Wakati tunaendelea kula kuku tusisahau tulipotoka, wekeza siku ukiwahitaji usije kuwa mzigo

Killing machine

JF-Expert Member
Jul 24, 2022
1,210
1,353
Habari za sasa hivi wakuu??

Kimsingi maisha yetu wengi tunao ishi mjini yame anzia vijijini kama sio kusomea Basi kukulia Kama sio kukulia Basi asiri zetu ni vijijini Miji yote mikubwa duniani ilianza kuwa vijiji ikakuwa ikawa miji hatimaye majiji.

Wakuu zangu mna kumbuka kuhusu funza, chawa, kunguni, siafu, koboko? Ndugu zangu mna ukumbuka ugali wa mtama na mlenda? Na maji ya kunywa yenye langi kama mfiyanzi, ugari maharage ambayo hayaja ungwa, ndizi parachichi bila mboga je, au ugali na parachichi lililo korogwa badara ya mboga?

Vipi kuhusu mkate/bumunda la pale makete, mnaikumbuka chumvi ya mawe, viazi mviringo kuchemshwa na msapuro hapo vipi, vipi kuhusu kitu kinaitwa mchanyato/ mchanganyiko wandizi na maharage?

Tanzania tumejaliwa makabira mengi mno, siwezi kuelezea vyakula vyote vya asiri tulivyo kulia lakini lengo niku kumbushana tu kwamba. Tumeteseka sana, tume kulia kwenye mazingira magumu Sana, tume vaa mavazi ya kutuaibisha, ndala za kushonwa,kutembea peku,kusoma kwa vibatari
n.k.

Sina shaka kama kuna mtu atanibishia kwamba alikuja mjini kutafuta bila shaka kila mtu alikuja mjini kutafuta na lengo kubwa nikujaribu kubadilisha maisha ya vijijini kwetu.

Kwa kuwa saidia mama zetu, baba zetu, wadogo zetu,Bibi zetu, na wengine waliotufanya tumefika hapa tulipo lakini tumefika mjini tume fanikiwa tumejisahau.

Kwamba kuna watu wana lala bila mwanga, kunawatu wanasoma bila mwanga, kuna watu Wana Kula chakula bila mafuta, kuna watu wanakunywa maji machafu, dada zetu Wana olewa wakiwa wadogo, wazazi wetu Wana nyanyaswa na majizi ya aldhi huko vijijini, tumejisahau why?

Tumelogwa na uzuri wa miji na majiji tulimo kuja kutafutia maisha, wana wake wazuri, viti vilefu, fashions, vyeo, madaraka, vinatu sahaulisha sana, tunajiona tumeshinda.

Ila tukumbuke kuna kuvunjwa miguu na bodaboda, magari, bajaji nk na baada ya hapo hatuta weza kufanya kazi marafiki watatu kimbia, watabaki nduguna wazazi tunao wasahau leo.

Tukumbuke pia kuna uzee tujitahidi kuwekeza tuliko toka ili tukija kuzeheka au kuludi Basi tusije kuwa mizigo kwa Kaka au wadogo zetu.

Tukumbuke pia kuna misiba huwa ina tokea rafiki zetu tunao kula nao bata siku wakija tutembelea/misibani nyumbani kwetu wasije tucheka kwani Bata tunazo kula sio masihara wakuu.

Mwisho wakuu zangu tuya jenge makazi yaliyo tulea, tutembelea wazazi walio tulea, pengine kweli hatuwezi kuwapa wanavho vihitaji lakini Basi tuwakumbuke japo kwa mafuta,chumvi, sabuni, na sukari, tuta barikiwa.

Hayo mengine ni majaliwa.
 
Back
Top Bottom