Ukweli mchungu, kuwa mzalendo wa dhati katika nchi za afrika hasa Tanzania ni kujitakia kifo kabla ya wakati wako

Poa 2

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
1,294
1,288
Jumapili njema

Hata mjinga naye ana mawazo, mtanisamehe Kwa kweli Leo Nina Anika ujinga wangu hadharani. Ukiacha tamaa na uchu wa MADARAKA Kwa viongozi wengi wa afrika, Kuna mambo mengi sana yanayofanya uzalendo kuwa fumbo Kwa viongozi wetu ndani ya nchi Zao. Ukoloni bado upo afrika tena mbaya sana kuliko ule wa kuchapana viboko, tunatawaliwa kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Kujinasua ni mpaka bara lote la Afrika liwe na sauti Moja, kisiasa, kiuchumi na kijeshi hili ni gumu sana, kwani wanaotutawala wako radhi kumwaga damu hili lisitokee na sisi waafrika hatuko tayari kumwaga damu Ili hili litokee. Maana hakuna njia nyingine yoyote zaidi ya ubabe kwamba tutajinasua.

Wako viongozi mbalimbali wa afrika walijaribu kuiunganisha afrika lkn kilichowakuta ni kuundiwa uongo na kuuwawa kikatili huku waafrika wengine wakishangilia( Muamar Gadafi wa Libya) Kiukweli waafrika tumekuwa walinzi TU wa rasilimali za wazungu zilizopo ardhini kwetu ambazo tulishang'anywa na hatuna jinsi.

Mahali/nchi ambapo waafrika wanajitambua kidogo kujaribu kurudisha au kuzuia rasilimali Zao zisiendelee kusombwa zimegeuka jehanamu ndogo, machafuko, vita, ugaidi, na mapinduzi ya kijeshi yaani umwagaji damu haviishi Kila Leo.(Kongo, sudani,afrika ya kati, somalia n.k).

Sasa Hali Iko je Tanzania?

Tuna amani hii ya maigizo Kwa sababu kwanza hatujawahi kuwazuia wazungu wasichukue hizi rasilimali Zao ambazo ni zetu( Madini, gesi, misitu, wanyama, ardhi n.k) Pili ni Kwa sababu chama Cha mapinduzi na vyombo vyake(Dola) kinapambana usiku na mchana kuzuia au kunyong'onyesha nguvu ya ukombozi na uzalendo wa kweli hivyo kurefusha mchakato wa ukombozi na ulinzi kamili wa rasilimali zetu, kazi hii ccm wameifanya vyema Kwa miaka mingi tangu walipokabidhiwa uhuru wa mchongo mwaka 1961.

Tatu amani hii ni Kwa kuwa uoga, ujinga, maradhi na umaskini umetutawala na hatuwezi kujilinda wala kulinda rasilimali zetu na tunafahamu hatuwezi hivyo tumekubali yaishe Bora liende. Nne Kwa kuwa Kuna Mungu aliumba huu ulimwengu hivyo Kwa ulinzi wake wa kipekee tupo na hii amani yenye maumivu laini sana.

Sasa ndugu zanguni Kwa Hali kama hii uzalendo utatokea wapi? Unapewa au kupambania uongozi mkubwa ktk nchi kama Tanzania ukiwa na moyo wote wa uzalendo na uchungu Kwa rasilimali za nchi mwisho unakuja kugundua miongoni mwa Siri kuu ni kwamba rasilimali zote zilizopo nchini mwako ni Mali za wazungu na huwezi kufanya chochote zaidi ya kuwa mlinzi wao tena kupitia ccm Yako huku ukifaidi kidogo ukipenda na usipokwenda na bitiwanakuchomoa utafanyaje ndugu?

Tupo KWENYE makucha ya ukoloni mbaya sana tuwaombee hata Hawa wanaoitwa viongozi wetu .
Na ndio maana ufisadi,wizi na uchu wa MADARAKA afrika na Tanzania hautaisha mile labda atakapoamua Mungu. Ripoti za Ma CAG miaka yote ni wizi na ufisadi mkubwa tusishangae ikiwezekana tuchekelee TU.

Wizi umekuwa ujanja Tanzania viongozi wengi wenye akili wanaona wanachofanya ni kuwaibia wazungu kutoka KWENYE misaada yao ya mchongo au kwenye rasilimali Zao ambazo ziko KWENYE ardhi yetu maana watanzania hawana chochote kilishakombwa kitambo na hata kuwepo KWENYE hizo ardhi ni huruma na fadhila TU za mabeberu yaani watanzania hawana Cha kuibiwa.

Ujinga ni kwamba hawa hawa waafrika wanaofikiri yanawaibia wazungu mwisho wa siku hizo pesa Zao za wizi wanaenda kuzificha huko huko Kwa wazungu na wakifa na pesa zinaishia huko huko Kwa mabeberu
Mliopo MADARAKANI pigeni pesa kiakili na muwekeze hapa hapa na maskini nao tuonje,

Jifunzeni Kwa yule Mzee born town enzi zake na hata Leo Huo ni ujinga wangu wa Leo. Uzalendo hapa bongo ni ndoto wajuba pigeni pesa kiakili raia wa kawaida tusijue maana mnazidi kutuumiza sana
 
Back
Top Bottom