FIKRA NASAHA
Member
- May 22, 2023
- 15
- 50
WANAOREJESHWANCHINI - TANZANIA
JE, SERIKALI IMEJIANDAA KWA MAISHA YAO BAADA YA REPATRIATION?
Kwanini kurejeshwa kwa Watanzania kutoka Afrika Kusini kusibaki tu kuwa safari ya kurudi nyumbani, bali iwe mwanzo wa mpango wa ajira, biashara na Reintegration.
Habari rasmi zina onyesha Serikali ya Tanzania imepanga kuwarudisha kwa hiari takriban raia 669 kutoka Afrika Kusini kutokana na hali ya chuki (xenophobia) dhidi ya wageni. Kundi la kwanza la vijana (karibu 173 kutoka KwaZulu-Natal/Durban) walirudishwa mwishoni mwa Agosti 2026 kwa ndege maalum, na mipango iliyopo ni kuwarudisha wengine kutoka miji ya Cape Town (karibu 300) na Johannesburg kufikia jumla ya raia 669.
Wengi wao walikuwa wameishi huko kwa muda mrefu, baadhi wakiwa na ujuzi, elimu au biashara ndogondogo. Kurudi kwao si jambo rahisi wameacha shughuli zao za kijamii, wateja, na maisha waliyo yajenga na sasa yamekatishwa ghafla.
Kwenye mitandao ya kijamii, kulionyeshwa video ya vijana wakiwa kwenye ndege wakirejea nyumbani, Tanzania. Kama ilivyo ada ya Watanzania haswa kwenye mitandao ya kijamii, gumzo likawa kubwa, wengi wakaonyesha wasiwasi wao kuwa hao vijana wanaweza kuongeza wimbi la uharifu, mitaani.
Wasiwasi wao una msingi mkubwa na unagusa eneo nyeti la usalama na maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kurudi kwa idadi kubwa ya vijana kwa wakati mmoja ambapo baadhi yao walijihusisha na matendo ya kiuhalifu na wengine walikuwa katika sekta isiyo rasmi kunahitaji mbinu za kimkakati ili kuzuia viashiria vya uhalifu na badala yake kuwatumia kama fursa ya maendeleo.
Serikali imeeleza kuwa mpango huo ulitokana na maombi ya wananchi wenyewe waliotaka kurejea Tanzania kwa hiari.
Kwa hiyo, si sahihi kuwatazama watu hawa wote kama "tatizo" au kuwaita wahalifu.
Hata hivyo, ni sahihi kabisa kujiuliza kuhusu maisha yao baada ya kurejea.
Kunahaja ya mpango endelevu lakini si kwa dhana kwamba vijana hawa ni wahalifu.
Utafiti unaonyesha kuwa kurudi kwa watu, hasa vijana, kunaweza kuongeza shinikizo kwa jamii na kuongeza hatari ya kurudia makosa. Mataifa mbalimbali yamekuwa yakikabiliana na changamoto kama hii kwa miaka mingi. Kama nchi kuna haja ya kuwa na mpango endelevu wa kuwarudisha na kuwaunganisha vijana hawa, hata kama idadi ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya vijana nchini.
Badala yake, mpango unahitajika ili kupunguza hatari za kijamii zinazo weza kujitokeza baada ya kurejea kwa idadi kubwa ya watu waliokuwa nje ya mfumo rasmi wa kiuchumi na kijamii kwa muda mrefu.
Kurejea kwa Watanzania kutoka Afrika Kusini ni jambo la kibinadamu na la kitaifa linalopaswa kuungwa mkono. Raia anaporudi katika nchi yake, anapaswa kupokelewa kama sehemu ya jamii yake na kusaidiwa kuanza upya.
Lakini nyuma ya zoezi hili kuna swali ambalo Serikali inapaswa kujiuliza mapema:
Baada ya kuwarudisha nyumbani, tuna wafanyia nini?
Swali hili si la kisiasa pekee. Ni swali la uchumi, ajira, ustawi wa jamii na, kwa kiwango fulani, usalama wa taifa.
Kuwa mtu ametoka Afrika Kusini hakumaanishi kwamba ni mhalifu.
Kuwa mtu alikuwa akifanya biashara ndogondogo Afrika Kusini hakumaanishi kwamba atakuwa mhalifu Tanzania.
Na hata kama baadhi ya walio rejea wamewahi kuwa na matatizo ya kisheria, haiwezi kuwa sahihi kuwahukumu watu wote kwa kosa la wachache.
Kwa hiyo, mjadala wangu si kwamba:
Huenda alikuwa:
Anakuta:
Hana mtaji, hana biashara, hana ajira, hana makazi yake mwenyewe, na hana mpango wa kazi.
Hapo ndipo swali la sera linapo anza. Kumleta mtu nyumbani ni hatua ya kwanza.
Kumwezesha kuanza maisha upya ndiyo hatua muhimu zaidi.
Utafiti wa Afrobarometer kuhusu vijana Tanzania unaonyesha kwamba asilimia 26 ya vijana walio ulizwa walisema hawana ajira na wanatafuta kazi. Aidha, asilimia 66 ya vijana walisema wangependa kuanzisha biashara zao wenyewe. Utafiti huo pia unaonyesha kwamba vijana wanaona uundaji wa ajira kuwa moja wapo ya maeneo muhimu ambayo Serikali inapaswa kuyawekea kipau mbele.
Tanzania pia ina idadi kubwa ya vijana wanao ingia katika soko la ajira kila mwaka. Afrobarometer ikinukuu makadirio ya World Bank, inaeleza kuwa takribani vijana 800,000 huingia kwenye soko la ajira kila mwaka.
Kwahiyo, vijana 669 (0.083625%) wanao rejea si idadi kubwa ikilinganishwa na nguvu kazi yote ya Tanzania.
Lakinihiyo si hoja.
Tatizo ni mkusanyiko wa mahitaji.
Vijana 669 wanaweza kuwa watu 669 wenye:
Katika jamii yoyote, vijana wanapo kosa:
AJIRA+ KIPATO + MWELEKEO + FURSA
Huongezeka mazingira ya hatari.
Sikwamba kila kijana asiye na ajira anakuwa mhalifu. Lahasha.
Lakiniukosefu wa fursa unaweza kumfanya mtu awe rahisi kuvutwa kwenye:
Kuzuia uhalifu kuna paswa pia kuhusisha kuzuia mazingira yanayo weza kuuchochea.
Hiindiyo maana reintegration ni suala la usalama pia.
Baadhiyao wameishi Afrika Kusini kwa muda mrefu.
Wameona:
Liwe:
Uwe mfumo wa kudumu kwa Watanzania wanao rejea kutoka:
Si kwamadhumuni ya kumchukulia kama mshukiwa. Bali kwa ajili ya kumsaidia.
Mfumo unaweza kurekodi:
Kwamfano:
Badalaya Serikali kutoa fedha bila mpango, ianzishe dirisha maalumu lauwezeshaji.
Mfano:
RETURNEEENTERPRISE FUND
Mfuko huu unaweza kutoa:
Serikaliinaweza kuingia makubaliano na:
Upimwe baada ya: Kuanzia Miezi 3, 6 hadi Miezi 12
Je:
Lakinikuna tofauti kubwa kati ya:
Security Monitoring na Stigmatization.
Mtuakifika Tanzania na kuambiwa:
Lakinitukisema:
Mfano:
Ikiwa katika wilaya fulani vijana 50 waliorudi wamekosa ajira baada yamiezi mitatu, hiyo iwe ishara kwamba:
Mpango haujafanya kazi.
Ikiwa biashara 30 zimefungwa ndani ya miezi sita:
Tatizo linahitaji kuchunguzwa.
Ikiwa vijana wengi wanahitaji mafunzo:
VETA na sekta binafsi zishirikishwe.
Hii inaweza kusaidia Serikali kufanya marekebisho kabla matatizo hayajawa makubwa.
