KALA JEREMIAH - WIZI MTUPU

KALA JEREMIAH - WIZI MTUPU

Joined
Nov 8, 2018
Posts
29
Reaction score
31
## 🎧 INTRO / UTANGULIZI
Marc, uliza wizi!
Hi..!!
0444 ...


## 🎤 VERSE 1
Wanasayansi walidai nilitokana na nyani, /
Biblia yangu inasema aliniumba manani /
Ndio maana naziona skendo mnazofanya gizani /
Dala dala zinakusanywa zinashusha Sinza makaburini /
Mchana dini, usiku ndani kimini /
Waumini yasafisheni mapito, Bwana yu waja /
Sikieni wito wa Kala na nguvu ya hoja /
Moja na moja sio moja /
Sifundishi uzembe, nafichua maovu kama tume ya Mwakyembe /
Sina upande, simtupi mkulima kama jembe /
Sauti yangu inawapa hope wachungaji wa ng'ombe /
Naliwaza masikini waishio ndani ya matembe /
Nawapa uono vipofu wa class ya pombe /
Bado..!! /
Na Udiscuss ugumu wa kesi Zombe /
Bado..!! /
Nashusha lecture kama chuo cha Mzumbe /
Jela masikini alale, tajiri asilale! Kwani? /
Mimi ni mdogo ila siwahofii magangwe /
Hata nikifa nife kiharakati kama Wangwe ..


## 🔄 CHORUS / KIITIKIO (×2)
Ona mnyonge nalia chozi la Damu /
Wizi mtupu..!! /
Ona kigongo na biashara Haramu /
Wizi mtupu..!! /
Ona kitambi kwa jambazi wa kalamu /
Ona ona ona ona ona /
Wizi mtupu..! /
Ona mnyonge nalia chozi la Damu /
Wizi mtupu..!! /
Ona kigongo na biashara Haramu /
Wizi mtupu..!! /
Ona kitambi kwa jambazi wa kalamu /
Ona ona ona ona ona /
Wizi mtupu


## 🎤 VERSE 2
Samaki wangu wa Mwanza vipi wanageuzwa silaha /
Nasimama na hoja kweli kama Doctor Slaa /
Mugabe ndo babu yangu aliyebaki hii Afrika /
Anayetetea mnyonge Zimbabwe najivunia /
Simfagilii mzuru anayemtesa Mtanzania /
Alozamia nchini kwake kujitafutia rupia /
My dear nipe stick ili niongeze idea /
Hisia zangu zinachoma mioyo ya Watanzania /
Nguvu, sababu na uwezo mimi ninao wa kuwafuta machozi waliovunjika mioyo /
Walioteswa na mapenzi, shida za dunia /
Matatizo mengi mengi, yatima nalia /
Wajane na ombaomba sichoki kusaidia /
Mama Kayanga klachi, nazidiwa na uzito wa gear /
Ama niache muziki nikaisome sheria /
Milipuko mikubwa ya bomu nani hatayakwepa /
Wangapi wamekula "B.O.T" na mchuzi wa "EPA" /
Wangapi tunakula mihogo na mchuzi wa papa /
Masikini kama mimi niishie malapa /
Chumba changu hakina umeme /
Na kodi bado nailipa, wanaiba kisha ......




## 🔄 CHORUS / KIITIKIO (×2)
Ona mnyonge nalia chozi la Damu /
Wizi mtupu..!! /
Ona kigongo na biashara Haramu /
Wizi mtupu..!! /
Ona kitambi kwa jambazi wa kalamu /
Ona ona ona ona ona /
Wizi mtupu..! /
Ona mnyonge nalia chozi la Damu /
Wizi mtupu..!! /
Ona kigongo na biashara Haramu /
Wizi mtupu..!! /
Ona kitambi kwa jambazi wa kalamu /
Ona ona ona ona ona /
Wizi mtupu..!



## 🎤 VERSE 3
Ma Albino wanasakwa kwa mapanga, wanachinjwa damu zao zipelekwa kwa mganga /
Mungu okoa ualbino, wanyoshee mkono hii dhambi, nahisi hata shetani haingui mkono /
Nasubiri jua kuzama, kesho wawite mkomo /
Kesho kesi, leo jaji tayari kafungwa mdomo /
Haya..!!!! /
Wana hisa kwa shetani, wanasingizia visimo /
Wamo kati yao hata ambao wana msimamo /
Waliokosa rangi ya kijivu, wakachanganya blue na njano /
Kwa kosa moja kwenye tatu, nne kwenye tano /
Ukapata tisa kwenye sita, mguu kwenye mkono /
Wakachanganya mguu na kichwa, mtaani wakaunda msemo /
Wamelala zaidi ya Porno /
Bandarini vitu feki vinafahirishwa mchana /
Cause ya mtu ni dili na bado watu wanaichuna /
Kwani nani atasema wenye midomo wamefungwa /
Midomo ina nguvu ya noti /
Wanaharakati wameshona na nyuzi ya koti /
TAKUKURU, maututu na uzito wa suti /
Du.!! /
Mtanzania, komaa na uzito wa hiyo bajeti /
Mungu wako yuko juu, usiloliweza yeye ataseti ....


