Binti jiepushe na mambo haya usije kuuawa kwenye mapenzi au ndoa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,881
Kwema Wakuu!

Baada ya kushauri Vijana wa Karne hii ya 21+ mambo ya kuzingatia ili wasijekuuwa na kujiweka matatizoni, Leo nitamalizia na Wanawake ili mambo haya yapungue.

Andiko hili nitaliandika Kwa makundi mawili ya watu(wanawake) kundi la Wafuata mifumo ya Kiimani, kundi la pili ni wasiofuata mifumo ya kiimani(Wahuni, wapagani na wendawazimu).

Ukiona nimeandika namna yoyote Ile isiyoendana na mafundisho ya kiimani basi ujue ushauri huo ni Kwa wahuni wasiofuata kanuni na mifumo ya kidini.

Watu wanasema mapenzi hayana Fomula lakini msemo huo upo Kwa Kundi la Wahuni, vichaa, na wendawazimu. Duniani hakuna kisicho na kanuni Kwa wanaoamini katika Dini au mifumo ya kiungu. Hata serikali nyingi Duniani hujua kuwa kila kitu kina Formula na Kanuni.

Mapenzi hayana Formula Kwa kizazi kisicho na maadili, kizazi cha wahuni, wapuuzi wasiotaka kufuata kanuni za Asili.

Ushaambiwa usioe au kuolewa mtu usiyefanana naye unakaza Fuvu oooh! Mapenzi sijui upendo unanguvu na blah!blah za kipuuzi, hakuna kisicho na nguvu Kama ukikipa nafasi nafsini mwako, mapenzi yananguvu Kwa wanaoendekeza Hisia na mihemko.

Siku zote Taikon atabaki na msimamo wa kushauri jamii kuwa Watu waoane wanaofanana Kwa angalau 70%
Masikini Kwa Masikini
Tajiri Kwa Tajiri
Muafrika Kwa Muafrika
Mzungu Kwa Mzungu
Mwerevu Kwa Mwerevu
Mjinga Kwa mjinga
Kichaa Kwa kichaa.

Maumbile yanayofanana, sio unaoa mtu ambaye hamuendani alafu ulete machafuko katika Dunia.
Ndio matokeo yake unaitwa Kibamia, na Mwanamke unaitwa Una Bwawa,

Unaitwa huna nguvu za kiume Kwa sababu mashine uliyoichukua inahitaji walau nguvu na mwendo WA dakika thelasini mpaka arobaini ilhali wewe dakika tano nyingi. Tafuta WA kufanana naye, wapo wanawake au wanaume ambao dakika tatu nyingi amefika mshindo, na wapo ambao bila dakika thelasini haoni ulichofanya.

Bado kuna watu hawanielewi au mnanielewa lakini mnakalia ukaidi,

Wewe sio mtu wa BATA alafu unaoa au kuolewa na mtu wa Bata wewe Kama sio kichaa ni Nani, Ndoa sio sehemu ya kubadilisha tabia na hulka ya mtu, Ndoa ni sehemu ya watu wanaofanana kuonyesha ufanano wao Kwa pamoja Kwa kushirikiana.

Yaani mwanamke sio mlevi au hupendi pombe alafu unaoelewa na Mlevi alafu unalalamika akinywa, au akikojoa Mkono unaonuka pombe chooni au kutapika, wewe ni kichaa WA kiwango cha lami.

Dunia itaendelea kutaabika Kwa sababu watu wanatafuta USAWA Kwa mambo yaliyotofauti, huwezi weka pamoja Mchawi na Mtu wa Mungu ATI waishi Kwa USAWA ndani ya Nyumba.

Binti yangu, nisikilize Kwa umakini, ikiwa nilikuzaa Masikini, na mpaka ukawa na akili ukawa Masikini basi olewa na Mtu unayefanana naye. Kama uchumi wako ni 50 basi olewa na 50 mwenzako au akizidi 60 akipungua 40 ili usimpe shida au asikupe shida mtu huyo.

Kila mwanadamu anaulimwengu wake, hivyo ili mtu awe na Amani lazima atafute mwenza anayefanana na ulimwengu wake. Sio upeleke ufukara wako Kwa Matajiri utahenyeka, na kunyanyasika.

Na sio upeleke Utajiri wako Kwa Masikini utakuja kuua bure, imagine unamhudumia mwanamke yeye na Wazazi wake, wadogo zake, unawajengea majumba na kuwainua alafu jitu lije kukusaliti ati linakuambia maneno ya kipuuzi, walahi huyo mtu wala sisemi hapa chakumfanya Ila kila mtu atafanya Kwa kadiri ya Mazingira yatavyokuwa.

Ninachosema hapa; Usioe fukara Kama wewe ni Tajiri. Kama Una 80% basi oa /olewa na 80% mwenzako au akizidi Sana 90% na akipungua Sana 70%. Huyo huwezi kumuua nakuhakikishia.

Huwezi kumuua mtu mnayefanana, mauaji mengi Duniani yanasababishwa na kutofautiana Kwa watu iwe kimtazamo, kiimani, kimaslahi, kibaraka, n.k. Watu wanaofanana kamwe hawawezi kuuana.

Mkristo Kwa Mkristo mwenye Imani zinazokaribiana mfano; Mkristo mwenye Imani 30% aoe/aolewe na Mkristo mwenye Imani 30% au ikizidi 40% ikipungua 20%.

Halikadhalika na Muislam, Imani zikaribiane, sio kisa ni Muislam mwenzako ndio uoe au kuolewa Naye😀😀😀 wakati Imani zinatofautiana, mwenzio labda Imani yake iko juu labda 80% ya kiislam alafu wewe ni 20% ya uislam, sasa akikuambia uvae Kwa kujistiri unamuona anakutesa, huyo hamfanani.

Binti na Dada zangu, FANYENI hivi,
1. Usiolewe na mtu mnayetofauti Kwa kiasi kikubwa. Hakikisha mnafanana. Hilo nimeelezea hapo juu.
Hata kwenye suala la uzuri. Wewe unajijua huvutii Sana, alafu unachukua mwanaume anayevutia Sana yaani labda uwiano ni 30:80 hapo mtauana tuu😀😀.

Msije leta unafiki hapa kuwa kila binadamu mzuri, ni kweli lakini uzuri unaviwango bhana, wapo wazuri WA kupitiliza mpaka 90% na wapo wazuri wa 10%. Halikadhalika na mambo ya akili, Utajiri, kimo n.k.

2. Usipende vitu vya Bure.
Limwanamke linalopenda vitu vya burebure Lina sifa ya upumbavu.
Yaani kupewapewa hata na watu wasiohusiana nalo.
Unakuta kuomba omba Pesa Kwa watu, mara Fulani ninunulie soda, Jamani Mia tano tuu unakosa, yaani upuuzi upuuzi tuu!
Mwanamke Mwerevu kamwe hawezi omba Pesa Kwa watu hovyo hovyo, ataomba pesa Kwa wazazi kisha ataomba pesa Kwa Mumewe.

Kuomba pesa ni kujidharaulisha alafu badae useme wenye pesa wanadharau, mwenye pesa hawezi kukudharau Kama humuombi pesa hiyo weka akilini mwako. Yeye ndio atajipendekeza na mtu anayejipendekeza kwako ataanzaje kukudharau? Tumia akili hata ya kuku.

Unakuta familia nzima ya mwanamke inaomba hela Kwa mwanaume ninyi si wapuuzi tuu! Alafu siku binti akizingua mnasema ni uamuzi wake, wakati mmekula pesa za watu. Hakika yake Mnatafuta watu ubaya,

Huwa nawaambia mabinti msipende kuwa mizigo Kwa wanaume zenu. Mwanamke fanya kazi hata ya kushona nguo, kuuza biashara ndogo ndogo, Kupika sambusa na Visheti , ujihudumie,

Siku ukiolewa mumeo akuhudumie Ila umsaidie kazi za uzalishaji, sio uwe Zigo la misumari na shetwaani mtaka Mali.

Unakuta limwanamke linafanya kazi, pesa yake ni Yale Ila ya mwanaume ni yawote, utapigwa RISASI pumbavu,
Vijana Kama umeoa mwanamke na Hana msaada wowote kwako kiuchumi Fukuza akakae kwao uone Kama huko kwao wanataka mtu asiyezalisha.
Ila msaidie Kwanza kumpa walau biashara afanye na Mali yoyote itakayopatikana iletwe nyumbani ipigiwe mahesabu.

