Wakati Mungu anaumba alipata wapi nyenzo?

Wakati Mungu anaumba alipata wapi nyenzo?

Kabla binadamu hajaumbwa Mungu alianza kuumba vitu na mazingira .

Kwa upande wa ardhi kama udongo hivi materials aliotumia hadi ukawa udongo sasa alipata wapi na hayo material yaliletwa na nani sasa.
Naona kama umesahau kidogo kwa sababu umejiuliza swali kuhusu Mungu, ambalo si swali mama. Swali mama linatokana na fact hii kwamba, Mungu hana mwanzo wala mwisho. Kwa akili yangu mimi hapa nilipo, angalau naweza kuelewa kiumbe kutokuwa na mwisho, lakini huwa akili yangu huwa inagota pale ninapoambiwa kuwa Mungu hana mwanzo. Si kwamba sikubaliani na ukweli huo, hapana isipokuwa akili yangu haitoshi kuweza kuuelewa ukweli huo, kwa hivyo inabidi niuamini tu. Na hii ni kwa sababu kwenye imani, kuna vitu tunavielewa na kuviamini, na kuna vingine viko juu ya uelewa wetu na hivyo tunaishia kuviamini tu. Uzuri ni kwamba, tusivyovielewa tukishaviamini, tunaona matokeo yake katika ulimwengu wa mwili na wa kiroho sawa na vile tulivyoamini, ila ukiambiwa utoe details za uelewa wako kuhusu vitu hivyo, unashindwa. Vivyo hivyo ukiambiwa utoe details kwamba inawezekanaje kiumbe akawa hana mwanzo, utashindwa vile vile, hili liko juu kiasi kwamba linazidi uelewa wa akili ya mwanadamu

Kwa hiyo ninachotaka kusema hapa ni kwamba issue ya Mungu kutokuwa na mwanzo, ni nzito mara trillion trillion kuliko swali jingine lolote ambalo akili ya mwanadamu inaweza kujiuliza kuhusu Mungu, likiwemo la wapi alipata mali ghafi ya kutumia katika uumbaji wake. Kwa hiyo kwa upane wangu mimi, swala la Mungu kutokuwa na mwanzo linaashiria divine power ya kiwango cha juu sana ambacho hakuna swali jingine mtu anaweza akajiuliza kuhusu Mungu, likavuka hili la Mungu kutokuwa na mwanzo. Ikiwa Mungu hata tu ule mwanzo hana, hii pekee inatosha nisimshangae kumuona anafanya uumbaji pasipo kutumia mali ghafi.

Kumbuka kuwa hapa simaanishi kuwa kuumba kitu bila kutumia mali ghafi si jambo la kushangaza, hapana ni lakushangaza sana isippkuwa simshangai Mungu kufanya hivyo kwa sababu yeye hata ule mwanzo tu hana, jambo ambalo ni la kushangaza sana kuzidi mengine yote!
 
Soma vizuri nimesema kabla hajaumba binadamu .
Nauliza wakati anaumba hivo alivyoumba kama ni udongo hayo material yalikuwa wapi
Hapo ulipofikia ndio ukomo wako wa kuelewa, kwahiyo hapo ndipo unatakiwa ukubali kuwa kuna MUNGU mwenye uweza zaidi. Halafu anza kuamini na kuishi kwa kutenda mema ili upate kufika alipo!
 
Hiyo ni lugha yakibinadamu hili uwelewe maaana mungu hata umbo hana yaani ni complicated kuelewa ili kumuelewesha mwanadamu malanyingi inatumika lugha lagiki kwako kuelewa mkuu mfano utasikia “Mungu alisema” mungu hana mdomo, hana sifa yakuongea so ni lugha ya kutuelewesha tu Boss.

Portfolio | 2020

Hapa si utakuwa umefanya tawlihi? Allah anasikia, anaona, anazungumza ndio maana alizungumza na Mussa katika bonde takatifu la Tuwa, pia Quran ni Maneno ya Allah
 
Yalikuwa wapi wakati huo hayakuwepo
Yalikuwa kwake kama vile ulivyo na sumakuy inashtua moyo wako kupampu damu. Mungu aliijua sumaku kabla ya kuumba wanadamu na akaitumia kushtua mioyo ya viumbe. Moyo wa nyangumi wenye kilo 600 nao unastuliwa na sumaku. Ukipiga hata walio maili 20 watausikia waonaje haya? UDONGO NAO ALIUUMBA HIVO HIVO. MFIKIRIE MUNGU KUWA NI WA AJABU. Usiku na mchana je ulianza vipi?
 