Familia ipewe elimu kwamba:
Wasiwasi usiwe:
Tuanze maandalizi sasa.
Si baada ya tatizo kutokea.
Hili si suala linalo tokea Tanzania tu peke yake. Afrika Kusini imekuwa ikikabiliana na ongezeko kubwa la shughuli za deportation na repatriation. Serikali ya Afrika Kusini iliripoti zaidi ya deportations 109,000 katika miaka miwili ya fedha iliyotangulia hadi Machi2026.
Nakatika 2026, mazingira ya uhamiaji nchini humo yamekuwa magumu zaidi,huku kukiwa na maandamano, vitisho na matukio ya xenophobia dhidi yawahamiaji.
HivyoTanzania haipaswi kuangalia tukio hili kama tukio la mara moja.
Inapaswakujiuliza:
Je, huu ni mwanzo wa mwenendo mpana wa kurejea kwa Watanzania kutoka Afrika Kusini tu au na nchi zingine?
Ikiwajibu ni ndiyo, tunahitaji mfumo wa kudumu.
Tuna sahau kwamba Hapo ndipo kazi rasmi inaanza.
Tunapaswakuhamisha mjadala kutoka:
"Tumewaleta nyumbani."
kwenda:
"Tume wasaidia kujenga maisha mapya."
Kipimocha kweli kiwe:
Ni fursa na changamoto kwa wakati mmoja.
Fursakwa sababu Tanzania inapata watu wenye uzoefu, ujuzi na maarifakutoka nje.
Changamoto kwa sababu baadhi yao wanaweza kurejea bila ajira, bila mtaji na bila mpango wa maisha.
Na hapa ndipo Serikali inapaswa kuwa makini.
Tusisubiri uhalifu utokee ndipo tuanze kujiuliza maswali.
Tusisubirimpaka kijana akose kazi miezi sita, mwaka mmoja, ndipo tumkumbuke.
Tusisubiribiashara yake ifungwe ndipo tumwambie Serikali ipo.
Tusisubirikijana akate tamaa ndipo tuanze kumtafuta.
Kwa hiyo, mapendekezo yangu ni kwamba Serikali itumie zoezi hili kuanzisha National Returnee Reintegration Programme yenye ushirikiano wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Kazi, Wizara yenye dhamana ya Vijana, SIDO, VETA, Halmashauri za jiji, sekta binafsi, taasisi za fedha na mashirika ya kijamii.
Kwawatu 669, hili linawezekana kabisa.
Na kama mpango utafanya kazi vizuri, vijana hawa wanaweza kugeuka kutoka kuwa watu tunao waogopa kuwa wataongeza uhalifu na kuwa wajasiriamali, wafanyakazi, walipa kodi na wazalishaji wanaochangia uchumi wa Tanzania.
Swalila msingi kwa Taifa sasa si:
Bali:
HILO NDILO SWALI AMBALO SERIKALI, BUNGE, WATAALAMU WA AJIRA, SEKTA BINAFSI NAJAMII WANAPASWA KUANZA KULIJADILI SASA.
JE, SERIKALI IMEJIANDAA KWA MAISHA YAO BAADA YA REPATRIATION?
Kwanini kurejeshwa kwa Watanzania kutoka Afrika Kusini kusibaki tu kuwa safari ya kurudi nyumbani, bali iwe mwanzo wa mpango wa ajira, biashara na Reintegration.
Habari rasmi zina onyesha Serikali ya Tanzania imepanga kuwarudisha kwa hiari takriban raia 669 kutoka Afrika Kusini kutokana na hali ya chuki (xenophobia) dhidi ya wageni. Kundi la kwanza la vijana (karibu 173 kutoka KwaZulu-Natal/Durban) walirudishwa mwishoni mwa Agosti 2026 kwa ndege maalum, na mipango iliyopo ni kuwarudisha wengine kutoka miji ya Cape Town (karibu 300) na Johannesburg kufikia jumla ya raia 669.
Wengi wao walikuwa wameishi huko kwa muda mrefu, baadhi wakiwa na ujuzi, elimu au biashara ndogondogo. Kurudi kwao si jambo rahisi wameacha shughuli zao za kijamii, wateja, na maisha waliyo yajenga na sasa yamekatishwa ghafla.
Kwenye mitandao ya kijamii, kulionyeshwa video ya vijana wakiwa kwenye ndege wakirejea nyumbani, Tanzania. Kama ilivyo ada ya Watanzania haswa kwenye mitandao ya kijamii, gumzo likawa kubwa, wengi wakaonyesha wasiwasi wao kuwa hao vijana wanaweza kuongeza wimbi la uharifu, mitaani.
Wasiwasi wao una msingi mkubwa na unagusa eneo nyeti la usalama na maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kurudi kwa idadi kubwa ya vijana kwa wakati mmoja ambapo baadhi yao walijihusisha na matendo ya kiuhalifu na wengine walikuwa katika sekta isiyo rasmi kunahitaji mbinu za kimkakati ili kuzuia viashiria vya uhalifu na badala yake kuwatumia kama fursa ya maendeleo.
Serikali imeeleza kuwa mpango huo ulitokana na maombi ya wananchi wenyewe waliotaka kurejea Tanzania kwa hiari.
Kwa hiyo, si sahihi kuwatazama watu hawa wote kama "tatizo" au kuwaita wahalifu.
Hata hivyo, ni sahihi kabisa kujiuliza kuhusu maisha yao baada ya kurejea.
Kunahaja ya mpango endelevu lakini si kwa dhana kwamba vijana hawa ni wahalifu.
Utafiti unaonyesha kuwa kurudi kwa watu, hasa vijana, kunaweza kuongeza shinikizo kwa jamii na kuongeza hatari ya kurudia makosa. Mataifa mbalimbali yamekuwa yakikabiliana na changamoto kama hii kwa miaka mingi. Kama nchi kuna haja ya kuwa na mpango endelevu wa kuwarudisha na kuwaunganisha vijana hawa, hata kama idadi ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya vijana nchini.
Badala yake, mpango unahitajika ili kupunguza hatari za kijamii zinazo weza kujitokeza baada ya kurejea kwa idadi kubwa ya watu waliokuwa nje ya mfumo rasmi wa kiuchumi na kijamii kwa muda mrefu.
Kurejea kwa Watanzania kutoka Afrika Kusini ni jambo la kibinadamu na la kitaifa linalopaswa kuungwa mkono. Raia anaporudi katika nchi yake, anapaswa kupokelewa kama sehemu ya jamii yake na kusaidiwa kuanza upya.
Lakini nyuma ya zoezi hili kuna swali ambalo Serikali inapaswa kujiuliza mapema:
Baada ya kuwarudisha nyumbani, tuna wafanyia nini?
Swali hili si la kisiasa pekee. Ni swali la uchumi, ajira, ustawi wa jamii na, kwa kiwango fulani, usalama wa taifa.
1. KWANZA: TUSICHANGANYE KUREJEA KWAO NA UHALIFU
Kuna hatari katika mjadala huu ambayo lazima tuepukane nayo.Kuwa mtu ametoka Afrika Kusini hakumaanishi kwamba ni mhalifu.
Kuwa mtu alikuwa akifanya biashara ndogondogo Afrika Kusini hakumaanishi kwamba atakuwa mhalifu Tanzania.
Na hata kama baadhi ya walio rejea wamewahi kuwa na matatizo ya kisheria, haiwezi kuwa sahihi kuwahukumu watu wote kwa kosa la wachache.
Kwa hiyo, mjadala wangu si kwamba:
Mjadalasahihi ni:"Vijana hawa watakapo fika Tanzania wataongeza uhalifu."
Hilo ni swali tofauti kabisa."Je, mazingira ya kiuchumi na kijamii baada ya kurejea yanaweza kuwaweka baadhi yao katika mazingira hatarishi?"
