Kusaidia Wakulima wa Tanzania, SIDO ihamishiwe OR TAMISEMI, Bila Viwanda vidogo vidogo Mazao yataendelea kuoza shambani na barabarani

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Mkoa wa Njombe kwa sasa Kilimo kikubwa ni maparachichi kwa sababu kuna soko la uhakika. Je baada ya miaka 5 ijayo soko hili litakwepo huko nje?

Njombe na Mbeya ni muhimu kukawa na kiwanda kidogo hata cha kusindika mazao kama Parachichi, Aples, Peazi ambazo leo hii zinauzwa debe moja kati ya elfu tano mpaka kumi na bado matunda haya yanaoza kwenye miti.

Kama kutakuwa na kiwanda kidogo cha kusindika matunda haya itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wakulima, itatoa Ajira na kuongeza pato kwa Taifa.

Mkoa wa Pwani Lindi , Mtwara na maeneo ya jirani, msimu wa Embe ni kama asilimia 60 ya embe zinaozea kwenye miti na barabarani, Wenye miti huuza embe zikiwa mbichi kwa bei ya kutupa. Ni muhimu maeneo haya kikaazishwa kiwanda cha kusindika matunda kitakachosaidia kupunguza au kuondoa kabisa upotevu wa mazao haya, miti ya miembe haina thamani kwa watu wa kanda hii.

Tanga pia Machungwa kwa asilimia nyingi yanapotelea shambani.

Mikoa mingi kuna weza Azishwa viwanda vidogo vya kusindika mazao tofauti, vitasaidia Ajira kwa vijana wengi, vitaweza ongeza pato la Taifa pia.

Miaka ya nyuma vilikwepo viwanda vidogo vidogo kama ZZK MBeya etc.

Viwanda hivi vilitoa ajira, viliongeza ubunifu, viliongeza pato etc.

Ikipendeza SIDO ipelekwe OR TAMISEMI ili RC wakasimamie iazishwaji wa Viwanda hivi vidogo vidogo ili kuweza kusaidia Wakulima wa Tanzania.

Ni muhimu SIDO ikaongezewa bajeti, Watalaam na iwezeshwe zaidi kama ambavyo VETA imeweza kuboreshwa ndani ya miaka mitatu hii, kwa sasa VETA ina Wataalam wa kutosha, Majengo ya kutosha na Mtaji wa kutosha .

Ni muhimu SIDO iwezeshwe ikawe mkombozi kwa kuazisha kusimamia, kuwezesha na kuendesha viwanda vidogo kutokana na upatikanaji wa mazao ya eneo husika

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania
 
Kwani vikiwa chini ya Wizara ya Viwanda RC hawezi kusimamia lakini anaweza kusimamia TARURA, TANROAD, RUWASA, police n.k au yeye ndiyo awe ana shinda site?
 
Kwani vikiwa chini ya Wizara ya Viwanda RC hawezi kusimamia lakini anaweza kusimamia TARURA, TANROAD, RUWASA, police n.k au yeye ndiyo awe ana shinda site?
Anaweza akasimamia mkuu, vyovyote itakavyokuwa SIDO iongezezewe nguvu , nashukuru umekubaliana na kuwa ni muhimu jambo hilo likafanyika hata kama SIDO itabaki ilipo Benjamini Netanyahu
 
Back
Top Bottom