Wahenga tujuane hapa..

Wahenga tujuane hapa..

SALOK

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2011
Posts
3,629
Reaction score
2,308
UNAKUMBUKA HILI SHAIRI...??
Weka ubeti unaoukumbuka...

Ninaye ndege mzuri, mrembo wa kupendeza,
Rangi zake mashuhuri, ni nne nawaeleza,
Ndizo rangi za fahari, urembo kuutimiza,
Ndege huyu ndege gani, hapa kwetu Tanzania?

Anayo rangi nyeusi, sote tunaitukuza, Nami nilipodadisi, Kumbe nimemwambukiza,
Nayo ni rangi halisi, ambayo imenikuza,

Rangi ya pili kijani, kwenye mbawa katimiza,
Nzuri isiyo kifani, kwenye mwanga hung’ariza,
Jamani niambieni, ndege amenipendeza,

Ya tatu ni ya ajabu, sambamba imejilaza,
Ni rangi ya kidhahabu, kwa haiba hushangaza,
Hima nipeni jawabu, jina linanitatiza,

Rangi ya nne bluu, mkiani kaeneza,
Rangi ya bahari kuu, na maziwa yalojaza,
Ndege arukapo juu, rangi hii hutokeza,

Aisee! Kiswahili Drs la sita mwaka 1995
 
Back
Top Bottom