Wakataa KUOA wengi ni wale ambao tuliumizwa na wapenzi tuliowapa hisia na tumaini la kudumu katika kweli. Hii imekuwa chachu ya fikra hasi kuhusu KUOA

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,411
11,061
Hello family,

Mods please tupeni fursa tuseme kweli, kweli inaponya.

Let speak the truth, the truth be told. Hakika nasema katika kweli hasira na chuki hasa katika mawanda ya ndoa si bure kuna chanzo, wengi wa wanaokataa ndoa na kuoa ni wahanga wa kuumizwa kihisia na kuharibiwa malengo hasa dhamira ya dhati ya kuwa na wenza wao au wapenzi wao katika kusudi la kudumu. Hivyo basi kuishia kupoteza tumaini na Imani ya kweli katika kupata mtu wa kweli na aliye sahihi kuishi nae kwa lengo la kudumu kama mke na mume.

Baadhi yetu tuliachwa na kusemwa vibaya kwa kejeli, matusi, dharau, wengine katika kadamnasi, heshima ilikufa kabisa.

Katika Hali ya kukosa tiba ya vidonda hivyo mbalimbali kwa vyanzo na matukio mbalimbali tumejikuta ni watu katili sana sana kihisia hatuogopi kuwa peke yetu, hatujali chochote kitu, na hasa pale unapokuwa na fimbo ya pesa ya kufanya chochote ni balaa.

Nawahusia vijana, mabinti, wanawake kwa wanaume weka akiba kwa kila jambo, timiza wqjibu mfahamu mpenzi wako kwa historia kila alipopita muulize ongea nae. Ipo siku atabadirika je wewe utakuwaje umejiandaa vipi kupokea kuachwa au kuachika.

Mapenzi ni amani, mapenzi ni chuki, mapenzi ni furaha, mapenzi ni hudhuni, kuna hisia, kuona na kusikia vyote vyetu.

Niwakaribishe kwenye ushuhuda na simulizi.

karibuni

wadiz a.k.a Baharia
 
Nataman Dunia ingerudi nyuma miaka 6. Ningeweza kubadilisha mwanzo...ndio bàsi tena majuto ni mjukuu ndio nishakua single mothers of two kids from two father's 😭
Yote ni maisha tena ukijikubali ni raha sana, muhimu uishi kwa misingi mizuri
 
tuliosoma uganda
FB_IMG_1685871933076.jpg
 
Nataman Dunia ingerudi nyuma miaka 6. Ningeweza kubadilisha mwanzo...ndio bàsi tena majuto ni mjukuu ndio nishakua single mothers of two kids from two father's 😭
Haijaisha Mpaka Ifike Mwisho, Zaeni Ndugu Zangu Taifa Linataka Nguvu Kazi
Hata Ukiweza Watoto Wakiwa 6 Na Baba Zao 6
Tazama Angel Bernard Anaolewa Anazaa Anaachika Anaolewa Tena Hachoki Kazi Moja
 
Katika Hali ya kukosa tiba ya vidonda hivyo mbalimbali kwa vyanzo na matukio mbalimbali tumejikuta ni watu katili sana sana kihisia hatuogopi kuwa peke yetu, hatujali chochote kitu, na hasa pale unapokuwa na fimbo ya pesa ya kufanya chochote ni balaa.
Sababu ya hovyo sana sana hii! Kijana oa, usipooa utaolewa! Unatakiwa shupavu, real men lazima uwe na ndoa, umiliki mwanamke na Watoto
 
Haijaisha Mpaka Ifike Mwisho, Zaeni Ndugu Zangu Taifa Linataka Nguvu Kazi
Hata Ukiweza Watoto Wakiwa 6 Na Baba Zao 6
Tazama Angel Bernard Anaolewa Anazaa Anaachika Anaolewa Tena Hachoki Kazi Moja
Hahahaha huu mfano wako sasa
 
Huenda kosa ambalo mie binafsi naona kama kuoa, kila nikijitazama naona sikufaa kuoa yani 😅😅. Kipengele unaanzisha vipi hoja ya kuachana na mtu .. kwanza familia zote zinapatana, ndoa ina amani.. Naumiza kichwa kishenzi hapa nachomokaje kwenye hili gereza aisee
Kwamba ndoa yako haina shida lakini hauitaki tu? Huku kwetu huwezi kueleweka, kwa weupe huko ndio ungeweza kueleweka na hiyo sababu yako ingesimama kama sababu toshelevu. Kwamba hakuna tatizo, sitaki tu ndoa na naona sikuwa designed kwa ajili hiyo, i made a mistake na blah blah zingine.

Kuna wengine wanajisikia hivyo, na wanaona wafanye vitimbi ili wapate sababu ya kuacha au kuachwa. 😅 Africa kugumu sana sijui kama tunaweza kuishi bila unafiki.

Swali kwako, Ukitoka humo una uhakika kuwa hautaitaka tena? Tabia ya mwanadamu ni kuchoka/kukinai na kukihitaji kitu tena baada ya muda.
 
Back
Top Bottom