mungu maana yake ni ukuu(nguvu zaidi ya.) hivyo basi hata mimi naweza kuwa mungu kama nitaweza kutumia utashi wangu vile ipasavyo kwani nina uwezo wa kutengezeza chochote ambacho nitakuwa nimekimudu kwa utashi nikao kuwa nao,pia mbali na kuumba kuna imani tegemezi naweza kuchukua watoto wadg wenye umri miezi kama 7 au 6 hivi nikaenda nao kuishi mbalii ambapo ni ngumu binadamu kudhuru huko nikaishi nao kwa huwaaminisha mimi ndio kila kitu kwao yaani mungu wao wale watoto wakakua na wakazaana mimi ikafikia umri fulani nikafa wale bado wataamini tu mimi ni mungu na hakuna mwingine zaidi ya mimi huo ni mfano hai...

sasa tuje kwenye hii dhana kuu ya umungu kiukweli haswa watu wa kiafrica iyo dhana tumeletewa na hatukuwa nayo zaidi ya kusujudia machifu,watemi na mizimu na maisha yalikuwa yakienda sawa kabisa na sheria zilikuwapo kulinga na kila kabila kutumia sheria zao kwa njia za kimila.....


tukirudi mwanzo kabisa kuhusiana na vitendea kazi na malighafi za kazi kuwa je huyo mungu ambavyo kama vile tulivyoaminishwa kuwa ndiye aliyeumba dunia hii tunayoishi hii leo alitoa wapi izo nyezo na hizo matilio za kuumbia dunia??......


kwanza kabisa suprime(mungu) nguvu hii haiko moja ziko nyinginyingi kwann nasema ziko nyingi hii nguvu ya umungu si moja ni ushilikiano wa wajuzi wengi natumia jina la WAJUZI kwa sababu tuweze lupata uelewa pasipo na ukakasi,hawa wajuzi walitengeneza kila tuvionavyo na tusivyoviona kwa manamba mengi ya umri mrefu toka huko zama na wapo wengi na pia wanasehemu yao ya kuishi kila linaloendea wao kama watayarishaji wa uundwaji wetu wanakuwa nao sambamba....


NITAENDELEA....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili lijamaa haliamini uwepo wa Mungu linawazia ubishi tu. Mambo ya rohoni hutafsiriwa kwa maneno ya rohoni so ka lijamaa hili liko mwilini hata ukimwambiaje ataishia kupinga tu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwanini uhitaji tafsiri ya rohoni wakati wewe unaya receive kwenye material and physical sense? What is the balance ?
 
Kabla binadamu hajaumbwa Mungu alianza kuumba vitu na mazingira .

Kwa upande wa ardhi kama udongo hivi materials aliotumia hadi ukawa udongo sasa alipata wapi na hayo material yaliletwa na nani sasa.
Huyo "mungu" unayemuwaza ambaye lazima apate "material" ndio aweze kuumba hayupo!

kabla ya vyote vingine Mungu pekee alikuwepo. Na ni Yeye pekee aliumba vingine vyote!
 
Time is an illusion, there is no past, present or future, everything just is as is and is forever is.

Well Said. Time does not exist.

I hold within my hands Grains of Golden Sand. How few they are, yet how they creep through my fingers to the deep while I weep.

Can I not grasp them?

Surely, all that we see or seem, is but a dream within a dream.

This Poem was written by Edgar Allen explaining the metaphor of life and the way we perceive time. He ended by saying that time is just a dream , an abstraction of the mind, but it never has and never will.

Life is really complex for those who really think and those who want to understand their true essence on earth.

Time( Golden Sand ) creep through our lives , we get old and then we can’t help; we just weep for the chance that we did not take. Sometimes we feel to grasp( the Denial of death ).

The truth is( Hakuna atakayekuja kujibu swali lolote la how this life came to be, ? Na hakuna aliyewahi kujibu. No saint, no prophet, no any être humaine dans univers. Cette question ça va reste mystère comme toujours.

It is just a blah blah God this God that, the Bible said this the Bible said that, Qur an said this Qur an said that — all that we see or seem is just a dream within a dream . Just to make us feel comfortable.

But the truth is always simple and clear that Life is a Mystery and no one knows anything about everything but they think they know .......

Think [emoji848]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom