Wazungu wapewe maua yao na si lawama, Utumwa ulikuwepo Dunia nzima, Wao ndio walikuwa wa kwanza kuanzisha harakati za kuufuta

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,119
Tunaanza na hapa kwetu Afrika, utumwa ulikuwepo hata kabla ya waarabu na wazungu kuja, hapo badae soko la watumwa wa kiafrika lilikuwa kubwa na kutufanya sisi kwa sisi waafrika tuanze kuuzana kwa wageni, hivyo nasi tulishiriki kwa kiasi kikubwa sana kwenye utumwa

Warabu walikuwa na watumwa na hapo badae kuanza kununua watumwa huku Afrika, hawa walipinga sana harakati za mzungu kupiga stop utumwa, ilibidi kuwe na jitihada za ziada, mpaka leo nchi za kiarabu kama Libya na Mauritania bado kuna biashara ya utumwa kwa waafrika wanaowakamata wakijaribu kuvuka nchi hizo kwenda ulaya.

India kulikuwa na watumwa ila mpaka leo wana matabaka ya kuamini flani yupo chini ya flani, makampuni ya wahindi hapa kwetu yamekuwa yakilalamikiwa baadhi ya mambo kufanyika kitumwa

Wazungu wao kwa wao walitumikishana, waingereza waliwahi kuwa na makoloni mengi hapa duniani kuanzia india, nchi za kiarabu, china, n.k.

China kulikuwa na watumwa

Israel kulikuwa na watumwa

Walatini walikuwa na wafltumwa, mfano mzuri muvi ya apocalypse

Kwenye vitabu vya dini kulikuwa na watumwa

..................

Lakini licha ya wazungu kupiga stop utumwa bado walikuwa na nafuu kwa mbali, walitupa elimu, waliruhusu watumwa tuweze kujiongoza kwa kiwango flani, waliruhusu kuzaliana leo hii kuna wamarekani babu zao walikuwa watumwa, ikafikia hatua wazungu wao wenyewe wakaona utumwa sio sawa wakaupiga ban.

Na kumbuka mwenye mamlaka makubwa ya kuchukua hatua hii ni yule anaetumikisha sio watumwa wanaotumikishwa,

Si kuharamisha tu utumwa kwa binadamu lakini wazungu wapo mbele zaidi wameweza kutokomeza kwa kiasi kikubwa unyanyasaji wa wanyama.
 
Atleast wazungu wanafanya vitu kwa standards
Ni kwamba waliupinga utumwa, hata kama ni kutumikishana basi kwa ustaarabu,

Leo hii mzungu akitaka kufungua biashara atapiga hesabu kwamba dereva wake walau ampe mshahara laki 4 ili atimize mahitaji yake kwa kiwango flani kinachojali utu.


lakini muhindi, muarabu, muafrika, mchina yupo tayari kuajiri dereva kwa mshahara wa laki 1 bila kujali hata kama anatengeneza faida kubwa.
 
Wacheni huu Ugaidi...


Hii sasa imekuwa kawaida sana hapa JF. Inatia Kinyaa.


Lazima mtu ujiulize, hivi huwa kunakuwa na Nyuzi ngapi hapa Jamiiforums zinazo toa Lawama kwa Wazungu?

Kuna upotoshaji mkubwa sana unaofanyika-Historia inapotoshwa, eti ni Wazungu ndio waliotokomeza biashara ya Utumwa? Kwamba Waafrika walitaka Utumwa uendelee? Kwamba walikuwa hawaoni mateso wanayopata? Mpaka mzungu aje kumwambia 'eti wewe unateseka sana sasa basi' Hii inachekesha na kukera, yaani inapuuza Utu wa Mwafrika 100%

Maxence Melo Hivi jamvi lako siku hizi limefikia hapa? You let these terrorist peddle this revisionist narratives?

