Wahenga tujuane hapa..

Wahenga tujuane hapa..

Nimekumbuka nilitembezewaga kichapo na mama aliunga fimbo kama 3 za matunda passion, mbona nilitaja ela zilipo🙆🏽‍♀️
Hata mimi nikitaja mbele ya Mwalimu mkuu 🤣🤣🤣
Noti za shilingi 20,50 na 100 nilificha kwenye malando (majani ya viazi)
 
Mwaka 1993 tukiwa na rafiki yangu siku ya Christmas tukamuibia binti wa watu shilingi 100 ili tukanywe soda na biscuits, ile kesi ilifika home nikapewa dawa yangu ya uhakika.
"Wakati wa ujana wangu mimi baba yenu ,shati dukani Shilingi 6 unapata ,kwa hivi sasa shilingi 6 hata soda hupati" - Maalimu Gurumo - Usia wa baba
 
Eeh hili shairi la zamani linarudisha kumbukumbu nyingi! Mimi nakumbuka ubeti huu: Ndege huyu wa ajabu, hupaa mbali na kwenda, Kwake hana mazibu, hata kama ni mvua, Akiwa na shilingi 200 za Mwinyi, ununue hela ya kutosha, Ndio maisha ya zamani, pesa ilikuwa na thamani! Hahaha hizo shilingi za Mwinyi zilinunua kila kitu! Siku hizi shilingi 200 haina maana kabisa. Watu wa leo hawataelewa hata tulivyokuwa tukipiga story na hizo hela. Kweli utamaduni ulikuwa na utamu wake.
 
Nilimwibia marehemu bibi sh 2000 nilikula wiki nzima na haikuisha nikanunua na saa 😂😂😂

Mwaka 1996 hiyo std 2 mpaka nilikamatwa hela nilikuwa naficha kwenye majani ya viazi vitamu shambani nyuma ya nyumba
Mkuu, kwa sisi gen z, hiyo 2000 mwaka 1996 ilikuwa ya pamoja? Au ndo mkusanyiko wa noti nyingi?
 
Nakumbuka soda yangu ya kwanza kunywa naenda kununua dukani mwenyewe ilikuwa fahari kama sijakosea
Fahari...soda maridhawa sana! Niliiona kwa ufupi sana....mwenzie alikuwa Vimto aisee!

Kuna namna na sisi GenZ tulihusika na life lenu wahenga!0
 
Na wewe siyo mhenga. Wahenga ni Sisi tuliotumia thumuni! Unaijua thumuni wewe? Au ile senti 5 ya samaki sijui alikuwa samaki gani yule mwenye mdomo umechongoka kama sindano!
Ukisikia hasira za...... tijara kwa mvuvi
jibu lake ndiye huyo sasa. MKIZI
 
"Wakati wa ujana wangu mimi baba yenu ,shati dukani Shilingi 6 unapata ,kwa hivi sasa shilingi 6 hata soda hupati" - Maalimu Gurumo - Usia wa baba
hapo sasa, drum, guitor na saxaphone tu. hakuna kudownload biti hapo..
 
Back
Top Bottom