Maxence Melo: Watanzania wana haki ya kutokuamini taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu kuhusu alipokuwa Makamu wa Rais

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
maxresdefault.jpg


Akizungumza East Africa Radio asubuhi hii, Disemba 12, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo amesema Haki za wananchi zinazopatikana nje ya mtandao zinapaswa kutolewa pia ndani ya mtandao kwa kuwa ni haki za msingi zinazogusa maisha ya watu.

Kuhusu kutokutolewa kwa taarifa za alipokuwa Makamu wa Rais Dkt. Mpango, Melo amesema Makamu wa Rais ni kiongozi wa umma, analipwa kwa pesa za umma. Hata kama alienda kwa kazi maalum ni lazima wananchi waambiwe kwa kuwa analipwa kwa kodi zao. Hata kama hawatasema kaenda kufanya kazi gani lakini wananchi wanapaswa kujua kaenda wapi, kwa siku ngapi.

Akitoa maoni yake kuhusu hatua ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye kuwashughulikia waliotoa Taarifa za uzushi kuhusu kifo cha Makamu wa Rais, Melo amesema "Nimesikia Waziri atachukua hatua, ni sawa. Lakini wewe pia ukiguswa sheria hii ichukue mkondo wake, isionekane ipo kwa ajili ya kulinda viongozi pekee. Kuna ushahidi wa matukio mengi yametokea kwa wananchi na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa"

Ameongeza "Sheria ya Makosa ya Mtandao (Kifungu cha 16) inasema anayetoa taarifa za uongo kwa makusudi atashughulikiwa. Kazi ipo kwenye kuprove kama mtu alifanya kwa kusudi, lakini sheria hizi hazitumiki zikivunjwa kwa wananchi wa kawaida lakini zikivunjwa kwa viongozi ndio zinafanya kazi. Kuna "impunity"

Katika hatua nyingine, amebainisha kuwa kwenye matukio muhimu yanayohusisha viongozi wa kitaifa taarifa sahihi zinapaswa kutolewa. Kama kuna uzushi taarifa sahihi zitolewe kuondoa uzushi huo maana kukaa kimya huendeleza kusambaa kwa uzushi.

Melo aliulizwa pia ni kwa nini habari za uzushi kuhusu afya ya Makamu wa Rais ziliendelea kusambaa hata baada ya Waziri Mkuu kutoa taarifa. Alisema watanzania wana haki ya kutokumwamini Waziri Mkuu, yaliwahi kutokea enzi za Uongozi wa Hayati Magufuli, mazingira ya wakati huo na sasa kwa kiasi fulani yalikuwa yanafanana.
 
View attachment 2840103

Akizungumza East Africa Radio asubuhi hii, Disemba 12, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo amesema Haki za wananchi zinazopatikana nje ya mtandao zinapaswa kutolewa pia ndani ya mtandao kwa kuwa ni haki za msingi zinazogusa maisha ya watu.

utokea enzi za Uongozi wa Hayati Magufuli, mazingira ya wakati huo na sasa kwa kiasi fulani yalikuwa yanafanana.
Mpango , kama makamu wa Rais amewadhalilisha WATANZANIA nikiwepo mimi.

Kitendo cha kuongea uhongo mbele ya madhabau ya Bwana hakikubaliki , Naongea kama mkistu alie hai na Mungu wangu najua yu pamoja nami

MPANGO a.k.a Makamu wa Rais wa JMT hatengwe na kanisa, na watz wote period ,
 
View attachment 2840103

Akizungumza East Africa Radio asubuhi hii, Disemba 12, 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo amesema Haki za wananchi zinazopatikana nje ya mtandao zinapaswa kutolewa pia ndani ya mtandao kwa kuwa ni haki
Ni kweli kabisa! Viongozi kabla ya kuapa na hata wakati wa kuapa huwa wanasema ni "watumishi/waajiriwa wetu" na ndivyo hata Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania inavyotaka wawe. Lakini wakishamaliza kuapa tu sisi ndio hugeuka kuwa watumishi wao na hatuna tena njia 'effective' ya kuwaajibisha. Kulikuwa na kifungu kwenye ile Katiba ya Warioba, ambacho kiliondolewa wakati wa kukarabatiwa kwa "Katiba ya Warioba" kwenye Bunge Maalumu la Katiba. Hicho kifungu kiliwapa wananchi mamlaka ya kuwaajibisha wabunge wao.

Ndivyo walivyokuwa wamependekeza kwenye kukusanya maoni Tanzania Bara na Visiwani. Lakini baadaye wanasiasa waliona watakosa kura na wananchi watawabugudhi na kukiondoa hicho kifungu. Ukiwa kiongozi unakuwa bosi, mwananchi aliyekuchagua umsimamie anakuwa mtumishi/mfuasi.
 
Hakunaga kitu kibaya hapa duniani kama Kutoaminika

Watu wanampenda Tundu Antipas Lisu kwa sababu anaamika, hilo tu!
Hakika wewe u mshirika wa Lissu mwaminifu.

Ninajua leo hii Lissu akihamia ccm mtafanya sherehe mwezi mzima.

Huwa Lumumba inatafuta sana sababu ya kumchafua lkn siku zote wamekwama kabisa.

Lissu ni kweli amejiweka mbali na tamaa ya mali.

Lakini m/kiti wetu fununu nyingi sana
 
Back
Top Bottom