Wakulima wa Tanzania hawapo huru kwa sababu ya siasa mbovu za CCM

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,755
Ero sobhai.

Takwenya kokoo wote humu?

Mwangaruka wabhabha na mamayo

Enewei kama salaam haijawachangamsha haya changamkeni na hii.

Serikali ya Tanzania imefunga ndoa isiyo ya kawaida na Chama Cha Mapinduzi ili kukisaidia kisalie madarakani na kuwafanya Watanzania kuwa manamba wa kudumu wa nchi hii.

Uwepo wa Bodi za mazao ambapo badala ya kushughulika na kuboresha ubora na kuweka miongozo chanya ya kulimo nchini, bafala yake Bodi hizo zinasimamia udunishaji wa juhudi za wakulima.kwa kuwakandamiza kupitia upangaji wa bei za mazao wanayolima kwa jasho lao.

Soko la dunia limesheheni wanunuzi ambao wana umoja wao wa kupanga bei za mazao ambapo pia wanakutana na kuvutana na jumuiya za wakulima wanaotaka bei stahiki kwa mazao yao.

Tanzania imeendelea kuwafanya Wakulima wake kama mtaji wa CCM kwa kutumia misuli yake kupanga bei zisizoendana na uhalisia wa soko la.dunia. Serikali inajua kuwa soko la nchi jirani lina bei nzuri na mkombozi kwa mkulima lakini itafunga mipaka ili kuwawezesha madalali wanaotumika na CCM kununua kwa bei ya chini sana (elekezi) tena kwa lazima kutoka kwa wakulima tena wakilindwa na sheria.

Bei ya Korosho mwaka huu imeanguka sana katuka soko la ndani ingawa serikali haikuwahi kupunguza bei za pembejeo za kilimo huku ikihakikisha kila mkulima anawajibika kukopa hizo pembejeo na kuja kukatwa kwenye mauzo ambayo pesa inayokatwa haimuachii unafuu mkulima. Jambo hili lipo kwenye mazao ya biashara karibu yote nchini. Kila zao lina Bodi yake ya udhibiti bafala ya Bodi za kukuza na kuendrleza mazao hayo

Wakulima wa Tanzania walipaswa kuwa matajiri na wangeweza kutikisa uchumi wa Afrika kwa faida ya Nchi yetu. Lakini siasa za kipuuzi na chafu za CCM zitaendelea kudunisha nchi na watu wake huku chama kikiweka nguvu isiyo ya kawaida kwenye kukuza deni la taifa kwa kukopa kutoka nje mikopo ambayo sehemu kubwa inaishia mifukoni mwa viongozi wa kitaifa.

NINI KIFANYIKE
  1. Ikatae CCM na mambo yake yote.
  2. Usipoteze kura yako kwa mgombea yeyote wa CCM kuanzia juu hadi chini
  3. Elimika, yes pata ufahamu wa yanayojiri nje ya mipaka ya nchi yetu hususan maendeleo ya kisekta
  4. Usimsahau Mungu all the time
  5. Elimisha wanao kuhusu uovu wa CCM
CC: Lucas mwashambwa Pascal Mayalla Erythrocyte Sky Eclat sky soldier sifi leo figganigga Mshana Jr Retired Mzee Kigogo raraa reree Depal zitto junior Mdude_Nyagali Gwappo Mwakatobe johnthebaptist GENTAMYCINE dronedrake Demi To yeye na kadhalika
 
As long as ccm iko madarakani basi maendeleo tusahau
Karibia ilani zake zote wanashindwa kuzitekekeza. Alikiri Mzee Mkapa kuwa ilani hazitekelezeki.

Tukikatae chama.hiki hata waje na ahadi nzuri namna gani
 
Umeanza vizuri kuandika ila ulipomalizia na Mambo ya kampeni ya vyama umeharibu kila kitu.

CCM ndio cha kilichojiimarisha kila kona ya nchi.

Kuna vijiji havina kiongozi wa upinzani sasa tutavichaguaje na hali ya kuwa havijajipanga kuchukua nchi ?

Vyama vya Upinzani ndivyo vilivyoua Democrasia ya nchi hii. Kila kiongozi wa Upinzani nia yake ni ama kupata Ruzuku au kuhamia CCM.
Na sio kuimarisha siasa za kidemokrasia.

Kuhusu Mkulima na mazao yake umeongea vizuri sana.
 
Mkuu
Soma.heading vizuri. Nimeitaja CCMkuanzia juu hafi chini.