Slavery was and is still a global stain, but attributing its demise solely to the white man is a fallacy, Mababu zetu walipinga haya vikali, halafu anakuja mtu na kuwapuuza kabisa na vistori vya vijiweni. Let us not be fooled. Beneath the veneer of reasons lies a dangerous distortion of history.
Nakusii mkuu, kama wanao hawasomi haya, usituachie wanetu wayasome haya.
 
Halafu anakuja kenge wa dini fulani anadai kuwa wazungu ndio walikuwa vinara wa biashara ya utumwa na si waarabu ili hali kuna mikataba kama heligoland na moresby treaty ya kukomesha biashara ya utumwa
 
Hapa Afrika hata kabla ya mzungu kuja kulikuwa na utumwa, Machifu wa kiafrika walianza kuuza watumwa wa kiafrika kwa watu wa nje, hata leo hii mtu akiwa na house girl ana mtrat kama mtumwa kuamka saa 11 alfajiri mpaka usiku ni kazi tu, mshahara elf 40.

Warabu walikuwa na watumwa, pia walipinga sana harakati za kupiga stop utumwa, kwa kiasi kikubwa vita hii ilifanikiwa japo mpaka leo ukienda nchi kama Libya na Mauritania bado kuna utumwa na biashara inaendelea.

India kulikuwa na watumwa ila mpaka leo wana matabaka ya kuamini flani yupo chini ya flani, makampuni ya wahindi hapa kwetu yamekuwa yakilalamikiwa baadhi ya mambo kufanyika kitumwa

Wazungu wao kwa wao walitumikishana, waingereza waliwahi kuwa na makoloni mengi hapa duniani kuanzia india, nchi za kiarabu, china, n.k. licha ya hivi ni wao ndio walioanzisha harakati za kuuharamisha.

China kulikuwa na watumwa

Israel kulikuwa na watumwa

Walatini walikuwa na wafungwa, n.k.

Kwenye vitabu vya dini kulikuwa na watumwa

Kiufupi wafungwa wengi walikuwa mateka wa vita za kikabila, wanaoshindwa wanafanyishwa kazi na kunyayaswa.

Lakini licha ya hivyo wazungu alipokuwa mkoloni sisi tukiwa watumwa, bado alikuwa na nafuu, walitupa elimu, waliruhusu watumwa tuweze kujiongoza kwa kiwango flani, angalau kwa mbali walikuwa na utu tofauti na wengine walikuw wanatoa sehemu za siri uwe kama ngombe wa kulima, n.k. ikafikia hatua wazungu wao wenyewe wakaona utumwa sio sawa wakaupiga ban.

Na kumbuka mwenye mamlaka makubwa ya kuchukua hatua hii ni yule anaetumikisha sio watumwa wanaotumikishwa,
Si kweli.Waarabu ndiyo walikomesha utumwa.Abolition of slavery!Arabs.😎
 
Alieanzisha biashara ya utumwa ndie alieikomesha baada ya kupata faida. Moja ya sababu ya kuzuia biashara ya utumwa ilikua kulinda soko la bidhaa zake na kuuza mitambo. Mapinduzi ya viwanda ni chachu kubwa katika ukomeshaji wa biashara ya utumwa. Ukomeshaji wa biashara ya utumwa ni jambo Pana lakini uthubutu waliouonesha uingereza kweli wapewe maua Yao.
 
Alieanzisha biashara ya utumwa ndie alieikomesha baada ya kupata faida. Moja ya sababu ya kuzuia biashara ya utumwa ilikua kulinda soko la bidhaa zake na kuuza mitambo. Mapinduzi ya viwanda ni chachu kubwa katika ukomeshaji wa biashara ya utumwa. Ukomeshaji wa biashara ya utumwa ni jambo Pana lakini uthubutu waliouonesha uingereza kweli wapewe maua Yao.
Ni kweli ukaziamini hizo sababu za kuambiwa kwenye vitabu vya history?Hukujiongeza?Hawakuwa na utu/sense of humour?Haukuwa ni ushenzi/heathenical business?Haikuwa dhambi/grand sin in terms of religional belief?Haikupitwa na wakati/outdated mitikasi?/ushamba?
 
Back
Top Bottom