Ripoti ya ziara yangu Kilimanjaro kuufunga mwaka 2020: Wachaga ni watu wa ajabu sana

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,148
UTANGULIZI
Kama nilivyoahidi hapa JF siku chache zilizopita kuwa nitakuja na ripoti kamili ya ziara yangu ya kutembea na kujifunza mkoani Kilimanjaro katika jamii ya kabila la Wachaga wakati wa kwenda kusheherekea sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya. Kila kitu kwa ufupi na ufasaha nitakiweka hapa.

Kwa kipindi cha wiki mbili mfululizo kuanzia tarehe 24 Disemba 2020 niliweka kambi uchagani, niliona mengi mazuri na mabaya, na kwa sehemu nitaeleza hapa.

Katika ripoti yangu hii nitazungumzia mambo kumi muhimu kadhaa ikiwemo Mandhari, Miundo mbinu, Ulevi, Maisha, Matambiko, Familia, Ngono, Maendeleo nk.

1. MANDHARI
Kiujumla nimejionea mazingira ya kiasili ya miti, migomba, mito, vijito yakiwa yamezunguka maeneo ya watu wanapoishi. Wazee na wenyeji wa siku zote, walinieleza kuwa kwa sehemu kubwa uoto wa asili umepotea na unazidi kupotea kwa kasi kubwa kwa kadri siku zinaposogea, huku kampeni ya upandaji miti ni kama imekufa, watu wanakata miti ya asili kwa spidi kali na hakuna kampeni kabambe kuzuia hilo. Maeneo kadhaa kuna watu walisema wanamkumbuka sana Marehemu Reginald Mengi(kuhimiza kupanda miti) na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wa zamani ambaye kwa sasa ni marehemu, Gama (kuzuia ukataji miti). Kwa sasa hakuna tena jemedari katika hilo.

2. MIUNDO MBINU
Wachaga hujali sana miundo mbinu ya kwao. Na jambo la kawaida sana uchagani kukuta watu wameingia gharama zao binafsi kujenga miundo mbinu ya barabara, maji, makaravati, vivuko vya watembea kwa miguu, umeme ili kufika nyumbani kwao, shambani kwao, Kanisani nk.

3. FAMILIA
Misingi mikuu ya kifamilia yaani (Ndoa, Wazazi, Watoto, Matunzo na Makuzi) nimeikuta iko vyema kabisa katika jamii zao. Karibu kila kaya niliyofanikiwa kuingia katika boma lao na kukaa nao, hicho kitu nilikikuta. Kwao maendeleo huanzia kwenye familia zao na huishia kwenye familia zao.

4. ULEVI
Pombe ni utamaduni wa kifahari kwa wachaga. Karibu kila kijiji nilichopita nilikutana na klabu cha mbege. Huko utakutana na waume kwa wake wanakunywa pombe za kienyeji na kisasa, wengine wamechoka na kuchakaa kama mateja, wakinywa pombe, iwe asubuhi, mchana, jioni au usiku. Hichi kitu inasemekana imedumaza nguvu kazi ya kifamilia, na wazee wanasema umaskini umeanza kuzinyemelea kwa kasi ya ajabu kaya kadhaa uchagani kwa sababu ya kuendekeza pombe. Wachaga wanaorudi Disemba ndio imekuwa kama kichocheo (catalyst) ya kukuza utamaduni wa ulevi uchagani. Ni vigumu kumtenganisha mchaga na pombe.

5. MATAMBIKO
Jamii za kichaga zinaamini vizuri tu kwenye mila za jadi(imani za kishirikina!), japokuwa wenyewe hawapendi kabisa kulisema au kuliweka wazi hilo kwa mgeni. Kwa uchunguzi wangu mdogo, ukiondoa kaya za kichaga zilizoshiba imani za kidini (hasa ulokole) ambazo zimeachana na hizo mila, kaya zingine huwezi kuzitenganisha na matambiko. Suala la kuzika, kuchinja, Kisusio, kunywa mbege na jani la sale ni vitu vilivyoficha mambo mengi mnoo kwenye imani za kijadi za kichaga. Inahitaji uwerevu kwa mgeni kuweza kugundua hilo. Binafsi nilipochunguza hayo matambiko sijaona tofauti na ushirikina mwingine wowote uliopo katika makabila mengine.

6. WANAWAKE
Mwanamke ndio uti wa mgongo wa maisha ya kifamilia ya wachaga. Hao viumbe wana uwezo mkubwa sana katika kusaka pesa na kutunza familia huko uchagani. Haijalishi wapi utakwenda uchagani, utakuta mwanamke anasaka pesa na kutunza familia. Jeuri ya mwanamke wa kichaga haiko kwenye pesa aliyonayo mfukoni bali iko kwenye uwezo wa kusaka pesa alionao, iwe kwa haki au kwa hila, mwanamke wa kichaga anasaka pesa tu.

7. NGONO
Kipindi cha Desemba huenda matukio ya ngono holela ndio hushika kasi. Safari za wachaga kurejea makwao Desemba huenda sambamba na kuchepuka kwa wanandoa na wadangaji kutumia fursa. Wahanga huwa ni watu wa jika moja ambao hukutana tena (reunion) baada ya kuwa mbalimbali kwa miaka kadhaa. Kiufupi sana, kwa sasa ngono zembe ipo sana uchagani kipindi cha Desemba na ukimwi umetikisa vilivyo uchagani.