Siasa za CCM zimewatia watu wengi upofu kutoona uwezo wao nje ya chama hiko.

Ikatar CCM kama.tulivyomkataa mkoloni. Habari za vyama hazihusiki na post yangu. Tanzania haitokaa ikose kiongozi kwa sababu DUTCHMANSHIP MUST ALWAYS HAVE THE CAPTAIN
 
Mkuu Msanii hongera kwa kujiweka pembeni na jinamizi la ccm....najua ulikuwa ccm ndaki-ndaki...huu ni muda wa kuikataa ccm kabisa.....japo wapinzani nao hawako tayari
 
Tumefanywa wajinga sana kwa miaka yote.
Ukuonekana una fikra mbadala wanakupa cheo au kifo

Tanzania inahitaji kukombolewa
 
Ero sobhai.

Takwenya kokoo wote humu?

Mwangaruka wabhabha na mamayo

Enewei kama salaam haijawachangamsha haya changamkeni na hii.

Serikali ya Tanzania imefunga ndoa isiyo ya kawaida na Chama Cha Mapinduzi ili kukisaidia kisalie madarakani na kuwafanya Watanzania kuwa manamba wa kudumu wa nchi hii.

Uwepo wa Bodi za mazao ambapo badala ya kushughulika na kuboresha ubora na kuweka miongozo chanya ya kulimo nchini, bafala yake Bodi hizo zinasimamia udunishaji wa juhudi za wakulima.kwa kuwakandamiza kupitia upangaji wa bei za mazao wanayolima kwa jasho lao.

Soko la dunia limesheheni wanunuzi ambao wana umoja wao wa kupanga bei za mazao ambapo pia wanakutana na kuvutana na jumuiya za wakulima wanaotaka bei stahiki kwa mazao yao.

Tanzania imeendelea kuwafanya Wakulima wake kama mtaji wa CCM kwa kutumia misuli yake kupanga bei zisizoendana na uhalisia wa soko la.dunia. Serikali inajua kuwa soko la nchi jirani lina bei nzuri na mkombozi kwa mkulima lakini itafunga mipaka ili kuwawezesha madalali wanaotumika na CCM kununua kwa bei ya chini sana (elekezi) tena kwa lazima kutoka kwa wakulima tena wakilindwa na sheria.

Bei ya Korosho mwaka huu imeanguka sana katuka soko la ndani ingawa serikali haikuwahi kupunguza bei za pembejeo za kilimo huku ikihakikisha kila mkulima anawajibika kukopa hizo pembejeo na kuja kukatwa kwenye mauzo ambayo pesa inayokatwa haimuachii unafuu mkulima. Jambo hili lipo kwenye mazao ya biashara karibu yote nchini. Kila zao lina Bodi yake ya udhibiti bafala ya Bodi za kukuza na kuendrleza mazao hayo

Wakulima wa Tanzania walipaswa kuwa matajiri na wangeweza kutikisa uchumi wa Afrika kwa faida ya Nchi yetu. Lakini siasa za kipuuzi na chafu za CCM zitaendelea kudunisha nchi na watu wake huku chama kikiweka nguvu isiyo ya kawaida kwenye kukuza deni la taifa kwa kukopa kutoka nje mikopo ambayo sehemu kubwa inaishia mifukoni mwa viongozi wa kitaifa.

NINI KIFANYIKE
  1. Ikatae CCM na mambo yake yote.
  2. Usipoteze kura yako kwa mgombea yeyote wa CCM kuanzia juu hadi chini
  3. Elimika, yes pata ufahamu wa yanayojiri nje ya mipaka ya nchi yetu hususan maendeleo ya kisekta
  4. Usimsahau Mungu all the time
  5. Elimisha wanao kuhusu uovu wa CCM
CC: Lucas mwashambwa Pascal Mayalla Erythrocyte Sky Eclat sky soldier sifi leo figganigga Mshana Jr Retired Mzee Kigogo raraa reree Depal zitto junior Mdude_Nyagali Gwappo Mwakatobe johnthebaptist GENTAMYCINE dronedrake Demi To yeye na kadhalika
1. Ikatae CCM na mambo yake yote.
2. Usipoteze kura yako kwa mgombea yeyote wa CCM kuanzia juu hadi chini
3. Elimika, yes pata ufahamu wa yanayojiri nje ya mipaka ya nchi yetu hususan maendeleo ya kisekta
4. Usimsahau Mungu all the time
5. Elimisha wanao kuhusu uovu wa CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom