Hata makabila mengine wana hayo magari na maisha mazuri sana, ila wengi wao wakishafanikiwa hawarudi makwao tena hawapapendi, hata watoto wao utakuta wanajitapa kijinga eti ooh unajua mimi asili yangu ni Namtumbo lakini sijawahi kufika, you know even My Dad ame settle hapahapa Dar. Sasa ndio hawa wakifika kwa wachaga wanashangaa nakuweka POST JF. Nilishawahi kufika sehemu moja Moro kwao na jamaa yangu kwakweli nilisikitika sana maana Hadhi na mali walizonazo Dar haziendani na kwao, tena Grandparents wote wapo lakini wanapoishi sasa!!!1 Jamaa akaanza kujibalaguza kwakusema eti Baba yake kawashawishi sana wazee hao kuhamia Dar ila wamegoma. Wachagga wana invest Mjini lakini wanahakikisha wanajenga kwao tena nyumba ya maana na wenzake wakiona mjengo nao wanahakikisha wanajenga na ndio maana kunazidi kuwa pazuri sana. WANA SPIRIT YA MAENDELEO NA ZAIDI WANAPAPENDA SANA KWAO . Tuige kutoka kwao. Makabila yote TZ tungekuwa kama hawa jamaa na makabila ya mbeya na Kagera basi kwa kiasi fulani tusingekuwa hapa. PIA TUACHE KUWAPIGA MAJUNGU ETI SERIKALI INAPAPENDELEA KWAO, WAKATI WAO NDIO WANAOPAPENDA KWAO.