## 🔄 CHORUS / KIITIKIO (×2)
Ona mnyonge nalia chozi la Damu /
Wizi mtupu..!! /
Ona kigongo na biashara Haramu /
Wizi mtupu..!! /
Ona kitambi kwa jambazi wa kalamu /
Ona ona ona ona ona /
Wizi mtupu..! /
Ona mnyonge nalia chozi la Damu /
Wizi mtupu..!! /
Ona kigongo na biashara Haramu /
Wizi mtupu..!! /
Ona kitambi kwa jambazi wa kalamu /
Ona ona ona ona ona /
Wizi mtupu..!


------------------------------
## 🧐 KIINI CHA HISTORIA: Viongozi na Matukio Yaliyotajwa
Wimbo huu uliotoka mwaka 2008 ni maktaba hai ya kisiasa. Hapa kuna dondoo za viongozi na matukio yaliyolengwa:


1. Dkt. Harrison Mwakyembe (Tume ya Richmond - 2008): Kala anafananisha rap yake na Kamati Teule ya Bunge iliyofichua ubadhirifu wa mkataba wa Richmond na kupelekea kuanguka kwa serikali (Waziri Mkuu kujiuzulu).

2. ACP Abdallah Zombe (Kesi ya Zombe - 2006): Inahusu sakata la mauaji ya kinyama ya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva teksi wao yaliyofanywa na kikosi cha polisi Sinza/Pande, na jinsi mfumo wa sheria ulivyogubikwa na utata.

3. Chacha Zakayo Wangwe (Kifo cha Mwanaharakati - 2008): Mbunge machachari wa Tarime (CHADEMA) aliyepoteza maisha kwa ajali ya gari yenye utata mkubwa Julai 2008. Kala anautumia kama mfano wa kufa akipigania haki.

4. Dkt. Wilbroad Slaa (Orodha ya Mafisadi - 2007): Mbunge aliyetikisa nchi kwa kusimama na nyaraka thabiti viwanja vya Mwembeyanga na kutaja majina ya viongozi waliotuhumiwa kula fedha za umma.

5. Kashfa ya EPA na BoT (2005 - 2006): Wizi mkubwa wa mabilioni ya fedha za wavuja jasho kupitia akaunti ya madeni ya nje (External Payment Arrears) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania.

6. Mauaji ya Watu Wenye Ualbino (2007 - 2009): Wimbi la kinyama la kukatwa viungo na kusakwa kwa maalbino nchini kwa ajili ya imani za kishirikina za kupata utajiri kwa waganga.

7. Robert Mugabe (Mapinduzi ya Ardhi - Miaka ya 2000): Rais wa zamani wa Zimbabwe anayetajwa kama mfano wa kiongozi aliyetetea wanyonge kwa kutaifisha ardhi ya wakoloni na kuirudisha kwa wazawa.

8. TAKUKURU na Wanaharakati: Kala anazisuta taasisi za kupambana na rushwa na watetezi wa haki kwa kulala, kuendekeza muonekano wa suti za gharama, na kunyamazishwa kwa nguvu ya noti...

Je, unaukumbuka mstari gani unaokugusa zaidi kwenye wimbo huu? Tuachie maoni yako hapa chini!


## 📻 KALA JEREMIAH – WIZI MTUPU (2008) 🇹🇿
Leo nimeamua kuweka kumbukumbu sawa ya moja kati ya nyimbo bora zaidi za Hip Hop ya harakati na mapinduzi ya fikra kuwahi kutokea nchini Tanzania. Huu ni wimbo wa "Wizi Mtupu" wa Kala Jeremiah.


Uchambuzi wa nyimbo za Kala Jeremiah unagusa matukio mbalimbali ya kihistoria, kisiasa, na kijamii nchini Tanzania.

Katika verse zote tatu, msanii huyu anakemea ubadhirifu, ufisadi, na ukatili wa kijamii huku akitaja viongozi na skendo kama vile Tume ya Mwakyembe (2008), kesi ya Zombe (2006), kifo cha Chacha Wangwe (2008), kashfa ya EPA, na mauaji ya watu wenye ualbino....
 

Attachments

  • Wizi_Mtupu_-_Kaya_Jermiah(360p).mp4
    10.9 MB
Back
Top Bottom