Mambo ya hela ya mwanamke ni yamwanamke ndio yanaangusha Nyumba nyingi Sana. Na mfumo wa kihuni, na unaotumiwa na watu wahuni ambao hujikuta kwenye umasikini.
Familia kubwa zote Duniani pesa inayozalishwa yoyote inapewa majukumu kulingana na majukumu waliyopeana Baba na Mama.

Usikubali Mwanaume aihudumie familia yako wakati sio wagonjwa huo ni Uhuni, amekuoa wewe sio familia yenu, labda Kwa mambo makubwa Kama magonjwa au majanga Kama Misiba na Ajali.
Unakubali Familia yako ihudumiwe alafu unakataa mumeo asitoke na Dada yako, unaumwa wewe!

Usipende vyabure, waambie wazazi wako wapambane na Hali zao. Wasaidie kidogo ulicho nacho wewe Kwa jasho lako na sio jasho la Mumeo, labda iwe Kwa matatizo makubwa. Hiyo ndio Heshima na Familia yako mumeo ataiheshimu.

Sio kulia shida kila siku za kwenu. Binti yangu sitaki uelezee shida zetu Mimi na Mama yako Kwa Mumeo, hatutaki msaada wowote kutoka kwenu, labda Kwa matatizo makubwa Kama nilivyosema. Dharau wengine hatutaki.

Nimekulea hivyo ulivyo, nimekusomesha hivyo ulivyo ili uweze kuwa msaada Kwa Mumeo sio kuwa zigo la misumari na kumtishwa Mkwe wangu matatizo ya ukoo, nilikufunza hivi ili ujitegemee na sio uwe mzigo.utapigwa RISASI Kwa upumbavu wako na wala sitakusikitikia.
Huwaga sisikitikii wapumbavu na wapenda Kitonga.

Nilikutunza uwe kama Mwanaume lakini sio uwe mwanaume, Mheshimu mumeo lakini usiruhusu akunyime haki zako, usicheke na Mwanaume ikiwa ataleta upumbavu,

Zingatia, kanuni ya mfanano ndio itakayotawala siku zote, ukiivunja unatafuta machafuko na maangamizo.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
 
kama hujawa tayari kuingia kwenye mahusiano/ndoa tafadhali acha kabisaa.
kama umeamua kuingia kwenye mahusiano/ndoa basi ni bora ukaingia kwa miguu yote na utulie na uwe muaminifu daima.

Nitashangaa sana kama makosa yatajirudia yaleyale, njia ya kuepuka ni rahisi, ni kuamua tu.
kila mmoja mwanamke au mwanamume mtizame mwenzio kisha jiulize unamuamini?! mnaaminiani?! hakuna usaliti?! kisha fanya maamuzi sahihi mapema ya kuacha au kukaa mbali.
 
Semina za huko makanisani na misilitini,sijui huwa zinasahaulika...?
 
Aisee kati ya kitu kinachonikera sana ktk mahusiano na wanawake wa kiTanzania ni hili la kuomba omba pesa, yaani sijui hua nayaonaje tu haya mamtu, wapo wanawake wastaarabu ni masikini kabisa lakini kamwe hakuombi pesa mpaka unamsaidia mwenyewe Kwa kujua wajibu wa MWANAUME, lakini yako majitu ukilitazama lina shepu tu ya kuvutia lakini kutwa kucha linakuletea shida za pesa utadhani liliambiwa wewe ndiyo bank kwake, majinga kweli kweli yani
 
Wanawake na kuomba ni nature kama dukani kwa mangi atakaa weee mpaka apewe au akopeshwe kulipa sasa ndo kasheshe atataka atoe.
 
Kama kawaida yako ndugu yangu TAIKON WA FASIHI_hongera kwa bandiko fikirishi na ni ukweli usiopingika kuwa tungeishi kwa kanuni hii ya UFANANO basi mishale mingi INGETUPITIA KWA MBALI KABISA KWENYE MAHUSIANO YETU...Endelea kutufundisha!!!!
 
Back
Top Bottom