2. TATIZO LINA ANZIA KWENYE MAISHA BAADA YA KURUDI
Fikiria kijana aliyekuwa Durban, Cape Town au Johannesburg kwa miaka kadhaa.Huenda alikuwa:
- Mfanyabiashara mdogo;
- Fundi;
- Dereva;
- Mfanyakazi wa hoteli;
- Mfanyakazi wa ujenzi;
- Mfanyakazi wa dukani;
- Mtoa huduma;
- Au mtu aliyekuwa akifanya biashara isiyo rasmi.
Anakuta:
Hana mtaji, hana biashara, hana ajira, hana makazi yake mwenyewe, na hana mpango wa kazi.
Hapo ndipo swali la sera linapo anza. Kumleta mtu nyumbani ni hatua ya kwanza.
Kumwezesha kuanza maisha upya ndiyo hatua muhimu zaidi.
3.TANZANIA TAYARI INA CHANGAMOTO KUBWA YA AJIRA KWA VIJANA
Hili ndilo linalofanya suala hili kuwa muhimu.Utafiti wa Afrobarometer kuhusu vijana Tanzania unaonyesha kwamba asilimia 26 ya vijana walio ulizwa walisema hawana ajira na wanatafuta kazi. Aidha, asilimia 66 ya vijana walisema wangependa kuanzisha biashara zao wenyewe. Utafiti huo pia unaonyesha kwamba vijana wanaona uundaji wa ajira kuwa moja wapo ya maeneo muhimu ambayo Serikali inapaswa kuyawekea kipau mbele.
Tanzania pia ina idadi kubwa ya vijana wanao ingia katika soko la ajira kila mwaka. Afrobarometer ikinukuu makadirio ya World Bank, inaeleza kuwa takribani vijana 800,000 huingia kwenye soko la ajira kila mwaka.
Kwahiyo, vijana 669 (0.083625%) wanao rejea si idadi kubwa ikilinganishwa na nguvu kazi yote ya Tanzania.
Lakinihiyo si hoja.
Tatizo ni mkusanyiko wa mahitaji.
Vijana 669 wanaweza kuwa watu 669 wenye:
- Familia;
- Watoto;
- Madeni;
- Mahitaji ya makazi;
- Mahitaji ya ajira;
- Mahitaji ya mtaji;
- Na matarajio ya maisha.
4. HATARI KUBWA SI LAZIMA IWE UHALIFU INAWEZA KUWA KUKATA TAMAA
Hapa ndipo mjadala wa usalama unapaswa kuwa wa kitaalamu.Katika jamii yoyote, vijana wanapo kosa:
AJIRA+ KIPATO + MWELEKEO + FURSA
Huongezeka mazingira ya hatari.
Sikwamba kila kijana asiye na ajira anakuwa mhalifu. Lahasha.
Lakiniukosefu wa fursa unaweza kumfanya mtu awe rahisi kuvutwa kwenye:
- Biashara haramu;
- Magenge;
- Utapeli;
- Matumizi mabaya ya dawa za kulevya;
- au shughuli nyingine za uhalifu.
Kuzuia uhalifu kuna paswa pia kuhusisha kuzuia mazingira yanayo weza kuuchochea.
Hiindiyo maana reintegration ni suala la usalama pia.
5. FURSA KUBWA AMBAYO TANZANIA INAWEZA KUITUMIA
Badala ya kuwaona vijana hawa kama mzigo, Tanzania inaweza kuwaona kama rasilimaliwatu.Baadhiyao wameishi Afrika Kusini kwa muda mrefu.
Wameona:
- Mifumo ya biashara;
- Masoko;
- Teknolojia;
- Huduma;
- Mbinu za ujasiriamali;
- Mazingira ya ushindani;
- Na namna biashara zinavyoendeshwa katika uchumi mkubwa zaidi wa afrika.
"Tutawafanyia nini?"
Liwe:
Hapondipo tunabadilisha changamoto kuwa fursa."Tunawezaje kutumia ujuzi na uzoefu walio upata nje ya nchi kuendeleza uchumi wa Tanzania?"
