Wakati Mungu anaumba alipata wapi nyenzo?

Wakati Mungu anaumba alipata wapi nyenzo?

Kwa hiyo Mungu yeye alitoka wapi
Mkuu nimekujibu kuwa WAPI(WHERE) haimhusu MUNGU....

Nikiulizwa WAPI "wa stendi" yupo nitauliza alipo na nitapata majibu yake......

WAPI inahusu viumbe na vitu vilivyopo katika SOLAR SYSTEM....
nje ya "solar system" ndipo MUNGU HUANZIA....na hakuitwi WAPI....akili zetu ,fikra na mawazo yetu hayajakuwa PROGRAMMED kuyajua hayo......

Binadamu ameumbwa na KIASI....
Ndio maana hawezi kula KILO 100...
Hawezi KUWA MREFU Kama mlima KILIMANJARO.....
Hawezi KUPAA angani Kama ndege....japo ndege ni kiumbe dhaifu chini ya binaadamu ....
 
Sunday school na makanisa mengi, yamejianzisha pasipo na mzizi wala jumbe, wengi wamejituma hawa qualify hata kufundisha na pia sunday school hazipewi uzito zinachukuliwa kama sehemu ya kuvuta mda 😀😀😀 wa ibada. Muulize mmoja ya wanao fundisha ujumbe wake ni nini ? Ujumbe wake ndio unaendana na anachojua na kufundisha na kama hana ujumbe hapo utakula chenga tu mkuu
 
Mfano mungu hayupo sisi tulio jiumba au tuliumbwa na nature vip nyenzo tulizitoa wap au mnataka kutumia io point kwa mungu tu wakat popote pale swal lenu Halina majibu
 
Sasa kama alikuwa akitamka tu kwanini siku ya 7 alichoka akapumzika?

Na yeye jinsi alivyo na akili aliumbwa na nani? Haiwezekani awe alitokea tu... Kama alitokea tu bila chanzo basi hata ulimwengu unaweza kutokeza bila muumbaji au akatokea Mungu mwingine mwenye nguvu kumzidi
Mungu hachoki.
 
Mungu hachoki.
Kwanini itumike dhana ya "kupumzika'' baada ya kumalizika shughuli ya uumbaji??

Kwasababu kupumzika kunahusishwa na uchovu.

Kwanini apumzike hali ya kuwa hajachoka??

Au unamaana nyingine ya kupumzika katika muktadha huu (uumbaji)??
 
Kabla binadamu hajaumbwa Mungu alianza kuumba vitu na mazingira .

Kwa upande wa ardhi kama udongo hivi materials aliotumia hadi ukawa udongo sasa alipata wapi na hayo material yaliletwa na nani sasa.
Sitokujibu kinadharia, Nitakujibu kwa jinsi nitakavyoongozwa na Roho Mtakatifu na kama ilivyoandikwa kwenye Biblia Takatifu. Ukisoma Yohana 1: 1 mpaka 4 inaeleza kwamba Mungu ni Neno na vyote vilifanyika kupitia yeye. Kwa kunena kwake vitu vyote vilifanyika. Mungu alinena na vitu vikatokea. Mwanzo 1:1 inasema "Hapo Mwanzo Mungu aliumba Mbingu na Nchi" kama Mungu ni Neno hivyo basi aliumba Mbingu na Nchi kwa kutamka. Hii inathibitishwa na Mwanzo 1:2 "Mungu akasema iwe Nuru, ikawa Nuru" kama nitakuwa nakujibu sawasawa ni hivi Material aliyotumia Mungu kuumba udongo ni Neno lake. Umeuliza tena Materiala hayo yakitoka wapi? Nakujibu: Materials hayo yalitoka Kinywani mwake.
 
Mfano mungu hayupo sisi tulio jiumba au tuliumbwa na nature vip nyenzo tulizitoa wap au mnataka kutumia io point kwa mungu tu wakat popote pale swal lenu Halina majibu
Hii ni Tu quoque fallacy. Kimsingi unachosema hapa ni kuwa hata nyinyi hamjui jibu hivyo mungu ni shortcut tuliyojitengenezea ili kujipa matumaini ya kujua.
 
Nitofautiane na wengine...

MUNGU haku-"create" japo versions za biblia zinasema aliumba (create)...

Kumbuka kila kinachokua Created huwa kina sifa ya kufa..kila klichoumbwa kinakufa.

bali

MUNGU ali-"organize" kwa maana ya kwamba kulikua na materials tayari (elements) ambazo alitumia kwenye kazi zake.

Na Elements are eternal.
 
Nitofautiane na wengine...

MUNGU haku-"create" japo versions za biblia zinasema aliumba (create)...

Kumbuka kila kinachokua Created huwa kina sifa ya kufa..kila klichoumbwa kinakufa.

bali

MUNGU ali-"organize" kwa maana ya kwamba kulikua na materials tayari (elements) ambazo alitumia kwenye kazi zake.

Na Elements are eternal.
Sasa hii wewe umeitoa wapi kama kwenye biblia haipo?.
 
Toeni jibu kamili nakama huna jibu kaa kimia. Maana inaonekana unashabikia tu hata mwenyewe hujui. Ukweli ni kwamba hata dini au Vitabu vyote Vya dini hajui Mungu alitoka wapi na hakuna anaejua .
 
Kupumzika inamaanisha aliendelea na kazi baada ya kupumzika hainamaana alimaliza kazi Yake.
 
Aseeee ila binadamu ni wabishi sana baada ya kusoma origin of the universe kwnye vi bing bang theory,Encounter theory,nebula theory bas tunajiona kama tunaweza kujudge uumbaji wa Muumba wetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom