Museveni asema alikataa ombi la kupiga marufuku mchele wa Tanzania. Adai wakulima wavivu walitaka kutawala soko

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,832
Rais wa Uganda leo wakati akitoa hotuba ya miaka 60 ya mapinduzi amesema aliletewa ombi la kupiga marufuku mchele kutoka Tanzania na kukataa ombi hilo.

Museveni amesema wakulima wavivu wa Uganda walitaka kutawala soko. Museveni amesema wakulima wa Uganda wanatakiwa kujua wana ushindani na si kutawala soko ili kupandisha bei.

Pia amesema hatua ya kupiga marufuku inaleta hali ya sintofahamu na kila nchi itaanza kumuwinda mwenzake. Amedai yeye sio kipofu na hawezi kufanya maamuzi ya namna hiyo.
 
Back
Top Bottom