Waliosambaza taarifa potofu dhidi ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kukiona cha mtema kuni. Waziri Nape atoa maelekezo

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Kupitia mtandao wa kijamii X, Waziri Nape Nnauye amesema kuwa ameelekeza vyombo vinavyohusika kuchukua hatua za mfano dhidi ya wote waliozusha na kusambaza taarifa za uongo dhidi ya Makamu wa Rais.

Nanukuu

"Pole sana Mhe Makamu wa Rais. Tumekusikia. Kwakuwa tuna sheria zinazoelekeza mitandao itumike vizuri na kwakuwa tuna Taasisi na watu wa kusimamia sheria hizi, bila kuathiri uhuru wa watu, TUTACHUKUA HATUA kutokomeza matumizi haya mabaya ya mtandao! Naamini wote watatuelewa.

Nimeelekeza vyombo vyote vinavyohusika kuchukua hatua za mfano, ili tujenge jamii inayoheshimu uhuru wa kila mtu. Uhuru wowote unapoingilia uhuru wa mwingine ni uvunjaji wa sheria, hatuwezi kujenga jamii inayoona hilo ni jambo la kawaida"

Pia soma > Makamu wa Rais Dkt. Mpango akutana na Rais Samia Ikulu ya Chamwino
 
Sasa kwani angetoa taarifa kwamba anasafiri kwenda nje ya nchi hata kupumzika angepungukiwa nini? Saa zingine wanapenda kuwaingiza watu kwenye matatizo ya kukwawazia mabaya kwa makosa yao wenyewe.

Kwani alishindwa nini kumwagiza msaidizi wake pale ofisini kuchapa taarifa kwa umma kwamba anasafari ya kiserikali nje ya nchi na mambo yakatulia.

Ni kusababisha usumbufu tuu usio na faida
 
Acha Nape alete mchezo kisa yupo katika kiti kile, siku zote madaraka huisha, na kuna maisha baada ya vyeo, Taifa tuna mambo bado mengi ya kuangaika nayo, sio vitu vyepesi.

Hivi mtu ambae ni public figure asipooneka for 1 month na hakuna Taarifa , kama binadam umeza jiuliza mangapi?

Ndo hivyo watu wamejiuliza mengi mpaka kufika mbali
 
Nilishasema CCM ni kama manyani tu....kiongozi mkubwa wa umma si kama mtu binafsi eti anaingia mitini tu.....aisee hii ngozi nadhani haitakuja kuendelea....watu wana PhDs wana behavi hivi, watu wasio na elimu wata behave vipi? ....yaani unatakiwa uwe mjinga wa kutupwa usioweza kutafakari jambo lolote ndiyo unaweza kuishi kwa amani nchii hii....mbona tunarudi nyuma sana dah
 
Kupitia mtandao wa kijamii X, Waziri Nape Nnauye amesema kuwa ameelekeza vyombo vinavyohusika kuchukua hatua za mfano dhidi ya wote waliozusha na kusambaza taarifa za uongo dhidi ya Makamu wa Rais

Nanukuu

"Pole sana Mhe Makamu wa Rais. Tumekusikia. Kwakuwa tuna sheria zinazoelekeza mitandao itumike vizuri na kwakuwa tuna Taasisi na watu wa kusimamia sheria hizi, bila kuathiri uhuru wa watu, TUTACHUKUA HATUA kutokomeza matumizi haya mabaya ya mtandao! Naamini wote watatuelewa

Nimeelekeza vyombo vyote vinavyohusika kuchukua hatua za mfano, ili tujenge jamii inayoheshimu uhuru wa kila mtu. Uhuru wowote unapoingilia uhuru wa mwingine ni uvunjaji wa sheria, hatuwezi kujenga jamii inayoona hilo ni jambo la kawaida"
Nape
Mpango ndiyo alimpa JPM kidudu cha Covid-19, asingekuwe yeye JpM angekuwepo.

Sexless anamshukuru sana Mpango
 
Nape wajibika kwanza wewe na wenzio kwa kukaa kimya taifa likipitia taharuki kwa kutokuonekana Makamu wa Rais. Mnatafuta wa kumuwajibisha kabla ya nyie wenyewe kuwajibika. Wajibu wenu ni nini kama mtaona kuna taharuki na kukaa kimya hasa wewe Waziri wa Habari? Kutunza heshima yako iliyobaki,tulia tu na ungana na wananchi kujifunza kwa haya yaliyotokea.
 
Kupitia mtandao wa kijamii X, Waziri Nape Nnauye amesema kuwa ameelekeza vyombo vinavyohusika kuchukua hatua za mfano dhidi ya wote waliozusha na kusambaza taarifa za uongo dhidi ya Makamu wa Rais

Nanukuu

"Pole sana Mhe Makamu wa Rais. Tumekusikia. Kwakuwa tuna sheria zinazoelekeza mitandao itumike vizuri na kwakuwa tuna Taasisi na watu wa kusimamia sheria hizi, bila kuathiri uhuru wa watu, TUTACHUKUA HATUA kutokomeza matumizi haya mabaya ya mtandao! Naamini wote watatuelewa

Nimeelekeza vyombo vyote vinavyohusika kuchukua hatua za mfano, ili tujenge jamii inayoheshimu uhuru wa kila mtu. Uhuru wowote unapoingilia uhuru wa mwingine ni uvunjaji wa sheria, hatuwezi kujenga jamii inayoona hilo ni jambo la kawaida"
Kwa nini serikali ilikaa kimya na kusababisha uvumi? Nape ni kati ya mawaziri mzigo sana
 
Back
Top Bottom