI, acha ujinga wa dini, dini ni kushika maagizo ya Mungu, ukweli mwingine ni huu, dini haileti chakula mezani, haijengi barabara, haishushi bei ya chakula, dini inakupa nafasi ya kutenda wema kwa watu na kisha kwenda kwa mwenyezi Mungu pekee,

Adamu alikabidhiwa kazi ya kuitunza aridhi, inapotokea mtu anachezea huu urithi aliotupa Mola wetu, kama wanavyofanya sisiem, tunawaambia hapana,

TANZANIA AMKENI
Wewe ndio wapaswa kuamka, chama chenye Robo tatu ya viongozi wenye Imani ya Dini moja kisha wakana? Wewe si mpumbavu tu? Si ni bora mngefungua kanisa ili mjipatie Waumini au muende msituni
 
Wakuu, tupo live leo kutokea Viwanja vya Uhuru, Bukoba kwenye uzinduzi wa Operation 255 Katiba Mpya okoa Bandari Zetu ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiongozana na Tundu Lissu na John Mnyika pamoja na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho watakuwa wanazungumza.

===

View attachment 2701418
Chopa iliyombeba Freeman Mbowe, Tundu Lissu na John Mnyika ikiwasili uwanjani

John Heche
Dola ya Marekani imefika 2550, maana yake maisha yanazidi kupanda. 90% ya ngano tunaagiza nje. Hii inamaanisha maisha yatakuwa magumu.

Wameuza madini yote, dhahabu, tanzanite, nickel n.k. Wamefikia sehemu wameamua kuuza bandari, sote katika nchi yetu bandari ni uchumi, usalama wa nchi, uhuru wetu. Bila aibu wanazunguka nchi nzima kutetea kuuza bandari zetu.

Lazima tujuandae kuchukua hatua kali dhidi ya Serikali hii.

Ezekiel Wenje
CHADEMA tunaamini katika sera ya majimbo, ni aibu bei ya kahawa Uganda ipo juu Uganda kuliko hapa. Nani ana mashaka kati yenu kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi hii?

Matatizo ya nchi hii hayahitaji maombi, yanahitaji akili. CCM wameishiwa, tukiwagusa tu kidogo wanakimbilia kwenye maombi. Nchi inabadilika kwa fikra, sio kwa maombi.

CCM na serikali wamekiri hawana uwezo wa kuongoza mashirika yetu, leo wamekiri hawana uwezo wa kuongoza bandari. Kama wameshindwa hivyo vichache, watawezaje kusimamia nchi nzima?

Tujipange kwa uchaguzi, tuje tuwashughulikie.
 
Attachments

  • 363463088_173201172436381_4297824750313085565_n.mp4
    6.3 MB
Back
Top Bottom