Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 2,494
- 6,450
Bila shaka mko vizuri wanajukwaa... Leo wacha niwape maneno ya yule mzee ili mnisaidie kuyatafakari.
Huyu mzee alianza kwa kuniambia kwamba kimsingi ndani ya kila mtu kuna mbawa za kuruka juu ya upeo wa mafanikio, lakini si kila biashara ni upepo unaoweza kumuinua kila arukaye.
Hii ni sentensi ambayo ilipenya kwenye ubongo wangu na ikanifanya nitulie kwa dakika au sekunde kadhaa kwa lengo la kuuacha ubongo wangu uichakate kwa kina ili niweze kuelewa maana yake ilikua ni nini hasa.
Na baada ya hizo sekunde kupita nilijikuta tu ghafla nauliza “kwanini”? Yule Mzee aliniangalia kisha akatabasamu na kuniachia swali, vipi wewe ni muamini au si muamini?
Nami nikajibu kwa haraka, “ni muamini”.
Nae akaendelea kusema, kama ni muamini basi bila shaka unaelewa kwamba sisi ni udongo, yaani na maanisha kwamba mwanadamu aliumbwa kwa udongo lakini wakati huo huo sisi wahenga husema pesa ni maua.
Kwahiyo kwa lugha nyingine ni kwamba pesa ni matokeo ya mbegu fulani iliyoota na kumea baada ya kupandwa kwenye udongo wa ardhi fulani.
Na kikawaida ni kwamba Kila udongo ulio juu ya ardhi fulani unao uwezo wa kuotesha mbegu itakayo pandwa ndani yake ila si Kila mbegu inayopandwa kwenye Kila udongo inayouwezo wa kumea na kuchanusha maua yenye kuleta matunda yenye afya inayotakiwa.
Hii yote ni kwasababu udongo wa ardhi moja huwa unatofautiana na udongo wa kwenye ardhi nyingine.
Ndio maana ukiangalia kwenye nchi yetu Kila ukanda huwa wanayo mazao yao yanayostawi kwenye udongo wa ardhi ya ukanda huo pekee na ukisema mazao hayo uyapeleke kwenye ardhi ya ukanda mwingine yataota ila yanaweza yasimee kwa namna ile ambayo inatakiwa.
Kwahiyo biashara ni mbegu na wewe ni udongo, sasa ili ujue ni aina gani ya mbegu inayoweza kumea vizuri kwenye huo udongo wa ardhi yako ni lazima ujue kwanza aina ya udongo ambao uko kwenye hiyo ardhi yako.
Sasa huu ni mtihani ambao watu wengi unawashinda na ndio maana unaona maua hayachanui kwenye udongo wa kila ardhi, kwasababu watu hupanda mbegu ambazo haziendani na udongo uliopo kwenye ardhi zao.
Na ukitaka uamini kwenye hili chukua muda wako wote na ufanye uchunguzi wa haraka haraka na utagundua kwamba biashara ambayo imempa utajiri rafiki yako na wewe ukienda kujaribu unaweza ukaangukia pua na kujikuta unaingia kwenye madeni yasiyo na msingi, na hii yote ni kwasababu udongo wa ardhi yako hauwezi kuifanya mbegu hiyo uliyoipanda iote, imee na kukupatia maua yenye kuleta matunda bora kama ambavyo imefanya kwa rafikiyo.
Hapo hapo nami ikabidi nimuulize swali huyu mzee, itakuaje kama nitaamua kubadili asili ya udongo huo ili iweze kuendana na udongo ambao nnauhakika mbegu fulani zikipandwa huwa zinamea kwa kiwango kizuri sana?
Nikaona huyu mzee ananyanyuka baada ya hilo swali langu, akaniangalia kisha akasikitika kidogo na akaniambia hapo lazima uwe tayari kuingia gharama zisizo na umoko kwenye Kila msimu mpya unapoingia kabla ya kupanda mbegu utatakiwa uhakikishe umeandaa shamba na kuufanya udongo wako uwe kama udongo wa ardhi ile yenye kuotesha mbegu hiyo isiyo fungamana na udongo wa ardhi yako.
Lakini nakuhakilishia kwakufanya hivi huwezi kupata matokeo yanayotakiwa hasa kigezo cha utofauti wa misimu utakapoingilia kati.
Kisha akaendelea kusema…
Niskilize kijana, ardhi inahitaji matunzo na matunzo Bora ya kila ardhi kwanza ni kuhakikisha unaiacha ifanye kazi katika namna yake ya asili.
Sasa unapoanza kuiongezea vitu ili uibadili ile hali yake ya asili na kuipeleka kwenye hali nyingine mwanzo itakupatia matokeo ila kadri siku zinavyoenda itakushinda kuimaintain kwa maana utahitajika kutumia gharama kubwa ili kuifanya rutuba iendelee kuwepo kwenye udongo wa ardhi yako na kuzuia ile tabia ya mabadiliko yake ya asili yasijitokeze kwa lengo la kulinda zao la asili tofauti ulilolioanda na kumea juu yake.
Na mwishowe itakushinda kwa maana hasara itakua kubwa kuliko faida na punde tu utakapoacha kufuata utaratibu huo mpya uliouanzisha kwenye hiyo ardhi basi utabaki na ardhi yenye udongo usioeleweka asili yake ni ipi na hapa ndio watu husema rutuba hamna na kwa maana hiyo basi hakutokua na mbegu ya aina yoyote itakayoota na kumea kwenye udongo wa ardhi hiyo na hii haitaishia kwa zile mbegu ambazo hazifungamani na ardhi yako kiasili bali hata zile ambazo zinafungamana nayo zitagoma kumea.
Kisha akaangalia saa yake, hapo hapo akaniaga na kupotelea gizani (halikua giza la kukosekana kwa mwaga bali lilikua ni giza la ukungu uliopelekea mawingu yatande hadi ardhini).