8. ELIMU
Jamii za kichaga zinatumia gharama na nguvu kubwa kuhakikisha watoto wao wanapata elimu ya uhakika na bora. Ni wepesi sana kuona na kuzifuata fursa za kielimu popote pale duniani. Michango ya pesa kifamilia na kiukoo kuwezesha elimu bora ya watoto wao ni jambo la kawaida kipindi cha Disemba. Katika hili wachaga wapo makini kupita maelezo. Tupende au tusipende, wachaga huenda wakaendelea kuwaburuta watu wengine kwenye jamii miaka na miaka hapa Tanzania.

9. UKABILA
Nilichogundua ni kuwa wachaga wanajuana kiukoo na sio kikabila. Wachaga wako katika jamii zaidi ya saba (Rombo, Marangu/Mwika, Kirua, Kibosho, Old Moshi, Uru, Mashame nk) zenye kutofautiana, kukinzana na kubaguana na ndani ya hizo jamii kuna koo kadhaa, na nyingi hazina ushirikiano wa moja kwa moja. Kifupi wachaga sio kikundi kimoja cha kikabila bali vikundi kadhaa vyenye lugha tofauti, tamaduni tofauti na mitazamo tofauti vinavyoishi kuuzunguka msitu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro. Uadui baina jamii mbili tofauti za kichaga kuna mahali ni mkubwa kupita maelezo. Wachaga wamejijengea social classes, hii hupelekea kubaguana na kudharauliana vilivyo. Wengi wanaotoka kwenye poor social classes hawapendi kurejea makwao kipindi cha mwisho wa mwaka (maana hupezwa na kudharauliwa sana). Nilichoweza kugundua ni kuwa rafiki mkuu wa mchaga ni mchaga mwenzake (wa jamii na ukoo wake) na adui mkuu wa mchaga ni mchaga mwenzake vile vile (wa jamii nyingine au ukoo mwingine).

10. MAENDELEO
Misingi muhimu ya kimaendeleo (familia, uchumi, elimu) imesimikwa vyema uchagani. Kinachoendelea kwenye maisha ya kila siku kwa wachaga sio kitu cha kubahatisha au kilichoanza jana bali ni kitu halisi kilichopangika miaka na miaka, kizazi na kizazi.
Koo na kaya nyingi za kichaga zina uhakika wa kuendelea kuwa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine.

ANGALIZO
Huu ni uchambuzi wangu binafsi kulingana na kile nilichokiona uchagani kipindi cha wiki mbili nilichofika kujifunza. Sina lengo la kubeza au kusifia chochote. Mtu mwingine yoyote anaweza kufika Kilimanjaro na kuja na uchambuzi wake. Aliyekwazika naomba anisamehe kwa uchambuzi wangu.
 
Kwakweli ukweli usemwe kuwa hawa watu wanakwenda kwao siyo kusalimia bali asilimia kubwa wanakwenda kuzindikwa,kuzikwa na kutambikwa ili wafanikiwe, wana amini sana kwenye ushirikina ili wapate hela.

Ndio maana hawa watu swala la kuua mtu kisa pesa ni swala jepesi la liko kwenye damu ya hawa wengi.

Kuhusu ulevi hawa watu ni kama wamelaaniwa kwenye pombe maana wakishaona pombe wanachanganyikiwa kabisa na watahakikisha wana maliza pesa yote kwenye pombe na hawa ukikutana nae ambae hanywi pombe ujue hajapata hela tu.

Ukifanya nao biashara jiandae.
 
Kiruuuu... nkiki..?? Ukiacha sifa ya jitihada na kujituma mwingine wote ni Uongo. wooi!! Acha nipitie kwa mama Mushi nikapate chubuku moja la mbege umeshanikera maiyakooo!

Munishi, massawe, Kina chuwa, kimario, Kimaro, Wakina Okama ocho yaadi skia hii mbusi inachoongea.
 
Kwakweli ukweli usemwe kuwa hawa watu wanakwenda kwao siyo kusalimia bali asilimia kubwa wanakwenda kuzindikwa,kuzikwa na kutambikwa ili wafanikiwe, wana amini sana kwenye ushirikina ili wapate hela.

Ndio maana hawa watu swala la kuua mtu kisa pesa ni swala jepesi la liko kwenye damu ya hawa wengi.

Kuhusu ulevi hawa watu ni kama wamelaaniwa kwenye pombe maana wakishaona pombe wanachanganyikiwa kabisa na watahakikisha wana maliza pesa yote kwenye pombe na hawa ukikutana nae ambae hanywi pombe ujue hajapata hela tu

Ukifanya nao biashara jiandae.
Tulia wewe, endelea kula matoke hapo Bukoba
 
Kwakweli ukweli usemwe kuwa hawa watu wanakwenda kwao siyo kusalimia bali asilimia kubwa wanakwenda kuzindikwa,kuzikwa na kutambikwa ili wafanikiwe..... wana amini sana kwenye ushirikina ili wapate hela.
Punguza chuki utakufa kwa kiharusi bwana mdogo. Hizo sifa ulizosema wewe zingekuwa za kweli hata mleta mada asingepoteza muda wake kwenda Uchagani kutafiti, Wachaga kuna mambo mengi mazuri ambayo makabila mengine wanaweza kujifunza kutoka kwao, hata wewe usione aibu kujifunza kutoka kwao.
 
Kwa ngono utakuwa umeikuta Sanaa Marangu. Ulichoacha ni kwamba wachaga wanaongoza kwa single mothers. Sababu ya ngono zembe!

Source: Maisha Forum 2017
 
Wewe isembo sikiliza.

Kuna mambo yapo kwa kila jamii naweza kusema ni ya ya mtu. Mfano Uzinzi

kuna mambo hawa jamaa ni unique kwao ukweli usemwe.
.
halafu hapo kwenye vilabu vya mbege umekosea.
Kila baada ya kaya 5 hukosi mbege
 
Back
Top Bottom