Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,162
- 3,162
Sote tunajua kuwa imani za dini (Ukristo na Uislam) vilikuwepo kabla ya utumwa. Umewahi kujiuliza wakati Waafrica wanauzwa kama Mbuzi kwenye masoko ya Ulaya, Marekani, Uarabuni, viongozi wa dini wa nchi hizo walikuwa wapi kupinga biashara hiyo, tena nchi kama Marekani watumwa wakilimishwa kwenye mashamba kwa uwazi kabisa? Jambo hili huwa najiuliza sipati majibu.
Kwa upande wa Tanzania, rasilimali zote nyeti zinamilikiwa na wawekezaji huku Watanzania wakibaki kama Watwana kwenye Maliasili zao. Madini yanachimbwa huku michanga ikibebwa na kupelekwa tusipojua, kilichomo humo hatujui, ndege kutoka Dubai inatua Loliondo na kuondoka, hivi tuna uhakika kama wanabeba wanyama hai? Vipi ule wimbo wa kwamba Tanzania iwe tayari kuelekea kwenye uchumi wa gesi ya Mtwara na Lindi, tena tunakaambiwa yatasambazwa mabomba ya gesi, kweli huo uchumi wa gesi tunauona?
Watanzania tusikubali kuingia kwenye mitego ya Wanasiasa, achaneni na propaganda za eti tusichanganye siasa na dini, viongozi wa dini zote, Waislam, Wakristo na dini nyingine, kemea mikataba mibovu. Tukiruhusu mikataba mibovu, vizazi vyetu bila kujali dini zetu vitaishia kuwa dereva bodaboda huku watoto wa kizungu wakitafuna urithi wetu.