6.PENDEKEZO: SERIKALI IANZISHE NRRP
Ninge pendekeza Serikali ianzishe mpango maalumu wa kudumu ambao unaweza kuitwa:NATIONAL RETURNEE REINTEGRATION PROGRAMME - NRRP
Mpango huu usiwe kwa ajili ya kundi hili pekee.Uwe mfumo wa kudumu kwa Watanzania wanao rejea kutoka:
- Afrika Kusini;
- Ulaya;
- Mashariki ya Kati;
- Asia;
- na nchi nyingine.
7. HATUA YA KWANZA: "RETURNEE REGISTRATION & SKILLS MAPPING"
Kilaanayerejea kwa hiari apewe nafasi ya kusajili taarifa zake za msingi.Si kwamadhumuni ya kumchukulia kama mshukiwa. Bali kwa ajili ya kumsaidia.
Mfumo unaweza kurekodi:
- Elimu
- Ujuzi
- Kazi aliyokuwa akifanya nje
- Uzoefu wa biashara
- Mtaji alionao
- Eneo analotaka kuishi
- Eneo analotaka kufanya biashara
- Mahitaji ya ajira
- Mahitaji ya mafunzo
- Tuna watu wangapi wenye ujuzi wa ujenzi?
- Wangapi wana uzoefu wa biashara?
- Wangapi ni mafundi?
- Wangapi wana uzoefu wa hospitality?
- Wangapi wanaweza kufanya kazi kwenye logistics?
- Wangapi wana uwezo wa kuanzisha biashara?
8. HATUA YA PILI: KUWAPA "RETURNEE STARTER PACKAGE"
Kilamtu anayerejea asiishie kupewa usafiri wa kurudi. Apewe mpango wakuanzia maisha mapya.Kwamfano:
Kwa Wafanya Biashara
- Mafunzo mafupi ya biashara;
- Usajili wa biashara;
- Elimu ya kodi;
- Huduma za SIDO;
- Upatikanaj wa mikopo midogo;
- Kuunganishwa na taasisi za fedha.
Kwa Mafundi
- VETA;
- Certification ya ujuzi;
- Kuunganishwa na makampuni;
- Apprenticeship;
- Zabuni ndogo za ndani.
Kwa Vijana Wasiokuwa na Ujuzi
- Vocational training;
- Digital skills;
- Driving/logistics;
- Hospitality;
- Construction;
- Agriculture;
- Electrical;
- Plumbing;
- Welding
- n.k
9. HATUA YA TATU: "R. E. F"
Hililinaweza kuwa mojawapo ya suluhisho bora zaidi.Badalaya Serikali kutoa fedha bila mpango, ianzishe dirisha maalumu lauwezeshaji.
Mfano:
RETURNEEENTERPRISE FUND
Mfuko huu unaweza kutoa:
- Mikopo midogo;
- Matching grants;
- Vifaa vya kuanzia biashara;
- Mafunzo;
- Mentorship.
10. HATUA YA NNE: PRIVATE SECTOR LAZIMA IHUSISHWE
Hili sijukumu la Serikali peke yake. Sekta binafsi inaweza kuwa mshirikamkubwa.Serikaliinaweza kuingia makubaliano na:
- Kampuni za ujenzi;
- Viwanda;
- Hoteli;
- Kampuni za logistics;
- Supermarkets;
- Kampuni za ict;
- Kampuni za kilimo;
- Kampuni za usafirishaji.
Serikali inaweza kusema:"Jitafutie kazi."
Hii ni approach ya labour-marketmatching."Tuna vijana wenye ujuzi walio rejea; kampuni zipi zinaweza kuwa chukua?"
11. HATUA YA TANO: MENTORSHIP YA MIEZI 12
Hili ni muhimu sana. Usalama wa mpango usipimwe siku ambayo ndege imetua.Upimwe baada ya: Kuanzia Miezi 3, 6 hadi Miezi 12
Je:
- Ana kazi?
- Biashara yake inaendelea?
- Ana kipato?
- Ana makazi?
- Watoto wake wanaendelea na shule?
- Ana changamoto gani?
- Anahitaji mafunzo gani?
12. POLISI WAHUSISHWE
Wawe sehemu ya mpango lakini si kwa mtazamo kuwa hao vijana ni wahalifu. Polisi wanaweza kushirikishwa katika mfumo wa kuzuia uhalifu.Lakinikuna tofauti kubwa kati ya:
Security Monitoring na Stigmatization.
Mtuakifika Tanzania na kuambiwa:
Tayari tumemtenga."Umetoka Afrika Kusini, wewe ni mtu wa hatari."
Lakinitukisema:
Tunamrudishakwenye mfumo wa jamii."Umerudi Tanzania; kama una changamoto ya ajira, biashara, makazi au ushauri, hizi ndizo huduma zilizopo."
13. SERIKALI PIA IFANYE "EARLY WARNING SYSTEM"
Hii sisurveillance ya watu. Ni mfumo wa kutambua matatizo mapema.Mfano:
Ikiwa katika wilaya fulani vijana 50 waliorudi wamekosa ajira baada yamiezi mitatu, hiyo iwe ishara kwamba:
Mpango haujafanya kazi.
Ikiwa biashara 30 zimefungwa ndani ya miezi sita:
Tatizo linahitaji kuchunguzwa.
Ikiwa vijana wengi wanahitaji mafunzo:
VETA na sekta binafsi zishirikishwe.
Hii inaweza kusaidia Serikali kufanya marekebisho kabla matatizo hayajawa makubwa.
14. JAMBO LINGINE MUHIMU: FAMILIA
Hatupaswikuwaangalia wao peke yao. Kijana anaporudi nyumbani anaweza kurejeakwenye:- Familia;
- Mwenza;
- Watoto;
- Wazazi;
- Ndugu.
Familia ipewe elimu kwamba:
Hiiinaweza kupunguza migogoro ya kifamilia, msongo wa maisha na kutengwa."Mtu huyu amerudi baada ya maisha ya nje; anahitaji muda wa kuzoea tena."
15. JE, KUNA SABABU YA KUWA NA WASIWASI KUHUSU UHALIFU?
Ndiyo, lakini kwa namna sahihi.Wasiwasi usiwe:
Huo ni mtazamo usio na ushahidi. Wasiwasi sahihi ni:"Vijana 669 ni wahalifu."
Jibu la sera linapaswa kuwa:"Je, Tanzania ina mfumo wa kutosha wa kuzuia kundi kubwa la watu wanaorejea bila kipato, bila ajira au bila mtaji kuingia katika mazingira ya kiuchumi na kijamii yanayo weza kuongeza vulnerability?"
Tuanze maandalizi sasa.
Si baada ya tatizo kutokea.
16. KUNA SOMO KUTOKA AFRIKA KUSINI
Hili si suala linalo tokea Tanzania tu peke yake. Afrika Kusini imekuwa ikikabiliana na ongezeko kubwa la shughuli za deportation na repatriation. Serikali ya Afrika Kusini iliripoti zaidi ya deportations 109,000 katika miaka miwili ya fedha iliyotangulia hadi Machi2026.
Nakatika 2026, mazingira ya uhamiaji nchini humo yamekuwa magumu zaidi,huku kukiwa na maandamano, vitisho na matukio ya xenophobia dhidi yawahamiaji.
HivyoTanzania haipaswi kuangalia tukio hili kama tukio la mara moja.
Inapaswakujiuliza:
Je, huu ni mwanzo wa mwenendo mpana wa kurejea kwa Watanzania kutoka Afrika Kusini tu au na nchi zingine?
Ikiwajibu ni ndiyo, tunahitaji mfumo wa kudumu.
17.TANZANIA ISIFANYE KOSA LA "SHORT-TERM RESPONSE"
Tatizokubwa la Serikali nyingi Afrika ni kushughulikia tukio, si mfumo.- Ndege imefika.
- Raia wameshuka.
- Wamepokelewa.
- Picha zimepigwa.
- Hotuba zimetolewa.
Tuna sahau kwamba Hapo ndipo kazi rasmi inaanza.
Tunapaswakuhamisha mjadala kutoka:
"Tumewaleta nyumbani."
kwenda:
"Tume wasaidia kujenga maisha mapya."
18. NINA PENDEKEZA KUWE MPANGO WA MIEZI 12
Mwezi 0-1
- Usajili;
- Skills Mapping;
- Mahali Wanapoishi;
- Mahitaji Ya Msingi;
- Familia;
- Ajira.
Mwezi 1-3
- Vocational Training;
- Business Training;
- Job Matching;
- Usajili Wa Biashara;
- Mentorship.
Mwezi 3–6
- Mikopo;
- Vifaa;
- Ajira;
- Incubation ya Biashara.
Mwezi 6–9
- Tathmini ya Kipato;
- Biashara;
- Ajira;
- Changamoto.
Mwezi 9–12
- Tathmini ya Mwisho;
- Biashara Zinazofanya Vizuri Kuongezewa Mtaji;
- Wanaohitaji Msaada Zaidi Kupewa Intervention Maalumu.
19. KIPIMO CHA MAFANIKIO KISIWE "IDADI YA WALIORUDISHWA"
Hili ni jambo muhimu sana. Serikali inaweza kusema:Lakini hicho si kipimo cha mwisho."Tume fanikiwa kuwarejesha Watanzania 669."
Kipimocha kweli kiwe:
- Ni wangapi wamepata ajira?
- Ni wangapi wameanzisha biashara?
- Ni wangapi wana kipato baada ya miezi sita?
- Ni wangapi bado wanahitaji msaada baada ya mwaka mmoja?
- Ni wangapi wameingia kwenye mafunzo?
- Ni biashara ngapi zimeendelea?
HITIMISHO
Kurejeshwa kwa Watanzania kutoka Afrika Kusini hakupaswi kutazamwa kama tatizo.Ni fursa na changamoto kwa wakati mmoja.
Fursakwa sababu Tanzania inapata watu wenye uzoefu, ujuzi na maarifakutoka nje.
Changamoto kwa sababu baadhi yao wanaweza kurejea bila ajira, bila mtaji na bila mpango wa maisha.
Na hapa ndipo Serikali inapaswa kuwa makini.
Tusisubiri uhalifu utokee ndipo tuanze kujiuliza maswali.
Tusisubirimpaka kijana akose kazi miezi sita, mwaka mmoja, ndipo tumkumbuke.
Tusisubiribiashara yake ifungwe ndipo tumwambie Serikali ipo.
Tusisubirikijana akate tamaa ndipo tuanze kumtafuta.
Kinga bora ya uhalifu wa baadaye inaweza kuwa uwekezaji wa leo katika ajira, biashara, ujuzi na matumaini.
Kwa hiyo, mapendekezo yangu ni kwamba Serikali itumie zoezi hili kuanzisha National Returnee Reintegration Programme yenye ushirikiano wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Kazi, Wizara yenye dhamana ya Vijana, SIDO, VETA, Halmashauri za jiji, sekta binafsi, taasisi za fedha na mashirika ya kijamii.
Kwawatu 669, hili linawezekana kabisa.
Na kama mpango utafanya kazi vizuri, vijana hawa wanaweza kugeuka kutoka kuwa watu tunao waogopa kuwa wataongeza uhalifu na kuwa wajasiriamali, wafanyakazi, walipa kodi na wazalishaji wanaochangia uchumi wa Tanzania.
Swalila msingi kwa Taifa sasa si:
"Tume waleta wangapi?"
Bali:
"Tume waandalia maisha gani baada ya kuwasili?"
HILO NDILO SWALI AMBALO SERIKALI, BUNGE, WATAALAMU WA AJIRA, SEKTA BINAFSI NAJAMII WANAPASWA KUANZA KULIJADILI SASA.